Serikali kupitia simu za mkononi, inaweza kukusanya fedha na kuanzisha Mfuko(Fund) wa kugharamia Bima ya Afya na Elimu ya Juu kwa Watanzania wote

Actually ukifanya sensa leo unaweza ukagundua kuwa pengine hata tumeshavuka million 65!
 
Azan Zungu nae ni CHADEMA?
 
Azan Zungu ametoa wazo kama langu ingawa mimi sikupendekeza iwe ni lazima bali iwe hiari kwa maswala ya Bima na kwa watakaokuwa tayari kuchangia.

Labda pia alisoma huu uzi.
Nakuombea huko mbele ya safari uje uwe Mbunge, au hata Waziri wa Afya
 
Ukiweka tozo kama hiyo inabidi TRA, TCRA na mamlaka zingine ziache kuzichaji mashirika haya tozo zake ili waweze kushusha gharama za uendeshaji na bei za huduma ziwe nafuu.

Ila haitawezekana kwa akili za hawa wanasiasa wanaojiita viongozi maana wanahisi wao wapo sahihi kuliko mtu yoyote...
 
Mkuu mbona sasa hivi uko mstari wa mbele kupinga tozo
 
Leo wanatangaza kugharamia matibabu ya Prof. Jay ili wapate political milleage na sio kuja na suluhu ya kudumu kuhusu Bima ya kueleweka na endelevu kwa kila mtanzania.

CCM ni mzigo kwa watanzania.
 
Halafu watu wanamlaumu president kumbe haya mawazo yametoka humuhumu kwa wanaJF wenzetu.

Mtatuua na hizi Kodi jamani
 


Hizi ni pesa za watu sio za serikali! Inabidi tuache utamaduni wa kufikiria pesa za simu ni za serikali. Pesa hizi ndiyo tunatumia pesa za watoto kwenda shule hivyo makato makubwa maana yake ni kupunguza pesa kwenye mzunguko na kupeleka kwenye bima kwanini watu wapewe bima na serikali!! . Tayari kuna makato na makato hayatakiwi kuwa makubwa kiasi cha kufanya wananchi warudi kitumia njia za posta na mabasi kituma pesa inabidi tuwe makini na tuache biashara ziendelee. Tuongeze vipato kwa kuongeza wawekezaji, kazi, uzalishaji na sio kuongeza makato kwenye uchumi mdogo. Mzunguko wa pesa ni mdogo bank zina riba za juu sana hivyo hakuna pesa za kutosha kwenye mzunguko. Nchi zilizoendelea wana mikopo na riba za chini hivyo watu wanachukua mikopo nafuu na kuongeza mzunguko wa pesa.
 
Bima ni yako na hulazimishwi. Wewe ona gharama ila siku yakikkuta, ndio utajua kuwa Bima ni muhimu.

Prof. Jay amehitaji milioni 20 na amebahatika kupata milioni 22.Kumbuka huyu alikuwa mbunge na usisahau ni mtu maarufu tangu zamani. Sasa jiulieze yakukute wewe nani atakuchangia milioni 20?Si utakaa tu unasubiri kufa.

Tambua watumishi wa umma wankatwa makato ya lazima kwa ajili ya Bima ya Afya tena hela nyingi tu kulingana na mshahara(kwa asilimia).

Watanzania mkikaa baa, mnatumia hela nyingi kwenye pombe na anasa nyingine bila kusahau mambo kama kubeti, n.k, ila mkiambiwa mchangie kwa hiari Bima kwa ajili ya matibabu yako, unaona gharama. Sisi watu wa ajabu sana.

Jiuluze ni kwani hata vigogo wanaostafu serikalini bado baadhi yao wanaomba msaada wa serikali kugharamia matibabu yao?

Tuache mentalily za kijinga kuhusu afya zetu. Isitoshe nimesema hii ni hiari na sio lazima.

Tukumbuke hata misaada tunayopewa na mataifa makubwa ni kodi na tozo wanazotozwa raia wa nchi hizo.
 
Khee

You mean tozo nyingine juu ya tozo ya miamala na kodi zinazotozwa makampuni ya simu?

Kwamba mawasiliano yawe ghali Tanzania kuliko nchi yoyote duniani?
 
Khee

You mean tozo nyingine juu ya tozo ya miamala na kodi zinazotozwa makampuni ya simu?

Kwamba mawasiliano yawe ghali Tanzania kuliko nchi yoyote duniani?
Sijui kama umesoma hii mada na kuelewa.

Halafu watu mnaopinga ndio nyinyi ambao ndugu zenu huko vijijini wakiomba msaada wa matibabu, mnaishia kuwasimanga na kuwaona ni mzigo, huku kila siku mnachangia harusi! Ajabu sana!

Kama hatuna utaratibu/utamaduni wa kuweka akiba ya fedha kugharamia dharura, iweje tuone umuhimu wa kuwa na bima ya afya? Sio kosa lako bali ni utamaduni mbovu tulioachiwa na wazee wetu.
 
Si mpaka niugue ya nini kutajirisha watu wakati maisha mafupi haya
Tozo unatoa hela, ila nafikiri ukiiugua,unatibiwa bila kutoa hela.Si ndio?
Tell him. kila siku anapiga kelele humu ooh serikali ya kijambazi na bado anatoa wazo la kuwakabidhi mabilion ya pesa
Kwamba tuisadie ccm wawe na hela nyingi zaidi za kufanya uhalifu kwa raia wa nchi hii?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…