Serikali: Kwa sasa Tanzania ina wagonjwa 66 wa Corona nchi nzima ndani ya mikoa 10 na mikoa 16 haina wagonjwa

Serikali: Kwa sasa Tanzania ina wagonjwa 66 wa Corona nchi nzima ndani ya mikoa 10 na mikoa 16 haina wagonjwa

Idadi ya wagonjwa imeongezeka kutoka wanne tuliokuwa nao wiki iliyopita hadi 66, hivi ni asilimia ngapi? Swali la ufahamu, wamepimwa kwa vipimo gani?
 
Waziri Mkuu: Wagonjwa wa Corona Tanzania ni 66

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema hadi kufikia Leo mchana, Juni 15,2020, Tanzania ilikuwa na jumla ya wagonjwa 66 wa virusi vya corona waliolazwa kwenye vituo mbalimbali vya kutolea huduma nchini.

Akizungumza bungeni, Dodoma wakati akieleza mafanikio ya serikali ya awamu ya tano, Majaliwa amesema kuwa bado Corona ipo wananchi waendelee kuchukua tahadhari.

"Taarifa mpaka leo kutoka kwenye vituo vya kutolea huduma vya serikali na binafsi inaonyesha kuwa tuna wagonjwa 66 katika mikoa 10 na mikoa 16 haina mgonjwa hata mmoja," amesema.

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
si walisema wamebaki wawili na wamepona ! na tukaambiwa korona hamna? hata barakoa. Ni Kama titi tu! tukavae na wake zetu!
Leo iweje wagonjwa tuambiwe Ni 66 Wakati watu wamerelax hawanawi tena ndoo haziwekwi maji, sabuni hakuna tena! korona hakuna
 
hongera kwa kuwa mhenga sisi juniors tujuane
Vya wahenga vizuri mkuu.Tafuta hicho kitabu ukisome ujue wahenga tulivyofaidi. Nikiwa mtoto wa level ya darasa la nne, kilinipa uelewa wa mambo mengi sana hadi walimu walinishangaa kwa maswali niliyokuwa nawauliza.
 
Back
Top Bottom