Serikali lawamani kuruhusu Mkusanyiko wa Maelfu kwenye Kilimanjaro Marathon wakati Taifa linapambana na Virusi vya Korona

Serikali lawamani kuruhusu Mkusanyiko wa Maelfu kwenye Kilimanjaro Marathon wakati Taifa linapambana na Virusi vya Korona

Ila watanzania tunastahili lawama kwa kiwango cha juu sana, haiwezekani pamoja na taarifa zote kuhusu Corona zinazosambaa kwenye mitandao na vyombo vingine vya habari japo huko wanaita "nimonia", bado kuna watu hawachukui tahadhari mpaka leo...
Tatizo hapa kwetu kila mtu ni mjuaji hivyo kutufanya kuwa wabishi
 
Ndio uwezo wetu wa kufikiri na kujiamulia ulipofikia!

Kuna watu nawaheshimu sana tena baadhi ni madaktari wa binadamu wamesafiri all the way kutoka dar na kwingineko ili wakasongamane!

Kila mtu na apambane na hali yake!
Kuna sehemu hapajakaa sawa na hili tutakuja kujilaumu sana baadae
 
Ukipata kirusi haiwi tena tishio kwako binafsi, bali unahatarisha maisha ya wengine ambao unaweza kuwaambukiza wakiwemo watoto na wazee wasiojiweza!
So mtu mzima anayejua kuna kirusi kinaua unasubiri serikali hii hii ya mawaziri wa tangawizi na malimao na season za nyungu iwahangaikie!
Hao wamejitakia, 90% wasomi, wanajua tahadhari ni pamoja na kuepuka misongamano isiyo ya lazima, barakoa, n.k Wanajua fika wakipata kirusi wakirudi majumbani wataambukiza familia.
Wanajitia hamnazo

Wacha wauza majeneza na wenye costa za kubeba maiti wapige hela.

Everyday is Saturday.............................. 😎
 
Hugo's pub kumeshona hatari..watu wamejazana ...yaani nyomi lote kutoka marathon limehamia hapo.....
 
Ila watanzania tunastahili lawama kwa kiwango cha juu sana, haiwezekani pamoja na taarifa zote kuhusu Corona zinazosambaa kwenye mitandao na vyombo vingine vya habari japo huko wanaita "nimonia", bado kuna watu hawachukui tahadhari mpaka leo....
Tuliomba Mungu kwa siku 3. Wala tusiwe na wasiwasi. Corona haipati kitu hapa!
 
Ila watanzania tunastahili lawama kwa kiwango cha juu sana, haiwezekani pamoja na taarifa zote kuhusu Corona zinazosambaa kwenye mitandao na vyombo vingine vya habari japo huko wanaita "nimonia", bado kuna watu hawachukui tahadhari mpaka leo...
Huu ni uthibitisho kuwa hakuna corona kivile!! Viwanja vya mpira vinajaa kila weekend!! Kwenye dala dala hakuna cha siti levo! Sokoni ndio usiseme!! Mashuleni, vyuoni!! Kama tungekuwa na corona yenyewe, ndani ya wiki moja pasingekalika!! Vifo havifichiki!! Vifo tunavyoshuhudia ni vya kawaida. Hakuna muda wowote usiokuwa na vifo!!

Hata kabla ya Corona kulikuwa na vifo!! Ila kwa kuwa vimetokea kwenye vuguvugu la tetesi za Corona basi kila anayefariki anabambikiziwa corona!! Ukitaka kujua corona inavyofanana nenda mexico au marekani!¡ Tanzania tunapaswa tumshukuru Sana Mungu kwa kutuepusha na corona!! Hata wazungu wanajua kuwa Tanzania hakuna corona!

Usione makelele yao, lengo lao ni kumnyima Mungu wetu utukufu na kujaribu kumkosoa Rais wetu!! Hivi hata kama huyo mtu ni punguani, hivi itawezekanaje tufundishwe kupambana na corona na nchi iliyopigika kwa corona hadi aibu? Marekani hawana ubavu wa kutufundisha namna ya kupambana na corona!! Wao ndio waje wajifunze kwetu!! Na Jambo la msingi ni kumtanguliza Mungu!
 
Tatizo moja tulilonalo watanzania, huwa tukiwaza korona tunafikiria mtu mmoja mmoja huwa hatuwazi hatari ya huyo mtu mmoja kwa wengine...
Jifungie wewe na familia yako kama unataka!! Hapo hakuna wa kukuambukiza !. Kuna aliyekuzuia kujiwekea lockdown?? Watanzania wengi ni wanafiki!! Utaikuta mtu anailalamikia serikali lakini mwenyewe hana hata habari ya barakoa!!

Mfano mzuri ni zytow!! Ziiiiitooooh!!! Huyu Bwana hakuna muda alijiwekea lockdown lakini Mara zote alikuwa anaiwekea shime serikali itangaze lockdown!! Huyu Bwana muda mwingi wala haukuwa anavaa barakoa lakini makelele hayamwishi!! Watu kama hawa si riziki kwa Taifa!
 
Sasa nimeelewa kwanini huyu Covid anawatembelea sana viongozi na wanachama wa CCM.

Kumeibuka genge maalum linalotaka kuishi kwa kufikirika kumridhisha Kiongozi Mkuu.

www.nytimes.com › style › the-psyc...
THE PSYCHOLOGY OF THE CULT EXPERIENCE - The New York Times

15 Mar 1982 — Dr. Cath defined a cult as a group of people joined together by a common ideological system fostered by a charismatic leader, where, he said, ''the expectation is that they can transcend the imperfections and finitude of life. '' He said: ''Often they set up a we-they philosophy: We have the truth and you do not
 
Hivi mpaka leo Kuna watu wanaamin barakoa zinasaidia eeh
Me nawashaur tu ikiwezekana hameni nchi nenden huko wanakoo vaa hizo barakoa na hawana misongamano
Kwa usalama wenu zaidi
Yaan tatizo watu hatuna shukran tunaangalia upinzan tu anayetupony corona ni MUNGU sio hizo barakoa
Na imeandikwa, usimjaribu Mungu wako.
 
Back
Top Bottom