Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akiwasilisha Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2026/27 leo Juni 11, 2026, Bungeni, Dodoma, amesema kuwa erikali imependekeza kufanya marekebisho makubwa kwenye kodi na ushuru wa mafuta ya kula, ikiwa ni pamoja na kuanza kutoza ushuru wa forodha wa
10% kwenye mafuta ghafi ya kula ya aina zote nchini, ikiwemo ya mchikichi, pamoja na yale yaliyochakatwa kwa kiwango kidogo (
semi-refined palm oil).
Waziri aliongeza kuwa hatua hiyo inaendana na mwelekeo wa sera za kikanda ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), ambapo nchi jirani za Kenya na Uganda tayari zimeanza kutoza ushuru wa
10% kwenye mafuta ghafi ya mchikichi kutoka nje ya jumuiya hiyo.
Mikakati
Katika kuendeleza matumizi ya mafuta ya kula yanayozalishwa kwa kutumia mbegu za ndani ya nchi, Waziri wa Fedha amezitaja hatua zingine zilizochukuliwa kuwa ni pamoja na:
- Msamaha wa VAT: Serikali itaendelea kutoa msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye mafuta ya kula yanayozalishwa nchini kwa kutumia mbegu zinazoshwa ndani ya nchi.
- Ushuru wa Mafuta Safi: Serikali itaendelea kutoza ushuru wa 35% au Dola za Kimarekani 300 kwa kila tani moja ya mafuta safi ya kula kutoka nje (refined oil), ikitegemea kiwango kipi kitakuwa kikubwa zaidi.
- Kanuni Mpya za Uagizaji: Serikali imeandaa kanuni mpya za uagizaji wa mafuta ya kula ili kudhibiti uingizaji wa bidhaa hiyo nchini na kukuza tasnia ya ndani.
- Utoaji wa Vibali Maalum: Kupitia Wizara ya Kilimo, serikali itatathmini na kutoa vibali maalum kwa waagizaji wa mafuta baada ya kujiridhisha juu ya uwekezaji wao katika uzalishaji wa mbegu za alizeti, pamba, na michikichi chini ya kanuni za COPRA za mwaka 2026.