Tetesi: Serikali mbioni kuchapisha noti mpya, kuna hatari ya kuelekea kwa Mugabe, harufu ya tenda za kifisadi zatawala

Tetesi: Serikali mbioni kuchapisha noti mpya, kuna hatari ya kuelekea kwa Mugabe, harufu ya tenda za kifisadi zatawala

Kuna tatizo moja ambalo tunashindwa hapa
Kuna wasomi wa uchumi ambao wapo wengi mpaka mawaziri wastaafu lakini wanashindwa hata kulizungumzia au kutoa rai mbele ya camera au kwa simu.

Wanaoongea nao wanaogopa kutajwa that's a shame

Bado tuko nyuma sana likifika suala la kuelezea mambo makubwa na ya msingi katika taifa.
Huku wenzetu waandishi wa habari watawatafuta wahusika au mpaka wastaafu na kuwauliza kuhusu chochote kinachotokea na huwezi kukuta hata mmoja anajibu eti mimi sio msemaji wa serikali

Watu wanajibu wanachoelewa na ni rai tu na uelewa wao kutokana na wanachokijua.

Hela zipo ila zinaelekezwa kwenye miradi mikubwa lakini mradi unaweza ukaenda polepole na huku hela zingine zinatumika kwa kulipa mishahara nk huku tukitafuta zingine kwa kuendeleza miradi

Kuchapisha hela sio suluhu ila kuzalisha zaidi na kupeleka bidhaa nje kwa wingi ndio sehemu nzuri ya kupambana
Kama livestock wanapelekwa kwa wingi nje ni kuongeza maradufu na tujifunze pia kusafirisha matunda yetu na mboga kwa wingi nchi za maghribi na middle East

Hilo tumefeli sana siwasifii Kenya ila wako vizuri kwa hili na May kilichompeleka huko ni mambo kama haya akifikiria brexit itakuwaje anaanza kujiandaa

Ifike mahali tuwe aggressive likifika suala la kujitanua kibiashara na tuache uswahili mwingi

Sent from my SM using Tapatalk
 
Chonde chonde hizo noti mpya waweke sura ya Magufùli kwa juhudi zake alizozifanya
 
Mkuu,umenikumbusha kitabu fulani kinaitwa 'His Excellence The Head Of The State' humo ndani humo mwanamama kwa jina la Nelly Takida

Kuna mtawala alitaka kuchapisha fedha Nelly Takida akagoma kwa kumshauri asichapishe tena alimpa formula za kiuchumi mwishowe mwanamama Nelly Takida alipuuzwa na kiongozi wa nchi yake (Kilitania) ali-print noti nyingi sana na kuwapa tenda rafiki zake bila kufuata taratibu za zabuni za ununuzi...gues what happened then!!!!!!?

Sent using Jamii Forums mobile app

Doh umenikumbusha akina Lesoni Kiama
 
Noti hazichapishwi .kwa sababu,hela ya kuwap tanesco tutatoa wapi walip lile deni
Pili,ni matumiz mabaya ya fedha za umma kulipa makampuni ya kigeni(ukitoa wachina na japan) ambao ilbaki kidog tu watulize kweny electronic passport.
Ccm hoyee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kichwa cha Habari na Habari yenyewe Kuna makosa ya uandishi Au kupotoshwa. Kuna vitu viwili lazima vieleweke moja ni KUPRINT NOTE MPYA kwa maana ya mwonekano mpya. pili ni kuprint notes hizi zinazotumika mpya ziingizwe kwenye uchumi. Kuprint note mpya kwa maana ya mwonekano haina madhara kabisa kiuchumu Sana Sana itasaidia kiuchumu .HILI LA PILI NDIO JIPU. yaan kuprint notes hizi zinazotumika Hapo ndio hatari Sana.ukiangalia hali ya uchumi kwa Sasa haaitaji kuongezea fedha kwenye mzunguko kwa njia ya printing itatupeleka Zimbabwe kabisa bila chenga .serikali ijikite kukopa Au kutafuta wawekezaji wakubwa na stimulas package zingine. Serikali na BOT wanayo haki ya kuprint notes zingine lakini si kwa Sasa ambapo wote ni mashahidi benki zinafungwa na kupost profit kushuka pia biashara Kubwa nyingi zinafungwa na Hakuna wawekezaji wapya wakubwa. Serikali iache uchumi ujiendeshe wenyewe kwa kuwa na uwiano halisi baina ya production na money supply. STOP INJECTING NEW NOTES IN THE ECONOMY

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama hii ni habari ya kweli, niseme tu naunga mkono..tena waprint nyingi magunia na magunia halafu rais mwenyewe azigawe barabarani kama anavyofanyaga kutafuta misifa.Nafikiri tukiupata uchumi wa Venezuela and Zimbabwe combined, watanzania ndio watajifunza, watajifunza pia ku ignore movie za kipuuzi na za kijinga kabisa kama zile za makontena.
 
BAADA ya uchumi wa nchi kuyumba na maisha ya wananchi kuwa magumu, Rais John Magufuli anahaha kufyatua noti mpya.

SAUTI KUBWA inatambua kwamba tayari serikali imeshaanza mradi wa ufyatuaji wa noti hizo.

Hata hivyo, mradi huo umekwama kwa muda kwa sababu ya kugubikwa na sintofahamu kati ya rais na washauri wake; na miongoni mwa kampuni zilizoingia katika mchakato huo.

Kampuni za kimataifa ambazo zimetambulika kuingia katika mzozo huo ni De la Rue International, Oberthur Fiduciare, na M/s Crane Currency.

Vyanzo vinataja ufisadi katika mchakato kama sababu mojawapo iliyosababisha mzozo huo. SAUTI KUBWA inafuatilia habari za kina kuhusu mzozo huo.

Baadhi ya washauri wa serikali wanapinga ufyatuaji wa noti mpya wakidai utaongeza mfumuko wa bei, utashusha zaidi thamani ya shilingi ya Tanzania; na utafanya maisha ya wananchi yawe magumu zaidi.

Baadhi ya wachambuzi na wachumi waliozungumza na SAUTI KUBWA wanasema iwapo serikali itachapisha noti hizo nchi inaweza kukumbwa na mdororo wa kiuchumi kama uliokumba Zimbabwe katika utawala wa Robert Mugabe.

Mchambuzi mmoja amesema: “Itasababisha mfumuko wa bei za kila kitu kwa namna itakayoifanya shilingi yetu isiwe na thamani kabisa. Hiki ndicho alichokifanya Mugabe miaka ya nyuma baada ya kunyang’anya wazungu mashamba yao na vitega uchumi kutoka nje kukauka.

“Matokeo yake ni kwamba Zimdollar ilipoteza thamani hadi ikabidi ifutwe kabisa. Leo Zimbabwe haina sarafu yake yenyewe, na wananchi wanalazimika kutumia dola ya Marekani na rand ya Afrika Kusini kwa ajili ya manunuzi ya kila aina. Huko ndiko Magufuli anapotaka kupeleka Tanzania. Ataharibu kila kitu kilichobaki.”

Mchumi mmoja anayeheshimika nchini, ambaye SAUTI KUBWA haitataja jina lake, amezungumzia mfumuko wa bei na mzunguko wa fedha. Anasema:

“Mfumuko wa bei uko chini ya asilimia nne (4%). Si mbaya sana. Mzunguko wa hela ni kidogo. Hii ni mbaya. Kuchapisha hela ni uamuzi mbaya kiuchumi. Ujazo wa fedha katika uchumi lazima uendane na kiwango cha shughuli za uzalishaji katika uchumi. Kuchapisha hela ni njia ya ‘kiswahili’ ya kukabiliana na changamoto ya kiuchumi.”

Uamuzi wa Magufuli kuagiza ufyatuaji wa noti mpya, unaakisi kituko cha Idi Amini (dikteta wa Uganda 1971-1979) ambaye alipoelezwa juu ya upungufu wa fedha katika mzunguko, aliamuru benki kuu: “fyatua nyingi zaidi.”

Akijadili hali hii, mhadhiri wa uchumi anayeishi Marekani, anasema kwa kirefu:

Kwanza, tuanze na kujua sababu za lazima za kuchapa pesa. Hii ni kweli kuwa serikali haina fedha za kuendesha shughuli zake na kulipa madeni.

Pili, ni kwa nini serikali haina fedha? Kwa kawaida, ukiacha misaada, serikali ina vyanzo vikubwa viwili vya mapato: (1) Kodi, (2) kuuza dhamana au bonds.

Kwa hiyo, yawezekana ukusanyaji wa mapato ya kodi umepungua Ila serikali haisemi ukweli ili kijipatia sifa za kijinga.

Pia dhamana za serikali huenda haziuziki kama ilivyokuwa awali.

Mambo yote mawili, kupungua kwa mapato ya kodi na dhamana hutokea iwapo uchumi umesinyaa: hakuna uzalishaji wa kutosha kutokana na kudorora kwa uzalishaji kiuchumi.

Nini hufanyika? Serikali ingeweza kukopa zaidi. Huenda wakopeshaki hawapo tayari kwa kuwa kiwango cha uaminifu wa serikali kimeshuka. Utakupunga credit rating ya Tanzania imeshuka sana kwa sasa.

Pia, serikali ingeweza kubana zaidi matumizi yake. Lakini hili nalo Ni gumu sana kwa sasa kwa kuwa tayari imebana hadi ukomo wake. Kumbuka pia kubana matumizi ya serikali hupunguza ukuaji wa uchumi. Kudorora kwa sekta binafsi ni matokeo ya serikali kupana matumizi.

Nini matokeo ya kuchapa pesa? Uchapaji fedha huwa na madhara hasi kiuchumi iwapo uzalishaji haukui. Yaani, kutakuwa na fedha zaidi kwenye mzunguko zisizo na thamani. Matokeo yake ni mfumuko mkubwa wa bei. Kumbuka kilichotokea Zimbabwe kwa utawala wa Mugabe.

Mfumo wa bei usioendana na kipato halisi cha watu, utapunguza uwezo wa kutumia (purchasing power) na matumizi (consumption). Hapo uchumi utaendelea kuelekea shimoni zaidi.View attachment 853999


Kwan Tulipobadilisha Elfu Kumi ya Blue kuingia Elfu kumi nyekundu Uchumi ulidodora.

Hizo Ramli Chonganishi zimekaa kijuha-Juha
 
Hii taarifa imeletwa mara nyingi na imefutwa mara nyingi sana ! hongera mkuu kwa uzi wako kubaki
 
Back
Top Bottom