Serikali: Magari chini ya mwaka 2010 yasiingizwe nchini

Serikali: Magari chini ya mwaka 2010 yasiingizwe nchini

Nafikiri ndivyo ilivyo Kadiri gari inayoagizwa inavyokuwa ya Zamani na Kodi yake inakuwa kubwa.

Sasa hii Limit Ya Mh.Kasimu Inaenda Kuwaumiza WaTz sana.! Wengi Pesa za Kudunduliza ataweza Wapi kununua Gari Kisu cha 2017..?
Duh...Walala hoi Kazi tunayo...!

Vice versus
 
Hii kauli tunaweza kuichukulia poa lakini Kuna magari ya maana sana Hatutayaona tena yakiingizwa Nchini..
Haya yafuatayoView attachment 2181908View attachment 2181909View attachment 2181911View attachment 2181913View attachment 2181914View attachment 2181915
Magari Yoote haya yametengenezwa 2009 kurudi nyuma....

Siyo rahisi kutekelezeka kwa hyo kauli...

Sijui kama wanamaanisha kweli walichokisema
Tusubiri mheshimiwa Rais atasemaje maana huyu katelefoni siyo wa kumuamini sana maana hasemagi ukweli
 
Mmh hii ni ngumu kumeza aisee mimi IST nimenunua mwaka jana ya mwaka 2006 lkn chuma kimekuja kipya sanaaa sijui wazir mkuu anafikir barabara za wenzetu ndo kama zetu jmn, kwa hili sikubalian mana mfumo wetu wa kodi ni hovyo sana ist ya mwaka 2010 kwa uchache tutanunua 18m JR is it fair kweli?
 
Haitapotea ila tu bei yake itaimarika zaidi😅
Hawa wanajitekenya wenyewe, Tanzania bado sana- kama tupo kwenye uchumi wao wa makaratasi sawa, lakini kama ndo huu huu uchumi tunaoishi they are too theoretical.

Ni watanzania wachache sana wanaoweza kumiliki magari ya karibuni, unless kama wanataka kuturudisha enzi ambazo magari yanakutwa tu kwa Machifu.
 
Tumechelewa sana kuzuia nchi yetu kuwa jaa la mali chakavu. Hapo Kenya tu uamuzi kama huu waliufanya kitambo sana na maisha yanasonga. Kama kipato chako hakijafikia ngazi ya kununua gari, chukua chombo cha usafiri unachokimudu!
kenya na tanzania kiuchumi tofauti sana,kenya wana assemble magari mengi,tanzania labda wapige marufuku kuanzia 2000 kushuka chini...
 
Back
Top Bottom