Serikali kuunda timu maalum kusimamia urejeshaji huduma za usafiri wa vivuko Mafia - Pwani

Serikali kuunda timu maalum kusimamia urejeshaji huduma za usafiri wa vivuko Mafia - Pwani

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
WhatsApp Image 2024-10-26 at 16.34.27_2f9e4199.jpg

WhatsApp Image 2024-10-26 at 16.34.28_fdfa3213.jpg

Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Wizara ya Uchukuzi na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa itaunda Timu Maalum itakayoshughulikia na kusimamia urejeshaji wa huduma ya usafiri wa Vivuko vya MV Kilindoni na Meli ya TNS Songosongo vinavyofanya safari kati ya kituo cha Mafia - Nyamisati (Kibiti) vilivyosimamisha huduma ya usafiri tangu tarehe 10 Oktoba, 2024.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa Wilayani Mafia Mkoani Pwani wakati akikagua matengenezo ya Kivuko cha Meli ya TNS Songosongo kinachosimamiwa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kupitia Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa leo Oktoba 26, 2024

Bashungwa ameeleza kuwa Serikali inatambua umuhimu wa huduma ya usafiri wa vivuko katika Wilaya ya Mafia ambayo imesimama kutokana na vivuko vya MV Kilindoni na Meli ya TNS Songosongo kupata hitilafu ambapo sasa kazi ya matengenezo inaendelea kwa vivuko vyote wiwili.

“Serikali ipo kazini, na kupitia timu hii kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani itafanya jitihada za haraka za kurudisha huduma za vivuko viwili vya MV Kilidoni na Meli ya TNS Songosongo ili kuwaondolea adha wana Mafia ya kukosa usafiri wa Vivuko”, amesisitiza Bashungwa.
WhatsApp Image 2024-10-26 at 16.34.26_356c8cd5.jpg

WhatsApp Image 2024-10-26 at 16.34.26_8f2f2c7a.jpg
Bashungwa ameeleza kuwa Mkakati wa Serikali ni kuongeza kivuko kingine ili kusaidia wakati wa dharura kwa kutoa huduma kwa wananchi pindi kivuko kingine kinapopata hitilafu.

Aidha, Bashungwa amewahakikishia Wananchi wa mafia kuwa Timu hiyo ya Wataalam itafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha wanarejesha huduma za vivuko haraka iwezekanavyo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amesema Ofisi yake inaendelea kuongea na Wawekezaji wa Sekta binafsi watakaoweza kufanya uwekezaji wa huduma ya Usafiri na Hoteli ili kushirikiana na Serikali katika utoaji wa huduma hizo ambazo zitaendelea kufungua uchumi wa Wilaya ya Mafia.
WhatsApp Image 2024-10-26 at 16.34.25_3c904fd9.jpg


===================​

BASHUNGWA AMPIGIA SIMU KATIBU MKUU AMTAKA KUPIGA KAMBI MAFIA HADI HUDUMA YA USAFIRI WA KIVUKO ITAKAPOREJEA.

“Msitoke Mafia mpaka Kivuko kianze kutoa huduma kwa Wananchi”

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amempgia simu na kumuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Eng. Aisha Amour na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Ufundi na Umeme (TEMESA), Lazaro Kilahala kufika mara moja katika Kisiwa cha Mafia kupiga kambi kusimamia matengenezo ya Kivuko cha MV Kilindoni na kuhakikisha hawatoki mpaka huduma ya usafiri wa kivuko kati ya Nyamisati - Mafia itakaporejea na kutoa huduma kwa wananchi.
WhatsApp Image 2024-10-27 at 11.04.15_a2955c0a.jpg

WhatsApp Image 2024-10-27 at 11.04.16_d35ff4c9.jpg
Bashungwa ametoa maelekezo hayo wakati akitoa ufafanuzi kwa Wananchi kuhusu kusimama na kukosekana kwa huduma ya usafiri wa vivuko katika Wilaya ya Mafia Mkoani Pwani ambapo Wananchi wamelalamikia kukosa huduma ya vivuko na kupelekea kutumia vyombo vya usafiri visivyo salama na uhakika pamoja na kushindwa kusafirisha bidhaa na huduma nyingine.

“Katibu Mkuu kufika kesho kutwa wewe au Naibu Katibu Mkuu uje hapa Mafia uambatane na Mtendaji Mkuu wa TEMESA mpige kambi muone kilio na uchungu wa wananchi wa Mafia wanaoupata, Msitoke hapa mpaka kivuko kianze kutoa huduma kwa wananchi. Kivuko kikianza kufanya kazi ndio mnipigie simu niweze kuwaruhusu kutoka huku Mafia”, amesisitiza Bashungwa.

Waziri Bashungwa ameeleza kuwa Serikali inatambua usafiri unaotumika kufika katika kisiwa cha Mafia ni usafiri wa vivuko na ndege ambapo sasa Serikali inaendelea na jitihada za kurejesha huduma ya usafiri wa vivuko kwa kuwa sio wananchi wote wana uwezo wa kutumia usafiri wa ndege.

Aidha, Bashungwa ameeleza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa inaendelea na ukarabati wa Meli ya TNS Songosongo itayosaidia kutoa huduma ya usafiri kwa wananchi wa Mafia wakati Kivuko cha MV Kilindoni kikiwa kwenye matengenezo.
WhatsApp Image 2024-10-27 at 11.04.17_5ab6626c.jpg
Bashungwa ameeleza kuwa Serikali imetenga fedha zaidi ya Shilingi Bilioni 9 kwa ajili ya ujenzi wa kivuko kipya kitakachotoa huduma za usafiri kati ya Mafia na Nyamisati na hivyo kuongeza idadi ya vivuko kuwa vitatu.

Katika nyakati tofauti, Wananchi wa Kilindoni Wilayani Mafia wameiomba Serikali kusimamia na kutatua kero ya huduma ya usafiri wa vivuko wanayoipata katika Wilaya hiyo ambayo imesababisha kuongezeka kwa gharama za maisha na wananchi kushindwa kupata huduma nyingine za kijamii.


Pia soma ~ Kwanini tukarabati kivuko kwa Tsh. bil 7.5 wakati kipya ni bil 8.5?

UPDATES
- MV Kilindoni yarejesha huduma ya usafiri Mafia
 
Back
Top Bottom