Serikali lawamani kuruhusu Mkusanyiko wa Maelfu kwenye Kilimanjaro Marathon wakati Taifa linapambana na Virusi vya Korona

Serikali lawamani kuruhusu Mkusanyiko wa Maelfu kwenye Kilimanjaro Marathon wakati Taifa linapambana na Virusi vya Korona

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Watu walikuwa wengi kwelikweli, ni maelfu ya watu wamekusanyika kwa ajili ya kushiriki mashindano ya Kilimanjaro Marathon. Miongoni mwao wapo ambao hawakuvaa barakoa kabisa, na wamo amabao walizivaa na kuzivua.

Mkusanyiko wa mahali hapo ulikuwa ni mkubwa kiasi kwamba kaa kuna wstu wana virusi vya korona basi huenda kukawepo na usambazaji wa virusi kwa kiwango cha kutisha.

Katika mazingira kama haya, serikali inaruhusuje mikusanyiko kama hii?

Je, kufanya hivyo siyo kuhatarisha usalama wa Nchi?

Maana hawa watu wanatoka kila kona ya nchi. Je, namna hii siyo kusambaza virusi kwa kasi ya kutisha?

Serikali hii ndo inasema kuwaambia wananchi wafuate maelekezo ya wataalamu, lakini wakati huohuo inabariki na kusaidia kuwezesha mambo yote ambayo wataalamu wanashauri yasifanywe!

Leo kwenye mashindano hayo ya Kilimanjaro Marathon alikuwepo mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mama Mgwitra katikati ya msitu wa watu ambao hawajavaa barakoa waa kuweka social distance maana ni vigumu katika mkusanyiko huo kuweka hiyo social distance!

Kwa kweli inasikitisha, kuona serikali inajaribu kujifanya kuwa hili tatizo ni la mtu binafsi na si la Taifa kwa ujumla wake, otherwise niambieni kwa nini serikali inaruhusu miusanyiko kama hii inayoweza kupelekea usambaaji wa kirusi kuwa wakutisha? - Serikali inataka kuachieve nini?

Wananchi wanakufa kwa "changamoto", Tunawazika, na tunaendelea kushuhudia hii hali kila kukicha, mbona basi mamlaka zetu zinajaribu kujifanya kuwa hili tatizo siyo big deal hadi kuruhusu mikusanyiko kama hii?

Hii ni aibu kubwa kwa raisi Magufuli, Waziri wa Michezo, Waziri wa Utalii na serikali nzima ya Mkoa wa Kilimanjaro, Waandaaji na Washiriki wote wasiochukulia tatizo hili kwa uzito wake, Ni aibu kubwa na kutokujali kwa kiwango cha juu kupitiliza! :

Hebu Tazama hili nyomi katikati ya Pandemic, hivi sis tuko serious!

IMG_20210228_191744.jpg



IMG-20210228-WA0084.jpg


 
Ila watanzania tunastahili lawama kwa kiwango cha juu sana, haiwezekani pamoja na taarifa zote kuhusu Corona zinazosambaa kwenye mitandao na vyombo vingine vya habari japo huko wanaita "nimonia", bado kuna watu hawachukui tahadhari mpaka leo.

Huu ni ujinga wa hali ya juu sana dunia nzima inatushangaa, hii Corona inatufanya tugeuke kivutio cha watalii kwa namna tunavyo deal nayo, bado tupo zama za old stone age kabisa.
 
Ndio uwezo wetu wa kufikiri na kujiamulia ulipofikia!

Kuna watu nawaheshimu sana tena baadhi ni madaktari wa binadamu wamesafiri all the way kutoka dar na kwingineko ili wakasongamane!

Kila mtu na apambane na hali yake!
 
1. Kwa vyovyote vile mtu/kijana mwenye uwezo wa kukimbia 40km+ mwanzo-mwisho hawezi kupata corona.
2. Vijana wengi wanasafiri na magari yao. So hakuna risk yeyote apo.
 
Covid sio ugonjwa hatari, umekuwa overated, nimeugua huu ugonjwa mara 2 na sasa nahisi naumwa corona nasubiria tu harufu ikate nianze dose. Mara zote 2 sikunywa dawa yoyote na nimepona. Death rate ni asilimia 3 ya waathirika wote hivo 3% ni ndogo sana.

Screenshot_20210228-195058_Chrome.jpg
 
Mkuu wangu hapa naona Serikali tutaionea bure. Tunajua kabisa Head wa Serikali msimamo wake kuhusu Corona ulivyo, haamini kama ni Dangerous ki hivyo. Hapa ilikua tupambane tu sisi wenyewe.

Hapa cha kujiuliza ni kua sie wenyewe wakimbiaji tunakubalije kujichanganya namna hii? Hatujui kama huu ugonjwa ni hatari?
 
Natural Selection kama watu wanajijua wana matatizo alafu bila shuruti wanakwenda kwenye hatari; maybe wanastahili watakachokipata...., ila tatizo hilo janga wanalochuma wanakwenda kulila na wakwao...
 
Hivi mpaka leo Kuna watu wanaamin barakoa zinasaidia eeh.

Me nawashaur tu ikiwezekana hameni nchi nenden huko wanakoo vaa hizo barakoa na hawana misongamano.

Kwa usalama wenu zaidi.

Yaan tatizo watu hatuna shukran tunaangalia upinzan tu anayetupony corona ni MUNGU sio hizo barakoa
 
Back
Top Bottom