Serikali kupitia TRA pitieni Mapungufu ya Kikokotoo cha Kukadiria Ushuru wa Kuingiza Magari used

Kila nchi zina policy zake, ila sisi ni moja ya nchi tulio na gharama kubwa ya kuimport gari.

Kenya hatupishani sana ila Uganda wako chini sana.
Kenya gari ya mwisho kuingiza ni ya 2017 (8yrs) mwakani inakuwa mwisho 2018.. nje ya hapo haiingii labda ipite tu (IT). Ushuru hautofautiani sana but ni cheaper for the same YOM compared to us (kwa magari madogo)
 
hapana sio kweli hao uliowataja hawawezi nunua ist ni sisi wenyewe hoja ya jamaa ni kwamba mfano unakuta bei ya gari ya 2005 ni 5m ila kodi ni 10m jumla 15m hoja ya mwamba ni kwamba kwa gari ya 2020 mfano iwe 8m afu kodi iwe 3 au 5 ambapo unapata 11m au 13m faida ni kwamba tutapata gari latest kwa bei rahisi lakini kwa sasa gari ya 2020+ kodi yake si chini ya 20m kwa hiyo ist afu bei ya gari unakuta dolla 4500 au 6000
 
Kodi ipo kwenye sheria, TRA anatekeleza tuu, hapo ni kushauri wabunge walete kitu chenye nafuu
 
Hii ni kweli

Imagine unaagiza gari 15M


Ushuru kikokotoo kinapiga 12m
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…