Serikali mbili kuelekea moja v/s Serikali mbili kuelekea tatu: Nguvu za kimaslahi v/s nguvu za Kizalendo

Serikali mbili kuelekea moja v/s Serikali mbili kuelekea tatu: Nguvu za kimaslahi v/s nguvu za Kizalendo

KISHADA

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2012
Posts
2,226
Reaction score
3,293
Mwanzoni mwa miaka ya 80 na Mwishoni mwa miaka ya 90, ulikuwa ukihoji chochote kuhusu muungano uliandamwa sana na kuitwa muhaini. Tunakumbuka sakata la Aliyekuwa Rais wa Zanzibar wakati huo Mzee Jumbe la kulazimishwa kujiuzulu na sakata maarufu la kuchafuka hali ya hewa ya siasa Zanzibar iliyopelekea Viongozi kadhaa wa Serikali Zanzibar kufukuzwa Kwenye Chama (CCM). Mambo ni mengi lakini kwa ufupi ilikuwa ni vita ya Kizalendo baina ya pande mbili za muungano wetu. Wakati viongozi na watawala kutoka upande wa Bara walitumia nguvu nyingi kujenga muungano wenye nguvu na kutaka kuwa na nchi moja kutoka nchi mbili, wenzao wa Zanzibar walipigania nchi yao na uzalendo kwa Zanzibar.

Masuala ya kujiuliza hadi leo nini kilisukuma ajenda hizo kwa pande zote mbili? jee ni kwa sababu za Kizalendo za dhati au ubinafsi? Kwa nini kama kulikuwa na nia njema kuhusu Muungano wetu kusiandaliwe chombo maalumu cha utatuzi wa changamoto kisheria? Huko tuache.

Miaka ya 95 hadi sasa na kwa upande wa bara kuliiibuka mitazamo ya serikali mbili kuelekea tatu na kuzuka kwa kundi maalumu la G55. Kuanzia hapo hadi sasa kuna sauti za kudaiwa Serikali ya Tanganyika chini chini mpaka kuibuka kwa Mjadala wa katiba mpya miaka ya 2010. Watanzania wengi waliunga Mkono pendekezo la hoja ya serikali Tatu na kuona umuhimu sasa wa kuwepo serikali ya Tanganyika ambapo mwanzo hata kuitaja ulionekana muhaini. Nini kimepelekea yote haya?

Kwamba sasa madai ya kuwepo Tanganyika kama mshirika mwenza wa muungano hayachagizwi na upande wa Zanzibar Pekee baada ya muda mrefu wa malalamiko na sasa upande wa bara nao wanachagiza kulikoni? ni dhahiri kuna ufa umeonekana.

Huku ni kukua kwa hisia za kizalendo kwa pande zote. Makosa yanayoendelea kuibuka kwa gharama za kuulinda muungano wetu ili kuondoa kero kwa upande mmoja ndio huzalisha hisia na udadisi za kizalendo kwa upande mwengine. Wengine wakilalamika kubebeshwa mzigo na wengine wakilalamika kunyanganywa fursa zao. Mengi yamesemwa na wataalamu mbali mbali na kupendekeza mifumo tofauti kwa miaka kadhaa ingawa hadi sasa suala la Muungano kupatiwa ufumbuzi linaumiza kichwa na kuwagawa watu.

Limewagawa watu hadi kwenye chama Tawala CCM. Kundi la G55 lilitoka ndani ya CCM, Kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa Zanzibar miaka ya 80 kuliimega CCM na kufukuzana wenyewe na kuzaa upinzani mkali hadi leo.

Kwenye mapendekezo ya Rasimu ya Warioba ya Serikali tatu kuna mvutano baina ya CCCM wenyewe kwa wenyewe na baadae upinzani. Kwenye Bunge na Baraza la wawakilishi linaloongozwa na CCM kulikuwa na mvutano vile vile.

Nini kinakwamisha haya na kupata muungano unaoungwa mkono na wengi?

Mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 2009 yanayotambua Zanzibar ni nchi ni kielelezo cha wazi cha vita ya kizalendo kwa wazanzibari kwa nchi yao bila kujali itikadi zao.

Kwa upande wa Bara tuliona G55 na baadhi ya watu kuunga mkono serikali tatu. na kwa sasa kuna sauti zinavuma chini chini za Tanganyika kubebeshwa mzigo wa Zanzibar. Uko wapi uzalendo na wazalendo wa Tanganyika?

Kwa Watawala jee wakati haujafika wa kulitatua suala la muungano wetu na mnasubiri nini?

Tatizo hasa ni nini? Tukisema ni maslahi binafsi tutakosea?
 
Serikali mbili kuelekea moja ni nguvu ya kizalendo!
Inawezekana ikawa ni sawa lakini sasa hivi kuna mvumo wa sauti wa kuitaka Tanganyika iletwe tena kutoka upande wa pili wa bara, hali hii haijazoeleka kulikoni?
 
Back
Top Bottom