SoC01 Serikali Kuu Punguzeni Kuwafanyia Kazi Wananchi

SoC01 Serikali Kuu Punguzeni Kuwafanyia Kazi Wananchi

Stories of Change - 2021 Competition

Mulokozi GG

Member
Joined
Jul 14, 2021
Posts
34
Reaction score
44
Kilikuwa kipindi kigumu nilipo jua uhalisia kuwa ukikubali kuishi ni lazima ufanye kazi, na maendeleo ya mtu ni kinyume sawia na ubora wa juhudi zake katika kazi anazozifanya. Sababu hakuna aliye umba chochote duniani vyote vilivyopo vilikuwepo na vipo, hivyo ni lazima tujifunze jinsi ya kuendana navyo. Sikuwa na mbadala zaidi ya kuuchukua ukweli mchungu zaidi ya kuendelea kuishi kwa kujifariji au kufarijiwa.

Iwe kwa kujua au kwa kutokujua ni jukumu la mtu mmoja mmoja ndani ya Taifa kuamua kuishi kwa kufarijiwa au kutafuta maarifa na ujasiri wa kuishi uhalisia/kufanya shughuli zitakazo mfanya akidhi mahitaji yake ya kila siku. Katika kufanya kazi zitakazo mfanya kukidhi mahitaji yake, shughuli zote anazozifanya mtu ndani ya jamii ni mchango wa mmoja kwa moja kwa Nchi yake chini ya muongozo wa serikali kama chombo chenye dhamana ya kusimamia na kuongoza watu na rasilimali ndani ya Nchi husika.

Kwa kuanganazia viunzi vya serikali ni dhahili kuwa serikali ya Nchi ni mjumuiko wa kanuni au taratibu pamoja na wale wanao simamia taratibu hizo. Hivyo serikali kama kiongozi wa jamii ni msingi unaoweza kuifanya jamii itoke katika hali moja hadi hali nyingine kupitia njia inazo zitumia kuanzisha na kutekeleza kanuni na taratibu zinazo wekwa kama muongozo ndani ya jamii au Taifa.

Kile ilicho nacho na inacho kipata serikali inakitegemea kwa njia moja au nyingine kutoka kwa wale walio ndani ya jamii, hivyo matumizi ya serikali ni zao la juhudi za watu ndani ya Taifa husika. Bila kujali kiwango cha akiba ilicho nacho serikali, mipango mingi ya matumizi yajayo hufanywa kulingana au kutokana na matarajio kuwa mapato yake yajayo yatakuwa katika kiwango fulani (kilichopo sasahivi, kipande au kishuke kulingana na hali ya uchumi ilivyo na itakavyo kuwa). Tanzania kama Taifa linalo fuata mfumo wa Kibepari(katika matendo) serikali yake imekuwa ikipanga, ikihaidi na kutoa baadhi ya huduma bure na katika misingi ambayo huduma hizo uhalisia wake zimegeuka kuwa mzigo kwake.

Ifahamike wazi kuwa gharama na huduma zote zinazotolewa bure na serikali, huduma hizo siyo bure bali zinalipwa na watu wote ndani ya Taifa katika muundo wa kodi. Mfano kwa kutumia sera ya elimu bure; kipindi cha nyuma kila mzazi alikuwa na jukumu la kugharamikia elimu ya mtoto wake yeye mwenyewe kutokana na kipato chake.

Hivyo lilikuwa ni jukumu la mzazi kutumia nguvu na juhudi zake zote na kila aina ya rasilimali iliyokuwepo kuhakikisha mtoto wake anapata elimu. Mwaka 2016 elimu ya msingi na sekondari ilianza kugharamikiwa na serikali. Hii inamaanisha kuwa jukumu na gharama zilizo kuwa za mzazi mmoja mmoja kwa mtoto wake ili apate elimu, ziligawanywa sawa kwa WaTanzania wote katika sura ya kodi na si vinginevyo.

Kwa kujua au bila kujua katika kiasi cha kodi alichokuwa analipa kila Mtanzania kuanzia mwaka 2016 aliongezewa kiasi kadhaa cha kodi kwa ajiri ya gharama za elimu ya msingi pamoja na sekondari. Hii ilifanya majukumu na kazi za wazazi kama mwanachi kwa watoto wao kuanza kutekelezwa na serikali badala ya Wananchi kufanya kazi zao huku wakiongozwa na serikali.

Hata hivyo kutolewa kwa baadhi ya huduma chini ya kivuli kuwa ni bure siyo ishara kuwa serikali ina pesa au akiba nyingi, kwani kupanda kwa baadhi ya kodi au huduma (kama gharama za umeme) na kuanzishwa kwa kodi mpya (tozo) ni miongoni mwa viashilia hai vya njia na juhudi za serikali kukusanya pesa ili kuendelea kumudu huduma hizo na majukumu yake mengine.
Hivyo kuanzia mwaka 2016, kodi iliyoongezeka ili kukidhi gharama za elimu ya msingi na sekondari ni sehemu ya kile kinachoitwa mfumuko wa bei na kupanda kwa gharama za maisha.

Maswali ya kujiuliza ni, je huduma na mazingira mengine kama sehemu ya majukumu yanayo tekelezwa na serikali yana hali gani, kiasi cha kutoa baadhi ya huduma bure katika mfumo huu wa Kibepari? inaoufuata katika matendo.

Je gharama hizo kwanini zisitumike kutengeneza mazingira yatakayo wahamasisha watu kuongeza kipato chao zaidi ya kutegemea kuhudumiwa bure?

Hizi gharama zinazo tumika katika kivuli cha kutoa huduma bure lakini zikilipwa na Watanzania wote kama kodi, ushuru na tozo nyinginezo zinaweza kutumika katika mazingira yafuatayo; kupunguza kiwango cha kodi kinacho lipwa na wafanya biashara pamoja na kupunguza gharama za umeme ili kuwahamasisha watu kuongeza ubunifu na kunufaika na juhudi zao. Zaidi ya kuwaaminisha kuwa wanapewa huduma bure wang'ali wanazilipia kama kodi.

Gharama hizi zinaweza kutumika kufanya utafiti wa mfumo bora zaidi wa elimu utakao mfanya mtu mmoja mmoja kuwa na ujuzi wa kujitegemea na kuanza kutekeleza mfumo huo wa elimu badala ya huu unao wafanya wahitimu kuwa wahanga wa ajira.

Gharama hizi zinaweza kutumika kuboresha miundo mbinu kama barabara, ili hata mkulima aliye kijijini mazao yake yapande thamani sababu ni rahisi kuyasafirisha na kumfanya ajihudumie mwenyewe. Kwani asilimia kubwa ya barabara Nchini bado zipo katika kiwango cha chini hasa zile za vijijini baadhi zikiwa hazipitiki kabisa kipindi cha mvua.

Mfano kwa mjibu wa ukurasa wa the global economy taarifa za mwaka 2019 Tanzania ilikuwa katika nafasi ya 66 kwa ubora wa barabara duniani Kati ya Nchi 141, ikiwa na alama 4.1 ikilinganishwa na alama 6.5 za Taifa lilokuwa linaongoza duniani. Hiki ni kiashiria tosha kuwa bado tunao uhitaji mkubwa wa miundo mbinu ya msingi kama barabara.

Niwe muwazi kuwa sipingani na juhudi zozote za serikali katika kutoa huduma za bure kwenye jamii kwani ni kuwarudishia watu kile kilicho chao kama msaada wa moja kwa moja kwa wengi ndani ya Taifa. Msingi wa hoja yangu ni kuwa huduma hizi zitolewe kulingana na uwezo halisi wa serikali na kwa kuzingatia matokeo au madhala ya mda mrefu yakatayo tokana na huduma husika.

Sababu zanazo ifanya serikali kuwaambia Wanachi kuwa baadhi ya huduma zinatolewa bure ing'ali zinalipwa kama kodi, ushuru na kwenye mfumuko wa bei ni ; Moja sababu za kisiasa machoni mwa watu(political popularity), mbili dhamila ya kutafuta njia ya kuwasaidia watu wenye uwezo mdogo ndani ya jamii na tatu kutotilia maanani madhala ya mda mrefu yatakayo tokana na uamuzi husika.

Njia zinazo paswa kutumika kuepuka changamoto za hivi ni ; Moja mipaka kwenye kauli za kisiasa na sera za Nchi . Hapa matamko ya kisiasa yenye madhala katika muenendo wa kiuchumi katika Taifa yawe yanajadiliwa na kuboreshwa na kamati maalumu kabla hayajaanza kutekelezwa kama utaratibu ndani ya Taifa.

Mbili, uudwe au utengenezwe mpango au dira ya Taifa ya miaka 50 hadi 100. Katika kutengeneza dira hii vyama vyote vya kisiasa pamoja na taasisi zote zenye ushawishi ndani ya Nchi zihusishwe moja kwa moja, ili kufikia mtazamo na makubalioano ya pamoja kama Taifa. Ili hata chama cha kisiasa kikitengeneza ilani yake iwe inaelezea kitakavyo itumia ilani hiyo kufikia dira ya Taifa, hivyo dira ya Taifa ndiyo iwe kipimo cha ubora wa ilani za vyama vya kisiasa.

Tatu ifahamike na iwekwe wazi kuwa njia pekee ya kumsaidia mtu au watu ni kuwapa maarifa sahihi na siyo kuwaondolea majukumu . Hapa utengenezwe mfumo wa elimu utakao mpa mtu mmoja mmoja ujuzi wa kujitegemea kwenye maisha, kwani kumuondolea mtu baadhi ya majukumu inamfanya abweteke hali inayomfanya awe na hali ngumu zaidi ya aliyo kuwa nayo au aliyo itegemea.

Nne, utengenezwe utaratibu wa kutambua watu ambao hawawezi kumudu gharama za maisha yao wenyewe za kila siku kama yatima na walemavu.
Mfano kupitia njia kama zilizo kuwa zikitumika TASAF kubaini wenye uhitaji, lakini mfumo huu ujifunze kupitia changamoto na mapungufu ya TASAF ili uwe bora na makini zaidi kuhakikisha unawapata wale tu wenye uhitaji haswa. Watu watakaokuwa katika kundi hili ndio wapewe huduma maalumu kama elimu, matibabu pamoja na usafiri.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom