Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Mada hii imawahi zungumzwa humu. Naomba kukazia zaidi. Kama wewe ni mfanyabiashara utaona kuwa biashara inachanganya mwisho wa mwezi. Baada ya wiki hivi inakata kabisa. Unakuwa unadunduliza tu.
Ili walau biashara na mzunguko wa pesa uwe mzuri mwezi wote serikali na waajiri wengine wangefanya mpango huo mshahara ulipwe mara mbili kwa mwezi. Katikati na mwisho wa mwezi. Hii itasaidia kuchangamsha mzunguko wa pesa. Katikati ya mwezi kunakuwa kukavu sana vibarua na business za hapa na pale zinadorora.
Mtu anaweza kusema mbona kiasi cha pesa kwa mwezi ni kilekile, ni kweli lakini masuala ya kiuchumi huwa yanakuwa ya kimahesabu na ya kisaikolojia.
Zamani haikuwezekana sababu mishahara ilitolewa benki mkononi. Leo mtandao umerahisisha sana utumaji na upokeaji pesa.
Hebu serikali icheki hili. Mshahara utolewe kila baada ya wiki mbili. Hata kila wiki ikiwezekana. Mzunguko wa pesa ambao ni endelevu ni muhimu sana.