Serikali kutaja chanzo cha ajali ya ndege Bukoba Novemba 11, 2023

Serikali kutaja chanzo cha ajali ya ndege Bukoba Novemba 11, 2023

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Serikali imesema bado inaendelea kuchunguza taarifa za awali za ajali ya ndege ya Precison iliyotokea mkoani Kagera Novemba 6 mwaka 2022 huku ikitangaza kwamba itatangaza chanzo cha ajali hiyo Novemba 11 mwaka huu baada ya kukamilisha na kuchakata taarifa zilizokusanywa.

Akizungumza na wandishi wa habari Mkurugenzi Msaidizi wa Ajali za Ndege kutoka Wizara ya. Ujenzi na Uchukuzi, Redemptus Bugomola, alisema taarifa zinazotolewa na baadhi ya vyombo vya habari zinazotaja chanzo cha ajali sio sahihi.

Alisema taarifa zilizotolewa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makartie Mbarawa ni za awali hivyo wanapaswa kusoma kwa makini kabla ya kusambaza na kwamba "Chanzo cha ajali bado hakijabainika"

kwa sasa tunaendelea kuchakata taarifa mbalimbali ambazo tumezikusanya kutoka kwa mashuhuda na vifaa vilivyosalia katika ajali hiyo, baada ya kufanya uchambuzi tutabaini chanzo cha ajali.

Aliongeza kuwa: "Taarifa hiyo itachukua muda mrefu na baada ya kukamilisha uchambuzi ndipo tutatoa ripoti ya mwisho ambayo inatarajia kutoka Novemba 11 mwaka huu.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete, alisema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imeweka msukumo mkubwa katika kuhakikisha kunakuwa na vifaa vya kisasa vya utabiri wa hali ya hewa.

Alisema Tanzania ni chi ya kwaza Afrika kwa kuwekeza vifaa vya kisasa zaidi kwa ajili ya utabiri wa hali ya hewa. "Serikali tayari imenunua rada mbili za kisasa ambazo zinatarajiwa kuanza kufungwa hivi karibuni, lengo ni kuhakikisha taarifa zinazotolewa na mamlaka zinakuwa zakuaminika па kutumiwa na makundi mbalimbali katika shughuli za maendeleo. Aliongeza kuwa:

"Taarifa zinazotolewa na TMA ni muhimu hasa kwa wakulima, wafugaji na wavuvi hasa zikitumiwa vizuri zitaleta tija katika uzalishaji.
 
Kwamba baada ya marehemu kufikisha mwaka mmoja ndio inakua rahisi kwao kupata taarifa kuhusiana na chanzo.
 
Kwamba baada ya marehemu kufikisha mwaka mmoja ndio inakua rahisi kwao kupata taarifa kuhusiana na chanzo
Najaribu kuunganisha ishu ya muda wa marehemu na kupatikana kwa chanzo, unamaanisha nini?
 
Back
Top Bottom