Serikali: Makala ya BBC haina ushahidi. Tutachukua hatua kulinda uhuru, heshima na usalama wa nchi

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAKALA YA BBC

Serikali imesikitishwa na makala iliyochapishwa leo tarehe 13 Julai, 2026 na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kupitia kipindi chake cha "BBC Africa Eye" ambayo ime-beba maudhui ya upande mmoja, yaliyokosa ushahidi thabiti, yenye upungufu wa taar-ifa muhimu na yenye mwelekeo wa kuichafua heshima ya Tanzania Kimataifa.

Chombo cha habari cha BBC kimeendelea na mwenendo wake wa kuitangaza vibaya Tanzania kwa tuhuma nzito pasipo kutoa nafasi ya Serikali kujibu kama kinavyopaswa kufanya kwa mujibu taaluma ya uandishi wa habari licha ya Serikali kuwa tayari kutoa ushirikiano kama ambavyo kimefanya katika makala hii ambapo kilikataa kutoa nafasi kwa viongozi wawili wa upande wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kufuatia upungufu huu wa kiweledi ambao haukupaswa na hautegemewi kufanywa na chombo cha habari kinachotarajiwa kuwa na heshima kama BBC, Serikali ya Tanzania inachukulia kwa uzito mwelekeo wa maudhui ya BBC dhidi ya Tanzania na inafanya tathmini ya kina ya makala hiyo.
Mara tathmini hiyo itakapokamilika, Serikali itachukua hatua zenye lengo la kulinda uhuru, heshima na usalama wa nchi dhidi ya mashambulizi ambayo yanafanywa kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na kutoa ufafanuzi wa upo-toshaji na uchochezi wa makusudi uliojitokeza katika makala ya BBC.

Serikali inatoa wito kwa Watanzania wote kuwa makini na chokochoko zinazofanywa dhidi ya Tanzania kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, na inapenda kuwa-hakikishia wananchi wote kuwa itaendelea kusimamia misingi yote ya kudumisha amani, umoja na mshikamano wa Watanzania wote huku ikitekeleza afua mbalimbali za kukabiliana na changamoto zinazojitokeza kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa lengo la kuimarisha ustawi wa jamii.

Pia soma; BBC News Africa: Tundu Lissu: A Fight Too Far?
Serikali imejiset kwenye DENIAL MODE.
 
Kuna kitu nitakisema lakini watu wengi wanaweza kutokubali. Ni suala la muda tu lakini.... mtakuja kujua: Mwarabu ana mkono kwenye kinachoendelea sasa hivi Tanzania. Tena sana.
However, a report from The Times' Martyn Ziegler has revealed that it wasn't a committee that made the decision at al, but rather a single person.

"There are 18 members of FIFA's disciplinary committee but the unprecedented decision to lift Balogun's automatic ban was taken by just one person – the chairman Mohammad Al Kamali of UAE. No one else was consulted," Ziegler reported on Sunday.
==================
Waarabu kweli wana nguvu, DP World, Loliondo etc, angalia hapo hadi FIFA jamaa anaamua kadi nyekundu ifutwe baada ya kuongea na Trump. Samia hapo ndiyo anapojiegemea
 
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAKALA YA BBC

Serikali imesikitishwa na makala iliyochapishwa leo tarehe 13 Julai, 2026 na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kupitia kipindi chake cha "BBC Africa Eye" ambayo ime-beba maudhui ya upande mmoja, yaliyokosa ushahidi thabiti, yenye upungufu wa taar-ifa muhimu na yenye mwelekeo wa kuichafua heshima ya Tanzania Kimataifa.

Chombo cha habari cha BBC kimeendelea na mwenendo wake wa kuitangaza vibaya Tanzania kwa tuhuma nzito pasipo kutoa nafasi ya Serikali kujibu kama kinavyopaswa kufanya kwa mujibu taaluma ya uandishi wa habari licha ya Serikali kuwa tayari kutoa ushirikiano kama ambavyo kimefanya katika makala hii ambapo kilikataa kutoa nafasi kwa viongozi wawili wa upande wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kufuatia upungufu huu wa kiweledi ambao haukupaswa na hautegemewi kufanywa na chombo cha habari kinachotarajiwa kuwa na heshima kama BBC, Serikali ya Tanzania inachukulia kwa uzito mwelekeo wa maudhui ya BBC dhidi ya Tanzania na inafanya tathmini ya kina ya makala hiyo.
Mara tathmini hiyo itakapokamilika, Serikali itachukua hatua zenye lengo la kulinda uhuru, heshima na usalama wa nchi dhidi ya mashambulizi ambayo yanafanywa kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na kutoa ufafanuzi wa upo-toshaji na uchochezi wa makusudi uliojitokeza katika makala ya BBC.

Serikali inatoa wito kwa Watanzania wote kuwa makini na chokochoko zinazofanywa dhidi ya Tanzania kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, na inapenda kuwa-hakikishia wananchi wote kuwa itaendelea kusimamia misingi yote ya kudumisha amani, umoja na mshikamano wa Watanzania wote huku ikitekeleza afua mbalimbali za kukabiliana na changamoto zinazojitokeza kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa lengo la kuimarisha ustawi wa jamii.

Pia soma; BBC News Africa: Tundu Lissu: A Fight Too Far?
Hakuna hata ushahidi wa Tundu Lissu kupigwa risasi?
 
Walipewa nafasi wakaikataa .
Hujajibu maswali yangu.

Ofisi ya spika, waziri wa mashauri ya kigeni, waziri wa mambo ya ndani hizo ni ofisi tatu tofauti zenye majukumu tofauti na ndio hii kasumba mtu akifikiri wizara ni mtu bali majukumu.

Sasa kama BBC waliandaa session tofauti kuwahoji watu kutoka ofisi hizi kwa nyakati tofauti hiyo serikali iliogopa nini kuwapa nafasi?

Kwanini mlazimishe spika ahojiwe katika session ambayo mtu ameandaa maswali kwa waziri wa mashauri ya kigeni?

Waziri wa mambo ya ndani hawezi kujibu maswali ya ofisi ya spika .

Hivi ndio BBC walikataa ombi hilo.

Nakuongeza maswali mengine.

Ndani ya miaka hiyo 9 serikali ilishawahi kutoa taarifa uchunguzi wa tukio hili umefikia wapi?

Je akina nani walitoa walinzi pale kabla ya tukio hili?

Nani anazo au alitoa amri ya kuondoa CCTV muda tukio linatokea?

Nani alikamatwa kama suspect juu ya tukio hili?
 
Hukuielewa hiyo documentary.
 
Hukuielewa hiyo documentary.
Wewe ndio hukuielewa..

Tena hiyo documentary wamechagua wachache sana wa kuwahoji kuna wengi sana walitakiwa kuhojiwa kuhusu hilo tukio ila naamini wamefichwa ili wasije kupasua ukweli.
 
Tunavuna tulichopanda, baada ya tukio dhidi ya Lissu yalitokea mambo mengi ambayo hayakujutia tukio lile, hayo ndiyo yametumika kama majibu au maelezo ya upande wa pili, tulishuhudia Bunge likidai Lissu ametoroka vikao vya Bunge hivyo hastahili kulipwa posho na mishahara yake! Kipi kipya itaieleza dunia, inavuna ilichopanda.
 
Back
Top Bottom