Serikali kupanga bei kikomo ya Saruji kwa kila Mkoa

Serikali kupanga bei kikomo ya Saruji kwa kila Mkoa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ameiagiza Wizara ya Viwanda na Biashara ikamilishe utaratibu wa kuwa na bei kikomo ya saruji ili kuuwezesha kila mkoa kujua bidhaa hiyo inapaswa kuuzwa kwa bei gani kwa nia ya kuondoa upandishwaji holela unaofanywa na wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo Desemba 7, 2020, wakati akizungumza na wakuu wa mikoa, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Maafisa Biashara wa mikoa, mawakala wa saruji walioko mikoani na wakurugenzi wa viwanda vya saruji, kikao ambacho kimefanyika kwa njia ya video.

"Mfano saruji inazalishwa Tanga au Dar es Salaam, halafu Morogoro inauzwa kwa Tsh 28,000, sasa Kigoma itauzwaje lazima kuwe na bei kikomo", amesema waziri Mkuu.

Aidha Waziri Mkuu meongeza kuwa suala hilo halihitaji kuundiwa bodi kwa sasa, kwani vyombo vya kusimamia biashara vipo, wizara husika ipo, hivyo amewataka wahusika wote wahakikishe wanasimamia suala hilo kikamilifu ili kuwawezesha wananchi kupata bidhaa hiyo kwa bei nafuu.
 
Wanajichekesha tu.sukari yenyewe washashindwa mpaka sasa tunanunua kwa 3000
 
Wamemfanyia figisu Dangote mpaka ameamua kufunga kiwanda halafu leo wanakuja na ngonjera.
 
Nakumbuka kwenye kampeni za uchaguzi mkuu wa 2010, Dr. Wilbrod Slaa aliyekuwa mgombea urais wa CHADEMA alikuja na sera ya kuondoa nyumba za tembe kote nchini kwa kuhakikisha sementi inashuka kutoka bei ya wakati ule ya sh. 17'500 hadi sh. 5'000 kwa mfuko.

Ingawa Dr. Slaa hakushinda, lakini angalau tumshukuru JK kwa kutekeleza sera hii ya "wapinzani" kwa kufanya kila aliloweza kuhakikisha bidhaa hii muhimu kwa ujenzi wa taifa inashuka bei hadi sh. 10'000 kwa mfuko. Aliweza kutekeleza sera hii kwa "kuwavutia" wawekezaji kuanzisha viwanda vipya vingi kama vile Nyati, Camel, Dangote n.k.

Kinyume chake serikali ya Magufuli ilipoingia madaraka ikaja na sera za kupambana na "wapiga dili" (wawekezaji walipewa nafuu na JK) na matokeo yake bei ya bidhaa hii ikaanza kupanda hadi sh. 28'000 kama anavyosema mwenyewe Waziri Mkuu.

Kiufupi ni kwamba sera za zerikalinya Magufuli si rafiki kwa wawekezaji, balinzinasababisha matatizo na pale inapojaribu kutatua haifanikiwi bali husababisha matatizo zaidi.

Leo WM anafikiria kuanzisha bodi ya sementi kudhibiti bei lakini akili inakataa. Yaani ni kama vile hajui kilichopelekea bei kupanda mara dufu, bali maarifa yake yamegota na anaona namna pekee anayodhani kuwa ni suluhisho ni kupanga bei elekezi kwa kila mkoa. Yaani WM haoni kuwapa nafuu wawekezaji kama alivyofanya JK ili waanzishe viwanda kwenye kila mkoa kunaweza kupunguza bei ya bidhaa hizi.

Ukweli ni kwamba kupanga bei elekezi hakutapunguza bei na kufikia sh. 14'000 bali ni namna fulani ya kukubali kupanda kwa bei ila tu upandaji huo wa bei kusifanane katika mikoa yote. Kama sementi Morogoro inauzwa sh. 28'000, basi Dar iuzwe kwa sh. 25'000 na bila shaka Dangote Cement kutoka Mtwara itauzwa Kigoma sh. 48'000 na hapo serikali itajisifu imedhibiti bei. Yaani ni tatitizo juu ya tatizo.
 
Kinachonifuraisha kwa serikali hii ni kujifanya wanaweza kudhibiti mfumuko wa bei, kumbe hamna lolote[emoji23]
Yan ni sawa na kibogoyo aliyekosa meno yote ya kutafunia akabakisha ya mbele tu, alafu anatamba kutafuna mifupa.

Kwa nchi hii, ukiona bei ya bidhaa fulani inapanda kwa kasi, jua imeadimika. Full stop! Hawa wajinga kuja na vitisho kwa wafanyabiashara ni kujifanya tu waonekane wanawajibika, lakini hawana la kuzuia. Mifano tunayo mingi.

Kitu pekee ambacho wamekuwa wakiwahadaa wananchi ni kujifanya wanaweka bei elekezi ambayo mara nyingi ndio bei ya mfanyabiashara[emoji1787] alafu wanajifanya kutishia OLE WAKE ATAKAYEUZA ZAIDI YA BEI HIYO[emoji2957]

Wajinga sana! Kwa nini wasirudishe bei ya awali km kweli wanaweza![emoji35]
Na sisi tulivyokuwa wajinga tunashangilia[emoji848]

Ukibisha bisha, lakini huu ndio ukweli wenyewe. Viongozi wetu hawana meno inapokuja ishu ya mfumuko wa bei, na hapa ni bidhaa za ndani tu, sijui ikiwa za kutoka nje itakuaje[emoji2960]

Watatujibu SOKO LA DUNIA NDIO CHANZO[emoji1787]
 
Back
Top Bottom