Serikali kurejesha hoteli zake zinazoendeshwa na sekta binafsi ili kuboresha huduma

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amesema Serikali imejipanga kuboresha huduma kwa watalii katika nyanja mbalimbali ili kuvutia watalii wengi zaidi ikiwa ni mkakati wa kuwafanya watalii hao kuongeza siku za kukaa nchini na hatimaye kukuza pato la Taifa.

Amesema moja ya mkakati wa Serikali ni kuboresha huduma za malazi kwa watalii kwa kuzirejesha hoteli za wizara ambazo zinaendeshwa na sekta binafsi ambazo kwa ujumla wake hazifanyi vizuri.

Masanja amesema Serikali inaendelea mikakati ya kuhakikisha hoteli hizo mara baada kurejeshwa zinakuwa kinara kwa kutoa huduma bora kwa watalii.

========

Hizi hoteli ni zipi? Pili sekta binafsi ichemke Serikali ndio wataweza! Au watatumia kodi zetu kuziendesha?
 
Kila siku tunaambiwa ile Royal Tour ilizaa matunda ili wa-justify zile bilioni kadhaa walizotumia kucheza ile filamu walizopata toka kwa yule aliyewafadhili, kumbe hakuna ukweli wowote.

Naona Serikali itaenda kutoa ruzuku kwa hizo hoteli ili ziweze kujiendesha, kama walivyofanya kwa TTCL na ATCL hali yao ilivyokuwa mbaya, ni mwendo wa kutumia pesa za walipa kodi kufufua marehemu.
 
Kama hadi sekta binafsi imeshindwa kuziendesha zifanywe hostel tu, chuo cha ufundi au shule ya boarding. Hakuna biashara ya Hotel hapo, ni Serikali itaenda kutapanya tu pesa za walipakodi. Serikali haitakaa iwe na ufanisi kuliko sekta binafsi katika biashara ya Hotel.
 
Kwa sababu lazima wakubwa waibe na zifilisike
 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amesema Serikali imejipanga kuboresha huduma kwa watalii katika nyanja mbalimbali ili kuvutia watalii wengi zaidi ikiwa ni mkakati wa kuwafanya watalii hao kuongeza siku za kukaa nchini na hatimaye kukuza pato la Taifa.

Amesema moja ya mkakati wa Serikali ni kuboresha huduma za malazi kwa watalii kwa kuzirejesha hoteli za wizara ambazo zinaendeshwa na sekta binafsi ambazo kwa ujumla wake hazifanyi vizuri.

Masanja amesema Serikali inaendelea mikakati ya kuhakikisha hoteli hizo mara baada kurejeshwa zinakuwa kinara kwa kutoa huduma bora kwa watalii.

========

Hizi hoteli ni zipi? Pili sekta binafsi ichemke Serikali ndio wataweza! Au watatumia kodi zetu kuziendesha?
Nadhani kuna mengi nyuma ya pazia mmenikumbusha aliyenunua kiwanda halafu akakitumia kufugia mbuzi
 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amesema Serikali imejipanga kuboresha huduma kwa watalii katika nyanja mbalimbali ili kuvutia watalii wengi zaidi ikiwa ni mkakati wa kuwafanya watalii hao kuongeza siku za kukaa nchini na hatimaye kukuza pato la Taifa.

Amesema moja ya mkakati wa Serikali ni kuboresha huduma za malazi kwa watalii kwa kuzirejesha hoteli za wizara ambazo zinaendeshwa na sekta binafsi ambazo kwa ujumla wake hazifanyi vizuri.

Masanja amesema Serikali inaendelea mikakati ya kuhakikisha hoteli hizo mara baada kurejeshwa zinakuwa kinara kwa kutoa huduma bora kwa watalii.

========

Hizi hoteli ni zipi? Pili sekta binafsi ichemke Serikali ndio wataweza! Au watatumia kodi zetu kuziendesha?

Wakifanya hivyo tutarudi nyuma sana kiuchumi, Serikali isijihusishe na biashara, hizo hoteli zilikufa sababu ya uendeshaji mbovu. Fedha nyingi zilikuwa zinaibiwa na watendaji kiasi ambacho kilipelekea kufungwa kabisa hivyo kuzirudisha ni kurudi tena kule kule. Mimi nashauri kama wanaoendesha wameshindwa wanyang'anywe ili wapewe wengine.
 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amesema Serikali imejipanga kuboresha huduma kwa watalii katika nyanja mbalimbali ili kuvutia watalii wengi zaidi ikiwa ni mkakati wa kuwafanya watalii hao kuongeza siku za kukaa nchini na hatimaye kukuza pato la Taifa.

Amesema moja ya mkakati wa Serikali ni kuboresha huduma za malazi kwa watalii kwa kuzirejesha hoteli za wizara ambazo zinaendeshwa na sekta binafsi ambazo kwa ujumla wake hazifanyi vizuri.

Masanja amesema Serikali inaendelea mikakati ya kuhakikisha hoteli hizo mara baada kurejeshwa zinakuwa kinara kwa kutoa huduma bora kwa watalii.

========

Hizi hoteli ni zipi? Pili sekta binafsi ichemke Serikali ndio wataweza! Au watatumia kodi zetu kuziendesha?
Wafikirie vizuri waache tamaa, taasisi na biashara zote zinazoendeshwa na serikali huishia kufanya vibaya na kufa, mifano ni mingi ikiwa ni pamoja na ATCL, ITAKUFA HATA KABLA YA KUISHI!
 
Wajiulize kwanza mashirika yanayomilikiwa na serikali yakoje kibiashara,halafu wajiulize kama sekta binafsi wameshindwa kuziendesha wao serikali wana maajabu gani,wataalii ni watu wanaoangalia quality katika kila kitu.

Wageni watakutana na mabuibui yametanda vyumbani humo,wahudumu uniform zimepauka watakimbia tu
 
Kila siku tunaambiwa ile Royal Tour ilizaa matunda ili wa-justify zile bilioni kadhaa walizotumia kucheza ile filamu walizopata toka kwa yule aliyewafadhili, kumbe hakuna ukweli wowote.

Naona Serikali itaenda kutoa ruzuku kwa hizo hoteli ili ziweze kujiendesha, kama walivyofanya kwa TTCL na ATCL hali yao ilivyokuwa mbaya, ni mwendo wa kutumia pesa za walipa kodi kufufua marehemu.
Serikali ya awamu ya tano tu ndio ilikuwa inasema ukweli mkuu
 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amesema Serikali imejipanga kuboresha huduma kwa watalii katika nyanja mbalimbali ili kuvutia watalii wengi zaidi ikiwa ni mkakati wa kuwafanya watalii hao kuongeza siku za kukaa nchini na hatimaye kukuza pato la Taifa.

Amesema moja ya mkakati wa Serikali ni kuboresha huduma za malazi kwa watalii kwa kuzirejesha hoteli za wizara ambazo zinaendeshwa na sekta binafsi ambazo kwa ujumla wake hazifanyi vizuri.

Masanja amesema Serikali inaendelea mikakati ya kuhakikisha hoteli hizo mara baada kurejeshwa zinakuwa kinara kwa kutoa huduma bora kwa watalii.

========

Hizi hoteli ni zipi? Pili sekta binafsi ichemke Serikali ndio wataweza! Au watatumia kodi zetu kuziendesha?
hizi ni kadabra kadahhh tu...si ajabu lengo ni kuzirudisha kisha wauziane wao au wao ndiyo wachukue tenda za kusupply katika hotel hizo
 
Back
Top Bottom