Serikali kuna vitu inajitakia

Serikali kuna vitu inajitakia

Leverage

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2021
Posts
2,125
Reaction score
3,150
Nimesikia watumishi waliotumbuliwa jiji la DSM. Lakini hebu tujiulize Afisa biashara wa halmashàuri/jiji mwenye degree salary in laki 7.1 akikatwa inabaki laki 5. Afisa huyu mmoja anakusanya zaidi ya milioni 500 kwa mwaka. Kwa hali ya kawaida mnamuweka majaribuni.

Mbona TRA na taasisi nyingine mnawalipa vizuri? Kwanini halmashauri mishahara duni?

Take home laki 5 inaishia kwenye nauli na kodi ya nyumba tu.
 
Mpaka leo sijajua kwanini viwango vinatofautiana yaani wa halmashauri na taasisi ingine
 
Walau salary itosheleze mahitaji muhimu hata kama sio kubwa. Hiyo hela ya huyo afisa kwa taasisi nyingine hata dereva hamkuti. Njaa ikizidi maadili yanaondoka
Kuongeza mishahara hakuwezi kuizuia tamaa ya mtu kwenye suala Zima la upigaji

Ni sawa na umuhonge Sana mwanamke malaya ukitegemea pesa itamtuliza, hatakusaliti

Kuzuia Upigaji kunaongozwa na uzalendo wa mtu pamoja hulka binafsi ya kujizuia tamaa.
 
Walau salary itosheleze mahitaji muhimu hata kama sio kubwa. Hiyo hela ya huyo afisa kwa taasisi nyingine hata dereva hamkuti. Njaa ikizidi maadili yanaondoka
Watu wangefahamu majukumu ya driver akiwa na Boss wake, kuanzia safari mpaka anapopaki gari kupumzika, wangekua na heshima sana na drivers
 
Mpaka leo sijajua kwanini viwango vinatofautiana yaani wa halmashauri na taasisi ingine
TTCL kila mwaka hasara lakini Ilala, Kinondoni, Temeke kila mwaka wanakusanya bilioni kadhaa Ila angalia mishahara yao kulinganisha na ttcl
 
Back
Top Bottom