Serikali Kutumia Bilioni 33 Kusambaza Maji Jijini Dar es Salaam, Kibamba Yapata Bilioni 13.9 Mwaka Mpya wa Fedha 2024-2025

Serikali Kutumia Bilioni 33 Kusambaza Maji Jijini Dar es Salaam, Kibamba Yapata Bilioni 13.9 Mwaka Mpya wa Fedha 2024-2025

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
"Ipi kauli ya Serikali ya kutokamilika kwa miradi ya Maji katika Jimbo la Kibamba?" - Mhe. Issa Jumanne Mtemvu, Mbunge wa Jimbo la Kibamba

"Serikali imekamilisha ujenzi wa miradi mitatu ya usambazaji wa maji kutokea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hadi Bagamoyo (2B2F), Mshikamano na Kitopeni ambapo miradi hiyo inanufaisha wakazi wapatao 210,876 kwa Jimbo la Kibamba " - Mhe. Eng. Methew Kundo, Naibu Waziri wa Maji

"Serikali inaendelea na utekelezaji wa mradi wa usambazaji maji Kusini mwa Dar es Salaam Bangulo ambapo utekelezaji wake umefikia asilimia 25 na unatarajia kukamilika mwezi Desemba 2024 ambao utanufaisha wakazi 271,863 wa Jimbo la Kibamba. Serikali itaendelea kukamilisha utekelezaji wa miradi katika maeneo mbalimbali ikiwemo Jimbo la Kibamba" - Mhe. Eng. Methew Kundo, Naibu Waziri wa Maji

"Ukamilishaji wa miradi ni matanki ya kuhifadhia maji. Ili mradi ukamilike ni lazima usambazaji wa mabomba kwenda kwa wananchi ukamilike. Maeneo ya CCM ya zamani, Mpiji Magoe, Torino, Kwa Mkungi, Kwa Mzee Kadope na Kwa Yusuf Michungwani. Lini Serikali itatekeleza ahadi yake ya muda mrefu ya kupeleka mabomba?" - Mhe. Issa Jumanne Mtemvu, Mbunge wa Jimbo la Kibamba

"Uchumi Centre na Darajani ni muda mrefu hawajawahi kuona maji safi na salama. Serikali imefanya utafiti na ina nia ya kutekeleza mradi wa Shilingi bilioni 13.9. Je, ni lini Serikali itaanza kutekeleza mradi huo?" - Mhe. Issa Jumanne Mtemvu, Mbunge wa Jimbo la Kibamba

"Kupitia mradi wa kuboresha huduma za maji katika Mkoa wa Dar es Salaam, Serikali imetenga shilingi Bilioni 33 ambapo ndani yake kuna shilingi bilioni 13.9 kwaajili ya kutekeleza miradi Kibamba. Bajeti hii ya 2024-2025 itakapopitisha mradi utaanza kutekelezwa mara moja" - Mhe. Eng. Methew Kundo, Naibu Waziri wa Maji

maxresdefaultvbgtyh.jpg
kampuni-picwqasert.jpg
 
Back
Top Bottom