johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
- Thread starter
- #21
Manka huko Marangu chukueni tahadhari!ukichimama COVID ukitembea nzige.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Manka huko Marangu chukueni tahadhari!ukichimama COVID ukitembea nzige.
Na bado watu wakawa wanamcheka Mheshimiwa Wakili Hashim Rungwe aliposema ataleta midege ya kufanya kilimo cha umwagiliaji.Waziri wa kilimo Prof Mkenda amesema kuanzia kesho wataanza kumwaga viatilifu vya kuuwa nzige katika wilaya ya Longidi na Simanjiro kwa kutumia ndege...
Miaka ya huko nyuma kulikuwa na Shirika la kuzuia Nzige likiitwa Desert Locust Control Organization for Eastern Africa (DLCO-EA) Makao Makuu yakiwa Addis Ababa na ofisi za Tanzania zikiwa Arusha na bado zipo lakini hazitumiki. Shirika hili lilifanya kazi nzuri sana kuzuia Nzige kuanzia kule Jangwani wanakozaliana kabla hawajafika nchi wanachama kuleta madhara.Mwaka jana kipindi kama hiki tulitamba sana maombi yamedhibiti nzige na covid, naanza kuamini sasa kuna kitu tumemkosea mungu iweje mabalaa tuliyoyashinda yarudi kwa pamoja. Au kama tulienda kwa mganga alietusaidia hatukumlipa basi turudi kulipa deni yaishe jamani
Hatukutoa shukraniMwaka jana kipindi kama hiki tulitamba sana maombi yamedhibiti nzige na covid, naanza kuamini sasa kuna kitu tumemkosea mungu iweje mabalaa tuliyoyashinda yarudi kwa pamoja. Au kama tulienda kwa mganga alietusaidia hatukumlipa basi turudi kulipa deni yaishe jamani
Yale maombi tuliyo ambiwa na Jiwe yamefeli kuondoa nzige Kama alivyofeli kwenye corona👿Waziri wa kilimo Prof Mkenda amesema kuanzia kesho wataanza kumwaga viatilifu vya kuuwa nzige katika wilaya ya Longidi na Simanjiro kwa kutumia ndege...
Nimeipenda sana hii historia, ukweli kizazi cha zamani kilikuwa kinaona mbali sana kwenye maswala ya kimkakati na walikuwa na scientific approach ya kukikabili chanzo cha tatizo. Ni kweli kuna baadhi ya magonjwa na majanga huwezi kuyakabili peke yako. Wairudishe hiyo taasisi haraka sana.Miaka ya huko nyuma kulikuwa na Shirika la kuzuia Nzige likiitwa Desert Locust Control Organization for Eastern Africa (DLCO-EA) Makao Makuu yakiwa Addis Ababa na ofisi za Tanzania zikiwa Arusha na bado zipo lakini hazitumiki. Shirika hili lilifanya kazi nzuri sana kuzuia Nzige kuanzia kule Jangwani wanakozaliana kabla hawajafika nchi wanachama kuleta madhara.
Shirika lilianzishwa na Wakoloni wa Kingereza na kama lingekuwa bado hai lingekuwa na umri wa zaidi ya miaka 100 lakini bahati mbaya sana lilikufa likiongozwa na Tanzania Awamu ya Tatu kwa mara ya kwanza toka liundwe. Kwa nia nzuri tu Tanzania ikajenga hoja kwamba toka Shirika lianze haikuwa imewahi kuongoza ingawa ilikuwa mwanachama mwaminifu na kulipa michango yake kwa wakati.
Nchi zote wanachama ziliona kuna ukweli kwenye hoja hiyo kwa hiyo Tanzania ilipewa nafasi ya kupendekeza Mkurugenzi Mkuu atakayeongoza Shirika miaka 5 ijayo. Serikali ilitangaza nafasi hiyo na Watanzania wengi waliomba na alipatikana Prof mmoja toka SUA (ingefaa nimtaje maana alitia aibu) akahamia Addis kuanza kazi.
Miaka hata miwili ya uongozi wa Tanzania haikufika, Shirika likawa limekufa mpaka leo na Nzige wamepiga hodi zaidi miaka 70 bila Nzige hata kuonekana nchini.
Mkurugenzi alipoingia tu madarakani safari za Ulaya (alikuwa anajua Kingereza) zikawa haziishi mpaka nchi wanachama wakaanza kulalamika kuwa anatumia fedha vibaya kwa safari binafsi za Uswisi mwisho wakaacha kutoa michango, Shirika likafa mpaka leo. Mpe madaraka Musukuma atafuata wanawake weupe popote walipo!
Kufuata njia ya Rais wetu, naomba kuuliza dawa hii imepatikana kutoka wapi? ni nani watengenezaji wakuu wa dawa hii? Mnajuaje kama miongoni mwa kemikali zilizomo ndani ya dawa hiyo haziuwi wanaadamu kidogo kidogo? Mnataka kutwambia kuwa dawa hii imetengenezwa Tanzania, na watanzania kwa kufuata formula za watanzania bila ya msaada kutoka kwa hao mnaowaita mabeberu?Waziri wa kilimo Prof Mkenda amesema kuanzia kesho wataanza kumwaga viatilifu vya kuuwa nzige katika wilaya ya Longidi na Simanjiro kwa kutumia ndege.
Shule zitafungwa kwa muda wa siku nne na wananchi wanaonywa kutookota nzige na kuwala.
Chanzo: ITV habari
Maendeleo hayana vyama!
------
Waziri wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda, amesema kuanzia leo ndege itapuliza sumu kuua nzige katika wilaya za Longido na Simanjiro.
Aliyasema hayo jana alipotembelea eneo lililovamiwa na wadudu hao wilayani Longido.
Profesa Mkenda alisema wananchi wasiwe na hofu kwa kuwa nzige wote watadhibitiwa kupitia wataalamu wa Wizara ya Kilimo waliopo kwenye maeneo yote yenye dalili za uwepo wa wadudu hao.
Waziri Mkenda alisema wataalamu wa Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya Kudhibiti Visumbufu (TPRI) wapo wilayani Longido na Simanjiro wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu Dk Efrem Njau.
Alitoa mwito kwa wananchi wasiokote au kula nzige watakaokuwa wamekufa kwenye maeneo yote ambako ndege itapita kuwaua.
"Wananchi wakiona nzige wameanguka chini wamekufa wasiwachukue au kula kwa kuwa wengi watakuwa wamekufa kwa sumu" alisema Profesa Mkenda.
Alisema, nzige wa jangwani wana athari kubwa katika uzalishaji wa mazao ya chakula na malisho ya mifugo na kwamba, kwa siku kundi moja la nzige lina uwezo wa kuruka bila kutua kwa umbali wa kilometa 150.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido, Jumaa Mhina, ametoa agizo shule zote za msingi na sekondari kwenye maeneo ambapo ndege itapuliza viuatilifu kusitisha masomo kwa siku 4 kuanzia leo ili kudhidhibi watoto wasije wakapata madhara endapo watashika au kuchezea nzige watakaokufa.
Awali Wizara ya Kilimo ilitangaza kuwa serikali imeandaa vikosi viwili kupambana na nzige wa jangwani walioripotiwa kuingia katika wilaya za Mwanga, Simanjiro na Longido katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara wakitoka Kenya.
Naibu Waziri wa wizara hiyo,Hussein Bashe, aliyasema hayo jana alipozungumza na HabariLEO kuhusu mikakati ya serikali kuhakikisha wadudu hao hawaleti hawaharibu mazao ya wakulima.
Kwa mujibu wa Bashe, kikosi cha kwanza ni cha wataalamu wa ardhini wanaotumia dawa za kubeba mgongoni na pia kutumia magari yakiwemo matrekta kunyunyizia wadudu hao kuwaangamiza.
Alisema kikosi hicho kinafanya kazi vizuri na kwamba, kilianza kujiandaa tangu mwaka jana. Bashe alisema, kikosi cha pili kinatumia ndege kwa ajili ya kunyunyiza dawa katika maeneo yenye nzige.
Alisema serikali imejipanga kwa kuandaa dawa za kutosha, na kwamba, wakati wataalamu wa kilimo kutoka wizarani wakiendelea kupambana na wadudu hao ardhini, mipango ya kutumia ndege kwa ajili ya kuwanyunyizia dawa inaendelea.
Kwa mujibu wa Bashe, Tanzania ni mwanachama wa jumuiya mbili za kikanda za kupambana na nzige.
Jumuiya ya kwanza ni ya Kusini mwa Afrika ya kupambana na nzige wekundu inayoshirikisha nchi za Zambia, Tanzania, Zimbabwe, Afrika Kusini na Namibia.
Pia Tanzania ni mwanachama wa jumuiya ya mashariki inayopambana na nzige wa jangwani inayoshirikisha nchi za Uganda, Kenya, Tanzania, na Ethiopia.
Bashe alisema lengo la Tanzania ili kuweza kupambana na nzige hao ni kupata ndege tatu hadi nne kwa ajili ya kuimarisha kikosi cha anga.
“Mpaka sasa tuna ndege moja tu ambayo imeshafika nchini kutoka katika jumuiya ya mashariki inayopambana na nzige wa jangwani,”alisema.
Bashe alisema wamezungumza na Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) na wapo katika hatua za mwisho za kuipatia Tanzania ndege moja hivyo kutakuwa na ndege mbili.
“Pia tupo katika mazungumzo na jumuiya ya Kusini inayopambana na nzige wekundu ambapo wiki iliyopita tulizungumza nao na tunategemea wakati wowote tutapata ndege nyingine,” aliongeza Bashe.
Aliwaomba Watanzania kutokuwa na hofu kwa sababu serikali imejipanga vya kutosha kuwadhibiti wadudu hao.
Bashe alisema mara ya kwanza liliingia kundi dogo la nzige Januari 10 mwaka huu wilayani Mwanga na kwamba, wataalamu wa kikosi cha ardhini waliwaangamiza.
Alisema nzige walirudi tena Januari 16 mwaka huu katika wilaya na kutawanyika hadi Simanjiro mkoani Manyara.
Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Thomas Apson, alilieleza HabariLEO kuwa nzige walipita katika kijiji cha Karamandei kwenye kata ya Toloha wilayani Mwanga.
Apson alisema, hakuna uharibifu wowote uliofanywa na wadudu hao kwa kuwa walipita katika mapori wanakoishi wafugaji.
"Serikali imefanikiwa kwa asilimia kubwa kuwadhibiti wadudu hao. Kwa sasa hakuna madhara yaliyotokea kwa kuwa wadudu walivamia eneo la pori la kijiji hicho ambacho asilimia kubwa wanaishi wafugaji,” alisema.
Apson alisema tangu kuwepo kwa madai ya kijiji kuvamiwa na nzige, serikali iliandaa ndege itakayotumika kumwaga dawa kuwadhibiti kama wataalamu watathibitisha kuwa ni nzige.
Mkuu wa Wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe, alilieleza HabariLEO kuwa nzige walioingia wilayani humo walitoka Kenya kupitia Namanga na waliekea katika maeneo ya magharibi ya Kilimanjaro.
Chanzo: Habari Leo
Nahisi Makonda kachomoa betri sio bure.Mwaka jana kipindi kama hiki tulitamba sana maombi yamedhibiti nzige na covid, naanza kuamini sasa kuna kitu tumemkosea mungu iweje mabalaa tuliyoyashinda yarudi kwa pamoja. Au kama tulienda kwa mganga alietusaidia hatukumlipa basi turudi kulipa deni yaishe jamani.
Si mlituambia kupitia kwa gwajima kuwa mmewafukuza nzige kwa maombi, imekuwaje tena?Ni jambo jema.
Karibuni BAVICHA mje kupinga!
Mbona mwenyekiti wenu huwa hashirikishi ubongo kabla ya kulaumu wazungu? Kila siku mnatuaminisha kuwa wazungu wanataka kutumaliza kwa kutumia chanjo ya korona. Ajabu leo mnatumia teknolojia yao kuangamiza nzige.Wakati mwingine kabla hujaandika shirikisha ubongo!
Unapojibu jaribu kushirikisha makalio.Wakati mwingine kabla hujaandika shirikisha ubongo!