Serikali kurejesha hoteli zake zinazoendeshwa na sekta binafsi ili kuboresha huduma

Serikali kurejesha hoteli zake zinazoendeshwa na sekta binafsi ili kuboresha huduma

Huo ufanisi wa kuziendesha kwa tija utoke wapi mifano iko wazi mashirika ya umma mengi yanaendeshwa kwa hasara (Serikali kuyapatia pesa za walipa kodi) Naibu Waziri sio mgeni nchini hio kauli ameitoa akiwa timamu kabsa na anao uhakika wa anachokisema?
 
Arusha hotel
Dodoma hotel
Mwanza hotel
Zipo zingine za upande wa pili...

NB
Taarifa hii ina weza kuwa sio sahihi, ni ya kufikirisha
Arusha hotel haijawahi kuwa ya serikali ila nayo na Mt Meru Hotel zina hali mbaya sana
 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amesema Serikali imejipanga kuboresha huduma kwa watalii katika nyanja mbalimbali ili kuvutia watalii wengi zaidi ikiwa ni mkakati wa kuwafanya watalii hao kuongeza siku za kukaa nchini na hatimaye kukuza pato la Taifa...
Huyu naibu waziri inafaa atumbuliwe upesi.
Serikali kuendesha biashara yenye ushindani mkubwa kama hoteli Kwa ufanisi ni ndoto, haiwezekani, na mifano ni mingi na wanaifahamu
 
Kama hadi sekta binafsi imeshindwa kuziendesha zifanywe hostel tu, chuo cha ufundi au shule ya boarding. Hakuna biashara ya Hotel hapo, ni Serikali itaenda kutapanya tu pesa za walipakodi. Serikali haitakaa iwe na ufanisi kuliko sekta binafsi katika biashara ya Hotel
Sio kwamba hoteli hizo za serikali zinazoendeshwa kwa ubia na sekta binafsi zinapata hasara. Ukweli ukifanyika ukaguzi na taasisi yenye uadilifu utakuta wabia wa serikali sekta binafsi ndio wanapata faida huku wakiweza kuionyesha serikali kuna hasara. kwa lugha rahisi ni kwamba kuna ufisadi mkubwa unafanyika ili sekta binafsi waendeshe hoteli kama yao na huku wawekezaji ambao ni umma kupitia serikali yao wakiambulia nunge. vigogo wahusika serikalini kupitia wakuregenzi kutoka serikali wanaowekwa kwenye bodi ya hizo hoteli wanashirikiana na sekta binafsi kula mapato yatokanayo na uwekezaji wa umma.
Badala ya kuzirejesha hotelI kuendeshwa na yenyewe inabidi SERIKALI kujitafakari kwanza kwani sekta binafsi ndio wako vizuri kuendesha hoteli.
 
Hili linawezekana pia, hapo kinachotakiwa ni serikali kuziuza moja kwa muja tu na kuwa inakusanya kodi. Hakuna umuhimu wa serikali kushiriki katika biashara ya Hotel na kuwa inashindana na raia wake.
Sio kwamba hoteli hizo za serikali zinazoendeshwa kwa ubia na sekta binafsi zinapata hasara. Ukweli ukifanyika ukaguzi na taasisi yenye uadilifu utakuta wabia wa serikali sekta binafsi ndio wanapata faida huku wakiweza kuionyesha serikali kuna hasara. kwa lugha rahisi ni kwamba kuna ufisadi mkubwa unafanyika ili sekta binafsi waendeshe hoteli kama yao na huku wawekezaji ambao ni umma kupitia serikali yao wakiambulia nunge. vigogo wahusika serikalini kupitia wakuregenzi kutoka serikali wanaowekwa kwenye bodi ya hizo hoteli wanashirikiana na sekta binafsi kula mapato yatokanayo na uwekezaji wa umma.
Badala ya kuzirejesha hotelI kuendeshwa na yenyewe inabidi SERIKALI kujitafakari kwanza kwani sekta binafsi ndio wako vizuri kuendesha hoteli.
 
Kama hadi sekta binafsi imeshindwa kuziendesha zifanywe hostel tu, chuo cha ufundi au shule ya boarding. Hakuna biashara ya Hotel hapo, ni Serikali itaenda kutapanya tu pesa za walipakodi. Serikali haitakaa iwe na ufanisi kuliko sekta binafsi katika biashara ya Hotel.
Uko sahihi sana mkuu.

Hakuna nchi yoyote iliyoendelea au inayotaka kuendelea ambayo Serikali yake inafanya biashara. Kazi ya Serikali ni kuandaa mazingira wezeshi kwa sekta binafsi kufanya biashara na si kinyume chake.
 
Mbona pale Dodoma jiji wamewakodishia Best Western Hotels?
 
Back
Top Bottom