Serikali: Makala ya BBC haina ushahidi. Tutachukua hatua kulinda uhuru, heshima na usalama wa nchi

Serikali: Makala ya BBC haina ushahidi. Tutachukua hatua kulinda uhuru, heshima na usalama wa nchi

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAKALA YA BBC

Serikali imesikitishwa na makala iliyochapishwa leo tarehe 13 Julai, 2026 na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kupitia kipindi chake cha "BBC Africa Eye" ambayo ime-beba maudhui ya upande mmoja, yaliyokosa ushahidi thabiti, yenye upungufu wa taar-ifa muhimu na yenye mwelekeo wa kuichafua heshima ya Tanzania Kimataifa.

Chombo cha habari cha BBC kimeendelea na mwenendo wake wa kuitangaza vibaya Tanzania kwa tuhuma nzito pasipo kutoa nafasi ya Serikali kujibu kama kinavyopaswa kufanya kwa mujibu taaluma ya uandishi wa habari licha ya Serikali kuwa tayari kutoa ushirikiano kama ambavyo kimefanya katika makala hii ambapo kilikataa kutoa nafasi kwa viongozi wawili wa upande wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kufuatia upungufu huu wa kiweledi ambao haukupaswa na hautegemewi kufanywa na chombo cha habari kinachotarajiwa kuwa na heshima kama BBC, Serikali ya Tanzania inachukulia kwa uzito mwelekeo wa maudhui ya BBC dhidi ya Tanzania na inafanya tathmini ya kina ya makala hiyo.
Mara tathmini hiyo itakapokamilika, Serikali itachukua hatua zenye lengo la kulinda uhuru, heshima na usalama wa nchi dhidi ya mashambulizi ambayo yanafanywa kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na kutoa ufafanuzi wa upo-toshaji na uchochezi wa makusudi uliojitokeza katika makala ya BBC.

Serikali inatoa wito kwa Watanzania wote kuwa makini na chokochoko zinazofanywa dhidi ya Tanzania kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, na inapenda kuwa-hakikishia wananchi wote kuwa itaendelea kusimamia misingi yote ya kudumisha amani, umoja na mshikamano wa Watanzania wote huku ikitekeleza afua mbalimbali za kukabiliana na changamoto zinazojitokeza kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa lengo la kuimarisha ustawi wa jamii.

IMG_20260713_193757_444.jpg

Pia soma; BBC News Africa: Tundu Lissu: A Fight Too Far?
 
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAKALA YA BBC

Serikali imesikitishwa na makala iliyochapishwa leo tarehe 13 Julai, 2026 na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kupitia kipindi chake cha "BBC Africa Eye" ambayo ime-beba maudhui ya upande mmoja, yaliyokosa ushahidi thabiti, yenye upungufu w]

Kila siku wanadai hivyo. Msigwa si awaombe kwenda kuongea nao na kueleza upande wa pili.

Hivi hata hiyo ya Lissu kupigwa risasi na serikali kushindwa kufanya upelelezi nayo bado wanajitetea....!?
 
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAKALA YA BBC

Serikali imesikitishwa na makala iliyochapishwa leo tarehe 13 Julai, 2026 na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kupitia kipindi chake cha "BBC Africa Eye" ambayo ime-beba maudhui ya upande mmoja, yaliyokosa ushahidi thabiti, yenye upungufu waamano wa Watanzania wote huku ikitekeleza afua mbalimbali za kukabiliana na changamoto zinazojitokeza kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa lengo la kuimarisha ustawi wa jamii.
View attachment 3628549
Nchi yetu imepoteza jina lake kwa haraka mno
 
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAKALA YA BBC

Serikali imesikitishwa na makala iliyochapishwa leo tarehe 13 Julai, 2026 na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kupitia kipindi chake cha "BBC Africa Eye" ambayo ime-beba maudhui ya upande mmoja, yaliyokosa ushahidi thabiti, yenye upungufu wa taar-ifa muhimu na yenye mwelekeo wa kuichafua heshima ya Tanzania Kimataifa.
a, kiuchumi na kijamii kwa lengo la kuimarisha ustawi wa jamii.
View attachment 3628549
Kwamba wauwaji wapewe ushahidi au hawajui ushahidi unatolewa wapi wasubir ICC ndio watauona ushahidi, upumbavu ni mzigo
 
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAKALA YA BBC

Serikali imesikitishwa na makala iliyochapishwa leo tarehe 13 Julai, 2026 na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kupitia kipindi chake cha "BBC Africa Eye" ambayo ime-beba maudhui ya upande mmoja, yaliyokosa ushahidi thabiti, yenye upungufu wa taar-ifa
Kuna siku serikal ilishakubali wanapikosea?
 
Msigwa kila siku anazungumzia weledi akijiona yeye ni mtaalamu kuliko watu wote duniani, zaidi ya BBC na waandishi wake wote.

Alisema pia dhidi ya VOA, DW na CNN kuwa hawana weledi wowote zaidi yake.

Sasa tishieni kuifungia BBC kama mlivyotishia FB na Instagram kama hawatafunga account za Mange na Maria Sarungi tuone.
 
Zamani ilikuwa congo sudan elitrea

Sasa hivi tanganyika aaah nyie **** mmetuharibia nchi sana. Demokrasia inazidi kuzorota na kuzoroteshwa. Viongozi wastafu wapo wanaangalia tu. TISS mpo kwa ajili ya maslahi gani?
Kuna kitu nitakisema lakini watu wengi wanaweza kutokubali. Ni suala la muda tu lakini.... mtakuja kujua: Mwarabu ana mkono kwenye kinachoendelea sasa hivi Tanzania. Tena sana.
 
4. MASHARTI NA MUDA MAALUMU (The Ultimatum)

Kutokana na mapendekezo ya Mjumbe Maalum, CMAG imetoa maelekezo yenye ukomo wa muda (Time-bound actions) kwa Tanzania:
Ndani ya Siku 30: Kutatua suala la kushikiliwa kwa Tundu Lissu kupitia njia za kisiasa au kisheria, na kuwaachia wengine wote wanaoshikiliwa kwa kutumia haki zao kwa amani.

Ndani ya Siku 60: Kurejesha upatikanaji kamili wa mitandao ya kijamii na kuacha vitisho dhidi ya vyombo vya habari na watetezi wa uhuru wa kujieleza.

Ndani ya Siku 90: Kuitisha jukwaa shirikishi na la kuaminika la vyama vya siasa (likiongozwa na mwezeshaji huru) kujadili mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi, ushindani wa kisiasa, wafungwa, na uwajibikaji.

Bila Kuchelewa: Kuanza uchunguzi huru wa makosa ya jinai uliopendekezwa na Tume ya Uchunguzi, pamoja na fidia kwa wahanga.

MWISHO WA UBAYA NI AIBU.
 
Msigwa kila siku anazungumzia weledi akijiona yeye ni mtaalamu kuliko watu wote duniani, zaidi ya BBC na waandishi wake wote
Alisema pia dhidi ya VOA,DW na CNN kuwa hawana weledi wowote zaidi yake.
Sasa tishieni kuifungia BBC kama mlivotishia FB na Instagram kama hawatafunga account za Mange na Naria Sarungi tuone.
Huyu ni mbwa tu. Wanaandika wengine yeye anapewa kusoma.
 
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAKALA YA BBC

Serikali imesikitishwa na makala iliyochapishwa leo tarehe 13 Julai, 2026 na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kupitia kipindi chake cha "BBC Africa Eye" ambayo ime-beba maudhui ya upande mmoja, yaliyokosa ushahidi thabiti, yenye upungufu wa taar-ifa muhimu na yenye mwelekeo wa kuichafua heshima ya Tanzania Kimataifa.

Chombo cha habari cha BBC kimeendelea na mwenendo wake wa kuitangaza vibaya Tanzania kwa tuhuma nzito pasipo kutoa nafasi ya Serikali kujibu kama kinavyopaswa kufanya kwa mujibu taaluma ya uandishi wa habari licha ya Serikali kuwa tayari kutoa ushirikiano kama ambavyo kimefanya katika makala hii ambapo kilikataa kutoa nafasi kwa viongozi wawili wa upande wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kufuatia upungufu huu wa kiweledi ambao haukupaswa na hautegemewi kufanywa na chombo cha habari kinachotarajiwa kuwa na heshima kama BBC, Serikali ya Tanzania inachukulia kwa uzito mwelekeo wa maudhui ya BBC dhidi ya Tanzania na inafanya tathmini ya kina ya makala hiyo.
Mara tathmini hiyo itakapokamilika, Serikali itachukua hatua zenye lengo la kulinda uhuru, heshima na usalama wa nchi dhidi ya mashambulizi ambayo yanafanywa kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na kutoa ufafanuzi wa upo-toshaji na uchochezi wa makusudi uliojitokeza katika makala ya BBC.

Serikali inatoa wito kwa Watanzania wote kuwa makini na chokochoko zinazofanywa dhidi ya Tanzania kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, na inapenda kuwa-hakikishia wananchi wote kuwa itaendelea kusimamia misingi yote ya kudumisha amani, umoja na mshikamano wa Watanzania wote huku ikitekeleza afua mbalimbali za kukabiliana na changamoto zinazojitokeza kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa lengo la kuimarisha ustawi wa jamii.


Pia soma; BBC News Africa: Tundu Lissu: A Fight Too Far?
Haina ushahidi!Mnao uhakika?
 
Back
Top Bottom