Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Watu walikuwa wengi kwelikweli, ni maelfu ya watu wamekusanyika kwa ajili ya kushiriki mashindano ya Kilimanjaro Marathon. Miongoni mwao wapo ambao hawakuvaa barakoa kabisa, na wamo amabao walizivaa na kuzivua.
Mkusanyiko wa mahali hapo ulikuwa ni mkubwa kiasi kwamba kaa kuna wstu wana virusi vya korona basi huenda kukawepo na usambazaji wa virusi kwa kiwango cha kutisha.
Katika mazingira kama haya, serikali inaruhusuje mikusanyiko kama hii?
Je, kufanya hivyo siyo kuhatarisha usalama wa Nchi?
Maana hawa watu wanatoka kila kona ya nchi. Je, namna hii siyo kusambaza virusi kwa kasi ya kutisha?
Serikali hii ndo inasema kuwaambia wananchi wafuate maelekezo ya wataalamu, lakini wakati huohuo inabariki na kusaidia kuwezesha mambo yote ambayo wataalamu wanashauri yasifanywe!
Leo kwenye mashindano hayo ya Kilimanjaro Marathon alikuwepo mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mama Mgwitra katikati ya msitu wa watu ambao hawajavaa barakoa waa kuweka social distance maana ni vigumu katika mkusanyiko huo kuweka hiyo social distance!
Kwa kweli inasikitisha, kuona serikali inajaribu kujifanya kuwa hili tatizo ni la mtu binafsi na si la Taifa kwa ujumla wake, otherwise niambieni kwa nini serikali inaruhusu miusanyiko kama hii inayoweza kupelekea usambaaji wa kirusi kuwa wakutisha? - Serikali inataka kuachieve nini?
Wananchi wanakufa kwa "changamoto", Tunawazika, na tunaendelea kushuhudia hii hali kila kukicha, mbona basi mamlaka zetu zinajaribu kujifanya kuwa hili tatizo siyo big deal hadi kuruhusu mikusanyiko kama hii?
Hii ni aibu kubwa kwa raisi Magufuli, Waziri wa Michezo, Waziri wa Utalii na serikali nzima ya Mkoa wa Kilimanjaro, Waandaaji na Washiriki wote wasiochukulia tatizo hili kwa uzito wake, Ni aibu kubwa na kutokujali kwa kiwango cha juu kupitiliza! :
Hebu Tazama hili nyomi katikati ya Pandemic, hivi sis tuko serious!