Watu walikuwa wengi kwelikweli, ni maelfu ya watu wamekusanyika kwa ajili ya kushiriki mashindano ya Kilimanjaro Marathon. Miongoni mwao wapo ambao hawakuvaa barakoa kabisa, na wamo amabao walizivaa na kuzivua.
Mkusanyiko wa mahali hapo ulikuwa ni mkubwa kiasi kwamba kaa kuna wstu wana virusi vya korona basi huenda kukawepo na usambazaji wa virusi kwa kiwango cha kutisha.
Katika mazingira kama haya, serikali inaruhusuje mikusanyiko kama hii?
Je, kufanya hivyo siyo kuhatarisha usalama wa Nchi?
Maana hawa watu wanatoka kila kona ya nchi. Je, namna hii siyo kusambaza virusi kwa kasi ya kutisha?
Serikali hii ndo inasema kuwaambia wananchi wafuate maelekezo ya wataalamu, lakini wakati huohuo inabariki na kusaidia kuwezesha mambo yote ambayo wataalamu wanashauri yasifanywe!
Leo kwenye mashindano hayo ya Kilimanjaro Marathon alikuwepo mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mama Mgwitra katikati ya msitu wa watu ambao hawajavaa barakoa waa kuweka social distance maana ni vigumu katika mkusanyiko huo kuweka hiyo social distance!
Kwa kweli inasikitisha, kuona serikali inajaribu kujifanya kuwa hili tatizo ni la mtu binafsi na si la Taifa kwa ujumla wake, otherwise niambieni kwa nini serikali inaruhusu miusanyiko kama hii inayoweza kupelekea usambaaji wa kirusi kuwa wakutisha? - Serikali inataka kuachieve nini?
Wananchi wanakufa kwa "changamoto", Tunawazika, na tunaendelea kushuhudia hii hali kila kukicha, mbona basi mamlaka zetu zinajaribu kujifanya kuwa hili tatizo siyo big deal hadi kuruhusu mikusanyiko kama hii?
Hii ni aibu kubwa kwa raisi Magufuli, Waziri wa Michezo, Waziri wa Utalii na serikali nzima ya Mkoa wa Kilimanjaro, Waandaaji na Washiriki wote wasiochukulia tatizo hili kwa uzito wake, Ni aibu kubwa na kutokujali kwa kiwango cha juu kupitiliza! :
Hebu Tazama hili nyomi katikati ya Pandemic, hivi sis tuko serious!
Ila watanzania tunastahili lawama kwa kiwango cha juu sana, haiwezekani pamoja na taarifa zote kuhusu Corona zinazosambaa kwenye mitandao na vyombo vingine vya habari japo huko wanaita "nimonia", bado kuna watu hawachukui tahadhari mpaka leo.
Huu ni ujinga wa hali ya juu sana dunia nzima inatushangaa, hii Corona inatufanya tugeuke kivutio cha watalii kwa namna tunavyo deal nayo, bado tupo zama za old stone age kabisa.
1. Kwa vyovyote vile mtu/kijana mwenye uwezo wa kukimbia 40km+ mwanzo-mwisho hawezi kupata corona.
2. Vijana wengi wanasafiri na magari yao. So hakuna risk yeyote apo.
Covid sio ugonjwa hatari, umekuwa overated, nimeugua huu ugonjwa mara 2 na sasa nahisi naumwa corona nasubiria tu harufu ikate nianze dose. Mara zote 2 sikunywa dawa yoyote na nimepona. Death rate ni asilimia 3 ya waathirika wote hivo 3% ni ndogo sana.
Halafu eti uitishe Maombi ya siku tatu kumuomba Mungu aiponye nchi yako wakati hauko genuine, hauna dhati ya kupambana na tatizo. Huko siyo kutaka kulitumia jina la Mungu kisiasa tu?
1. Kwa vyovyote vile mtu/kijana mwenye uwezo wa kukimbia 40km+ mwanzo-mwisho hawezi kupata corona. 2. Vijana wengi wanasafiri na magari yao. So hakuna risk yeyote apo.
Mleta mada unachokiogopa wewe si lazima kila mtu akiogope Hiyo notion ya kudhani unachoogopa wewe kila mtu anapaswa kukiogopa haiko sahihi ndio maana hapo kuna waliovaa barakoa na wasiovaa
Mkuu wangu hapa naona Serikali tutaionea bure. Tunajua kabisa Head wa Serikali msimamo wake kuhusu Corona ulivyo, haamini kama ni Dangerous ki hivyo. Hapa ilikua tupambane tu sisi wenyewe.
Hapa cha kujiuliza ni kua sie wenyewe wakimbiaji tunakubalije kujichanganya namna hii? Hatujui kama huu ugonjwa ni hatari?
Natural Selection kama watu wanajijua wana matatizo alafu bila shuruti wanakwenda kwenye hatari; maybe wanastahili watakachokipata...., ila tatizo hilo janga wanalochuma wanakwenda kulila na wakwao...