Ulongupanjala
JF-Expert Member
- Apr 9, 2013
- 8,273
- 13,567
+ Kunyanduana bure kwa vigogo na chawa wao.Wengine watakuwa wanalala na kula bure huko
Tumeanza kurudi huko tulikoshindwa! Hawa vijana huko Serikalini hawasomi historia!! Hawajajua kinachotofautisha utendaji katika sekta ya umma na utendaji katika sekta binafsi? Wakati mwingine kukaa kimya kuna faida ya kuficha kuficha kiwango cha ujinga wako. Jaribu kurudisha uzalishaji wa bia kwenye Shirika la umma uone tofauti itakayotokea. Air Tanzania iko peke yake sasa lakini inapokea hela ya business class bila kutoa huduma uliyolipia pale kiwanjani!Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amesema Serikali imejipanga kuboresha huduma kwa watalii katika nyanja mbalimbali ili kuvutia watalii wengi zaidi ikiwa ni mkakati wa kuwafanya watalii hao kuongeza siku za kukaa nchini na hatimaye kukuza pato la Taifa.
Amesema moja ya mkakati wa Serikali ni kuboresha huduma za malazi kwa watalii kwa kuzirejesha hoteli za wizara ambazo zinaendeshwa na sekta binafsi ambazo kwa ujumla wake hazifanyi vizuri.
Masanja amesema Serikali inaendelea mikakati ya kuhakikisha hoteli hizo mara baada kurejeshwa zinakuwa kinara kwa kutoa huduma bora kwa watalii.
========
Hizi hoteli ni zipi? Pili sekta binafsi ichemke Serikali ndio wataweza! Au watatumia kodi zetu kuziendesha?
Kiufupi karibu kila mkoa kulikuwa ba hotel ya serikaliArusha hotel
Dodoma hotel
Mwanza hotel
Zipo zingine za upande wa pili...
NB
Taarifa hii ina weza kuwa sio sahihi, ni ya kufikirisha