Serikali kupitia simu za mkononi, inaweza kukusanya fedha na kuanzisha Mfuko(Fund) wa kugharamia Bima ya Afya na Elimu ya Juu kwa Watanzania wote

Mmmh[emoji19][emoji2955],

Iko very indirectly.
Kwa kawaida,unapokuja na wazo au kitu kigeni,watanzania huwa ni wagumu kukielewa/kukipokea na huchukua muda kukikubali na kukizoea kwahiyo sikushangai.
 
Mkuu tatizo nchi watu wana roho mbaya,wivu,wezi na wanakula hadi rambi rambi.Ingekuwa sio hivyo tungekuwa mbali sana kama taifa
 
Yaani mnawaza kuwanyonya wananchi tu sio...
 
Yaani mnawaza kuwanyonya wananchi tu sio...
Watanzania kwa mentality hizi,tutabaki kuwa masikini na kubaki nyuma.

Hiyo mia tano kwa mwezi unaweza kuiona ni nyingi, ila jiulize unatumia kiasi gani kwenye kununua airtime za kawaida au unatumia kiasi gani kunywa pombe au kununua vitu kama soda na vitu vingine vya aina hiyo kwa siku.
 
... halafu hao hao wanaenda kuzibadilisha matumizi. Zitaelekezwa kwenye manunuzi sijui ujenzi wa nini sijui a lot of white elephant projects. Zitatumika kumtukuza bwana yule na genge lake. Zitawekewa vikokotoo na kila aina ya mizengwe ili watu wakose au wapunguziwe haki zao.

Mara hii tumesahau wazee wetu wanavyoteseka kupata haki zao hifadhi ya jamii? Wazo zuri ila sio chini ya mboga mboga kwa kweli!
 
Dah!.. gharama za mawasiliano zitaongezeka likitekelezwa hili itabidi hata hizo vocha ziuzwe 600 au 700 badala ya 500.
 
Hiyo ni Bima kwa ajili ya Afya yako na inaweza isiwe lazima.Kumbuka watanzania wengi hawana Bima ya Afya na wako watu wanakufa kwa kukosa fedha za matibabu.Sasa kipi bora?
Najaribu kufikiria mtu achangie sh. 6000 kwa mwaka ( 500×12) na atibiwe "bure" wakati wowote atakapougua.....!! Aisee kweli bima ni mchezo wa kamali....!!
 
Kwa kawaida,unapokuja na wazo au kitu kigeni,watanzania huwa ni wagumu kukielewa/kukipokea na huchukua muda kukikubali na kukizoea kwahiyo sikushangai.
Kwa mtizamo wangu suala la jero hero Ni usumbufu, Kama zilivyofutwa road license zikaingizwa kwenye mafuta, Kama ilivyoanzishwa RDL railway development Levy on importation, ianzishwe Kodi ya bima ya lazima, na mfuko maalum wa kulea WATOTO walio mazingira hatarishi.ikiwa utakuwa 3% ya airtime charge maana yake ukiweka jero Kila siku kwa mwezi utachangia 450, Sasa hapo wapi watakoutumia mpaka 300,000 huyu atanikuta kachanhia 9000.
Ukweli Ni kwamba muda mwingi tunaotumia kwenye simu sio for economic productions, mostly for social reasons
 
Sipingi wazo lako mkuu ila najaribu kufikiri tu, kwa ikivyo sasa, NHIF inakusanya kwa uchache kabisa sh 54,000 kwa mwaka, na mpaka sh 1,500,000 kwa kiwango cha juu, sasa kwa idadi ile ile ya wachangiaji, inashindwa kutoa huduma ya afya kwa ubora unaostahiki, unadhani nini kinawashinda hawa wa sasa na kipi cha tofauti kitafanyika kwa hili wazo?

Hifadhi ya jamii ni moja ya mifano ya kuonesha kuwa, ilimradi utahusisha serikali na uendeshaji wa wazo lenyewe, basi mkwamo hauepukiki.

Na kuna mdau ameuliza kama takwimu ya wamiliki wa simu iko sawa? Na akasema kama iko sawa, inabidi ufanyike udadisi, kwakuwa asilimia 50 ya idadi ya watu wa TZ amesema ni watoto chini ya 18, ambapo TZ wanasema tuko takribani milioni 60.

VAT, PAYE na nyinginezo zitoshe kufanya jambo hilo. Tuanze na wale wenye exemption za kodi na wafananao, tuone tutapata ngapi toka maeneo hayo kisha tukimalizana na loose ends zote, ndo tufukirie kumkamua huyo ng'ombe anayekaribia kutoa damu.
 
Tujaalie bima hiyo iwe ni kwa wazee na watoto pekee. Ambapo idadi hao ni kama watu mil 30. Kwa bil 240 maana yake kila mfaidika analipa shs 8000 kwa mwaka. Hakuna bima ya afya ya kiasi hicho. Kwa Leo ninatofautiana Na wewe
 
Tembo,Simba mlima Kilimanjaro upo tuu wazungu wanataka walipie waangalie ninyi mmeweka Kodi kubwa kwa magari wanayopanda kuangalia wanyama wanaishia kupata magari mabovu na wakisimuliana hawarudi tena baada ya kupunguza Kodi ya Land Cruiser ili kuboresha mazingira mnataka tena kujibana hata ninyi msipigiane simu vocha tuu zina VAT bado hujaamisha fedha...
 
Salary Slip
Your idea is superb! Yaani kuna watu wengine hata hawana uwezo wa kugharmia matibabu. Ukiangalia kipindi cha Mimi na Tanzania kila wiki J4 kinachoendeshwa na Hoyce Temu ITV, utasikitika sana. If implemented, your ides could save lives of people. Idea hii inabidi iwafikie kwa haraka sana Mh. Ndugulile na Mh. Waziri wa Afya. Ninadhani pia kuwa wamo humu jukwaani. Au basi imfikie hata mtani wangu wa kuibiana ng'ombe. Mh. Dr. Mollel
 
Serikali inakusanya pesa nyingi kutoka vyanzo vingi ilivyonavyo lakini bado wazo lako halijawahi kufikiwa.. Pili katika watu milioni 40 sio wote kwao 500 ni fedha isiyo na madhara, wapo watu hawaweki hela kwenye simu mpaka line inafungiwa..
Angalau nusu ya hao million 40 ni uhakika kuwa 500 haiwezi kuwa na madhara kwao. Hata nusu tu ya watu hawa inatosha kabisa kwa wazo hili la Salary Slip kuwa implemented. Kumbuka pia kuna watu wengine wenye ukwasi wanaoweza wakawa wanachangia mfuko huu kwa hiari, wengine wana uwezo wa kutoa hata TZS Billion moja, au vimillion kadhaa, kwa mfano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…