KQ meant Kenya broNi KC. King's counsel.
Mimi km 80 kila siku kwenda shule hata kwa pikipiki nisingeweza aisee mbali mnoMzee wa kutembea Kilomita 80 kwa miguu kwenda shule kila siku sio wa kumuamini.
Kadri mnavyojitetea ndivyo ukweli unabainika!TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAKALA YA BBC
Serikali imesikitishwa na makala iliyochapishwa leo tarehe 13 Julai, 2026 na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kupitia kipindi chake cha "BBC Africa Eye" ambayo ime-beba maudhui ya upande mmoja, yaliyokosa ushahidi thabiti, yenye upungufu wa taar-ifa muhimu na yenye mwelekeo wa kuichafua heshima ya Tanzania Kimataifa.
Chombo cha habari cha BBC kimeendelea na mwenendo wake wa kuitangaza vibaya Tanzania kwa tuhuma nzito pasipo kutoa nafasi ya Serikali kujibu kama kinavyopaswa kufanya kwa mujibu taaluma ya uandishi wa habari licha ya Serikali kuwa tayari kutoa ushirikiano kama ambavyo kimefanya katika makala hii ambapo kilikataa kutoa nafasi kwa viongozi wawili wa upande wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kufuatia upungufu huu wa kiweledi ambao haukupaswa na hautegemewi kufanywa na chombo cha habari kinachotarajiwa kuwa na heshima kama BBC, Serikali ya Tanzania inachukulia kwa uzito mwelekeo wa maudhui ya BBC dhidi ya Tanzania na inafanya tathmini ya kina ya makala hiyo.
Mara tathmini hiyo itakapokamilika, Serikali itachukua hatua zenye lengo la kulinda uhuru, heshima na usalama wa nchi dhidi ya mashambulizi ambayo yanafanywa kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na kutoa ufafanuzi wa upo-toshaji na uchochezi wa makusudi uliojitokeza katika makala ya BBC.
Serikali inatoa wito kwa Watanzania wote kuwa makini na chokochoko zinazofanywa dhidi ya Tanzania kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, na inapenda kuwa-hakikishia wananchi wote kuwa itaendelea kusimamia misingi yote ya kudumisha amani, umoja na mshikamano wa Watanzania wote huku ikitekeleza afua mbalimbali za kukabiliana na changamoto zinazojitokeza kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa lengo la kuimarisha ustawi wa jamii.
Pia soma; BBC News Africa: Tundu Lissu: A Fight Too Far?
Hao ndio majirani zetu mkuu;Siku nilipoona nchi imezama rasmi ni pale Samuya alipowaalika CNDD-FDD ya Burundi kwenye uapisho feki kule maporini kwenye kambi ya jeshi.
Ukisoma historia ya CNDD-FDD halafu mtu aseme atakua nao bega kwa bega unajua ni kwamba nchi imepiga hatua 10 nyuma.
Mwamba ana maisha magumu sana.... Sijui kama huwa wanamkumbuka hata kumfuta jasho japo kidogo kwa kazi ngumu anayoifanya...Msigwa ni mashine ya kuchakata propaganda ya mafisadi na majizi.
Atasemaje hakuna ushahidi wakati video inaonyesha hadi makovu yaliyotokana na risasi na mishono baada ya operation kubwa alizofanyiwa Lissu?
Kwahiyo Msigwa anataka kusema Lissu alijipiga risasi 32 kwenye gari yake na 16 akazielekezea mwilini mwake?
Wao miaka 9 ya ukimya inatoa mwanya vyombo vyenye independent reporting vifanye nafasi yao, hivyo policcm na usalama wa ccm hawana wa kumlaumu sababu hawawezi kuchunguza tukio walilopanga na kutekeleza wao.
Msigwa haoni aibu hata maaskari na wanajeshi wengine mpaka wamestaafu ni wameoteana vitambi hawajawahi kumbana na shambulizi la risasi.
Na video inaonyesha hata Lissu ambaye alikua na changamoto ya miguu anashikiliwa kwa nguvu na kundi la policcm.
TISS hawasikilizwi. ukishauri unaonekana uko upande wa Lissu. Hawako huru wanalinda kitumbua chao. Katiba mpya ipatikane ili wakuu wa Taasisi wapatikane kwa mfumo tofati na sasa. CDF,CPF,DGIS, ... anaweza kuondolewa kazini kama tufanyavyo kwa house girl/boy?Zamani ilikuwa congo sudan elitrea
Sasa hivi tanganyika aaah nyie **** mmetuharibia nchi sana. Demokrasia inazidi kuzorota na kuzoroteshwa. Viongozi wastafu wapo wanaangalia tu. TISS mpo kwa ajili ya maslahi gani?
serikali isiyotokana na WANANCHI, ni genge la wahuni tu.Kuna siku serikal ilishakubali wanapikosea?
Na wakipewa nafasi kazi yao ni kukanusha chochote hata kwa mambo yenye ushahidi wa kutosha.Hawa nao wanakera
Kila siku wanalalamika wao tu kutopewa nafasi.
Hamna kitu mle ni makada tu. Nao ni waathirika wa CCM na serekali yake kama zilivyo taasisi nyingine za umma.Hivi TISS imenyamazishwa kisiasa??
Anatumika vibaya sana yule ipo siku atabanananishwa.Mwamba ana maisha magumu sana.... Sijui kama huwa wanamkumbuka hata kumfuta jasho japo kidogo kwa kazi ngumu anayoifanya...
Majirani wauaji na wasiofuata haki za binadamu?Hao ndio majirani zetu mkuu;
Tatizo nyie machadema mnatazama sana movie hivyo mnadhani uhusiano wa nchi na nchi ni kujipendekeza kwa mabeberu tu.
Yaani matamko ya EU na senate ya marakani, jumuiya ya madola ndio nchi inakuwa Imepiga hatua kiuchumi.
Hakuna raha wanakula mkuu huku damu za watu zikiwalilia aisee hata waende wapi ni kizazi na kizazi vitapita kwao ili wawe salama sio leo..Hiki kitengo kinapitia wakati mgumu sana... Waliosababisha haya yote wapo huko nchi za mbali wanakula raha....
CNN ilivyotaka kupata CCM's side of the story immediately baada ya massacre 29th-Oct-2025 walikwepa lakini baada ya documentary kuwa released wakaanza kumshambulia Larry Madowo personally mpaka wakafikia kusema ni figisu za Wakenya ilhali yeye Larry pale CNN ni muajiriwa tu na ile ilikuwa ni habari ya CNN iliyohakikiwa na CNN kabla ya kurushwa hewani. CCM/Serikali/Grey Msigwa walilialia kuwahadaa wananchi wakati ni wao waliikwepa CNN wakiogopa maswali yasiyo ya Kichawa.
Haiwezekani BBC waharibu reputation yao kutoa habari ambazo hazijahakikiwa, CCM/Serikali/Msigwa/Samia wanajulikana kwa kubobea katika uongo, giliba na kukanusha ukweli kipumbavu hivyo hata hii habari kuikanusha Msigwa amelenga wapumbavu wenzake ambao anaamini watamuamini yeye zaidi ya wanavyoiamini BBC.
Msigwa hauna akili.
Alafu angalia hata majibu Yao, mepesi mepesiiiii!!! Ya kukulupukaaaaaZamani ilikuwa congo sudan elitrea
Sasa hivi tanganyika aaah nyie **** mmetuharibia nchi sana. Demokrasia inazidi kuzorota na kuzoroteshwa. Viongozi wastafu wapo wanaangalia tu. TISS mpo kwa ajili ya maslahi gani?