Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,187
Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, akiwa mkoani Njombe, ameahidi kuwa, Serikali inatafajia kuzima mitambo yote ya TANESCO, inayotumia mafuta mazito baada ya kukamilika kwa Mradi wa Stiegler's Gorge ifikapo mwaka 2020.
Dk. Kalemani alieleza kuwa, umeme wa mafuta mazito ni wa gharama kubwa ndiyo maana Serikali inapambana kuhakikisha Mradi wa kuzalisha umeme wa Rufiji unakamilika haraka kama ilivyokusudiwa.
"Tulifanikiwa kuzima vituo vichache mwaka jana ikiwemo mitambo ya IPTL na kuacha mitambo ya Simbion na Agreco, lengo ni kupunguza matumizi ya uendeshaji wa TANESCO ambayo yalikuwa ni makubwa na tumefanikiwa kwa asilimia chache Shirika kuweza kujiendesha."
Mradi wa Stiegler's Gorge utazalisha MW 2,100 kwenye Gridi ya Taifa. Vilevile, utaongeza kilimo cha umeagiliaji kwa maeneo yaliyoko pembezoni mwa Mradi huo. Aidha, utaongeza utalii na kutoa ajira zaidi ya 1,500 wakati wa ujenzi na 500 wataajiriwa.