CreativityCode
Senior Member
- Aug 8, 2020
- 158
- 653
Shalom from Jerusalem.
Mara nyingi viongozi wa serikali mmesikika mkisema na kuona fahari kuwa mko kwa ajili ya kuwatumikia wanyonge kama vile wao pekee ndiyo wenye haki ya kuishi.
Pia mmekuwa mkifanya propaganda kuionesha jamii unyonge wa watu wengi unasababishwa na sisi matajiri.
Mnaanzisha vitendo vya kuhujumu biashara zetu matajiri ili kupata uungwaji mkono na hao wanyonge wenu.
Napenda kuwakumbusha kuwa utajiri wetu unatokana na akili zetu za kubuni biashara zinazotuingizia fedha pia kufanya kazi kwa jasho na damu usiku na mchana.
Tunawekeza nchini. Tunatoa ajira kwa watu wengi na hivyo kustawisha jamii.
Miaka yote mmetubagua sana na kutuumiza kwa kupandisha kodi bila kuzingatia faida tuipatayo na kusababisha wengine tufunge biashara.
Hii si sawa. Badilikeni.
Nasi ni watanzania tunastahili heshima.
Kwa mujibu wa katiba nyie ni viongozi wa watanzania wote, matajiri na masikini, wenye nguvu na wanyonge hivyo tumikieni watu kwa usawa kwa mujibu wa sheria.
Angalizo:
Ni fahari na baraka kuwa tajiri.
Unyonge na umasikini ni laana