Serikali: Marufuku Kutumia Ramani ya Tanzania kutoka Google Kufundishia Wanafunzi, Inaonesha Ziwa Nyasa liko Malawi

Akili gani hii?
Yaani kijiji chote kiambiwe shamba si lako ila mwenye shamba uwaambie wanao shamba ni la kwako bila kuwarekebisha wanaosema shamba si lako?

Baada ya miaka kadhaa ukifariki unategemea watoto wako wapigane na kijiji kizima? Anza na anayefundisha watu kuwa shamba si lako atengue kauli.
 
Serikali imezuia matumizi ya Ramani za google kufundishalia wanafunzi kuhusu mipaka ya Nchi hususani mpaka wa Tanznaia na Malawi.

Kwa kutumia google,mpaka wa Tanznaia na Malawi uko pembezoni mwa Ziwa na Malawi wanadai ndio mpaka halisi wakati Ramani za Tanzania zinassma mpaka uko katikati ya Ziwa kama ilivyo Msumbiji na kwenye mipaka mingine yote ya Maziwa tuliyonayo.

Ikumbukwe Malawi wanaita Ziwa Malawi na ndio linajukikana hivyo huko google lakini hapa Tanzania ni Ziwa Nyasa.

View: https://www.instagram.com/p/DD7DDWgNEYr/?igsh=MWRmdDYyNXU4cGpweg==
View attachment 3183712

My Take
Malawi wakubaliane na mpaka mpya hakuna namna mpaka utakuwa mwambao wakati huko Mozambique mpaka uko katikati.
View attachment 3183715

Hapa suluhisho ni sisi upande wetu maji tuyamwagie rangi ya kijani.
 
Ina maana mgogoro huu ulipoibuka awamu ya nne na kumchagua Joachim Chisano kama msuluhishi, uamuzi wake ulitolewa kwa kificho? Kama hivyo ndivyo kwa nini wananchi hawakujulishwa kuwa mgogoro umeisha?
Google hawana makosa maana wanafuata mipaka ya kikoloni iliyowekwa na wajerumani/ waingeleza baada ya kuuziana vipande vya ardhi vya makoloni yao kwenye ule mkataba wa Heligoland ambao ulihusisha Malawi, Zanzibar, Heligoland na Namibia. Wamalawi wamesimamia hapo na ni haki yao maana mipaka ya kikoloni ndio iliyokubaliwa na OAU kuwa kipimo cha mipaka ya kila nchi inayojitawala.

Huu mgogoro ulipaswa kuamuliwa mapema baada ya uhuru, badala yake Nyerere akaamua kuunganisha Tanganyika na Zanzibar huku akijua kuwa mpaka wa Tanganyika kwenye ziwa nyasa ni ardhi yake sio katikati ya ziwa kama ilivyo kusini kwenye mpaka wa Malawi na Msumbiji....
Alaumiwe nani kama sio Nyerere na awamu zote zilizofuatia baada yake?
 
Kwa mujibu wa Google basi hata Msumbiji haina Ziwa Nyasa! 😁
 
Wataalamu wa wizara ya mambo ya nje hawakuona google? Wakawaambie google wa update mpaka huo isije kukuza mzozo hapo baadaye
Kwani wewe unadhani hao wataalamu wa mambo ya nje hawajui kuwa mpaka haupo katikati ya ziwa?
Unafikiri Google wanabahatisha au wanasubiri waambiwe wapi mpaka upo?
Google wametumia facts zinazojulikana na kukubalika kimataifa kusema wapi mpaka ulipo.
 
Ina maana mgogoro huu ulipoibuka awamu ya nne na kumchagua Joachim Chisano kama msuruhishi, uamuzi wake ulitolewa kwa kificho? Kama hivyo ndivyo kwa nini wananchi hawakujulishwa kuwa mgogoro umeisha?
Google hawana makosa maana wanafuata mipaka ya kikoloni iliyowekwa na wajerumani/ waingeleza baada ya kuuziana vipande vya ardhi vya makoloni yao kwenye ule mkataba wa Heligoland ambao ulihusisha Malawi, Zanzibar, Heligoland na Namibia. Wamalawi wamesimamia hapo na ni haki yao maana mipaka ya kikoloni ndio iliyokubaliwa na OAU kuwa kipimo cha mipaka ya kila nchi inayojitawala.

Huu mgogoro ulipaswa kuamuliwa mapema baada ya uhuru, badała yake Nyerere akaamua kuunganisha Tanganyika na Zanzibar huku akijua kuwa mpaka wa Tanganyika kwenye ziwa nyasa ni ardhi yake sio katikati ya ziwa kama ilivyo kusini kwenye mpaka wa Malawi na Msumbiji....
Alaumiwe nani kama sio Nyerere na awamu zote zilizofuatia baada yake?
Ukweli wa hitimisho ya yale mazungumzo ya usuluhishi ikiwa Tanzania tulipoteza umiliki wa ziwa hautakuja kuambiwa popote na serikali, itabakia kuwa ni siri au subiri wakina Lissu kuja kutufichulia.

Na ikiwa mazungumzo yale yalizaa matunda mazuri kwa Tz ninakuhakikishia ungekuwa ndio wimbo wa serikali na CCM kila mahali.
 
Serikali imezuia matumizi ya Ramani za google kufundishalia wanafunzi kuhusu mipaka ya Nchi hususani mpaka wa Tanznaia na Malawi.

Kwa kutumia google,mpaka wa Tanznaia na Malawi uko pembezoni mwa Ziwa na Malawi wanadai ndio mpaka halisi wakati Ramani za Tanzania zinassma mpaka uko katikati ya Ziwa kama ilivyo Msumbiji na kwenye mipaka mingine yote ya Maziwa tuliyonayo.

Ikumbukwe Malawi wanaita Ziwa Malawi na ndio linajukikana hivyo huko google lakini hapa Tanzania ni Ziwa Nyasa.

View: https://www.instagram.com/p/DD7DDWgNEYr/?igsh=MWRmdDYyNXU4cGpweg==
View attachment 3183712

My Take
Malawi wakubaliane na mpaka mpya hakuna namna mpaka utakuwa mwambao wakati huko Mozambique mpaka uko katikati.
View attachment 3183715

Safi sana kwa ili tamko.kutoka kwa Serikali yetu.

GOD BLESS TANGANYIKA
 
Mnaanza kuikimbia dunia na Teknolojia?
 
Kama mpaka upo nchi kavu na si kati kati ya maji, walete boat za kijeshi za doria ndani ya hilo eneo wanalodai ni lao.., au wazuie watz wasiguse hayo maji, halafu tutajua ukweli ni upi..
Mambo yote ya ziwa Nyasa yanatawaliwa na "International Riparian Law ya mwaka 1982"

Whether Waingereza walimaliza au hawakumaliza, there is no way Malawi watakuja pata total ownership ya lake Nyasa
 
Ukweli wa hitimisho ya yale mazungumzo ya usuluhishi ikiwa Tanzania tulipoteza umiliki wa ziwa hautakuja kuambiwa popote na serikali, itabakia kuwa ni siri au subiri wakina Lissu kuja kutufichulia.

Na ikiwa mazungumzo yale yalizaa matunda mazuri kwa Tz ninakuhakikishia ungekuwa ndio wimbo wa serikali na CCM kila mahali.
Huu ni mgogoro wa kidiplomasia ambao hautatuliwi kwa matamko kama tunavyoona huko chamani, Serikalini au kwenye mamlaka za kidola. Sidhani kama tuna wanadiplomasia wenye uwezo wa kujenga hoja, imebaki mabavu tu. Hebu fikiria, Malawi ni nchi ya kiafrika tena ndani ya SADC kama Tanzania bado tumeshindwa kukubaliana juu ya mipaka ya kikoloni.
Stergomena Tax amekaa SADC miaka kumi ningetegemea kuwa angelianzisha huko au alivyokuwa waziri wa mambo ya nje. Sasa yuko ulinzi, vipi nchi hizi mbili zikitishiana vita kama ilivyokuwa miaka ya sitini na sabini, kwa ajili ya mpaka, atakuwa na la kujitetea?..... Hii Autopilot itatugharimu pakubwa!.
 
Back
Top Bottom