Tetesi: Serikali mbioni kuchapisha noti mpya, kuna hatari ya kuelekea kwa Mugabe, harufu ya tenda za kifisadi zatawala

Kuna tatizo moja ambalo tunashindwa hapa
Kuna wasomi wa uchumi ambao wapo wengi mpaka mawaziri wastaafu lakini wanashindwa hata kulizungumzia au kutoa rai mbele ya camera au kwa simu.

Wanaoongea nao wanaogopa kutajwa that's a shame

Bado tuko nyuma sana likifika suala la kuelezea mambo makubwa na ya msingi katika taifa.
Huku wenzetu waandishi wa habari watawatafuta wahusika au mpaka wastaafu na kuwauliza kuhusu chochote kinachotokea na huwezi kukuta hata mmoja anajibu eti mimi sio msemaji wa serikali

Watu wanajibu wanachoelewa na ni rai tu na uelewa wao kutokana na wanachokijua.

Hela zipo ila zinaelekezwa kwenye miradi mikubwa lakini mradi unaweza ukaenda polepole na huku hela zingine zinatumika kwa kulipa mishahara nk huku tukitafuta zingine kwa kuendeleza miradi

Kuchapisha hela sio suluhu ila kuzalisha zaidi na kupeleka bidhaa nje kwa wingi ndio sehemu nzuri ya kupambana
Kama livestock wanapelekwa kwa wingi nje ni kuongeza maradufu na tujifunze pia kusafirisha matunda yetu na mboga kwa wingi nchi za maghribi na middle East

Hilo tumefeli sana siwasifii Kenya ila wako vizuri kwa hili na May kilichompeleka huko ni mambo kama haya akifikiria brexit itakuwaje anaanza kujiandaa

Ifike mahali tuwe aggressive likifika suala la kujitanua kibiashara na tuache uswahili mwingi

Sent from my SM using Tapatalk
 
Chonde chonde hizo noti mpya waweke sura ya Magufùli kwa juhudi zake alizozifanya
 

Doh umenikumbusha akina Lesoni Kiama
 
Noti hazichapishwi .kwa sababu,hela ya kuwap tanesco tutatoa wapi walip lile deni
Pili,ni matumiz mabaya ya fedha za umma kulipa makampuni ya kigeni(ukitoa wachina na japan) ambao ilbaki kidog tu watulize kweny electronic passport.
Ccm hoyee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa walichapisha noti mpya ila mishahara ikabaki ile ile na maboom ya wanachuo yakawa yaleyale na hyo inflation itakayokuwepo!! Aisee maisha yatakuwa magumuuuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kichwa cha Habari na Habari yenyewe Kuna makosa ya uandishi Au kupotoshwa. Kuna vitu viwili lazima vieleweke moja ni KUPRINT NOTE MPYA kwa maana ya mwonekano mpya. pili ni kuprint notes hizi zinazotumika mpya ziingizwe kwenye uchumi. Kuprint note mpya kwa maana ya mwonekano haina madhara kabisa kiuchumu Sana Sana itasaidia kiuchumu .HILI LA PILI NDIO JIPU. yaan kuprint notes hizi zinazotumika Hapo ndio hatari Sana.ukiangalia hali ya uchumi kwa Sasa haaitaji kuongezea fedha kwenye mzunguko kwa njia ya printing itatupeleka Zimbabwe kabisa bila chenga .serikali ijikite kukopa Au kutafuta wawekezaji wakubwa na stimulas package zingine. Serikali na BOT wanayo haki ya kuprint notes zingine lakini si kwa Sasa ambapo wote ni mashahidi benki zinafungwa na kupost profit kushuka pia biashara Kubwa nyingi zinafungwa na Hakuna wawekezaji wapya wakubwa. Serikali iache uchumi ujiendeshe wenyewe kwa kuwa na uwiano halisi baina ya production na money supply. STOP INJECTING NEW NOTES IN THE ECONOMY

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama hii ni habari ya kweli, niseme tu naunga mkono..tena waprint nyingi magunia na magunia halafu rais mwenyewe azigawe barabarani kama anavyofanyaga kutafuta misifa.Nafikiri tukiupata uchumi wa Venezuela and Zimbabwe combined, watanzania ndio watajifunza, watajifunza pia ku ignore movie za kipuuzi na za kijinga kabisa kama zile za makontena.
 


Kwan Tulipobadilisha Elfu Kumi ya Blue kuingia Elfu kumi nyekundu Uchumi ulidodora.

Hizo Ramli Chonganishi zimekaa kijuha-Juha
 
Hii taarifa imeletwa mara nyingi na imefutwa mara nyingi sana ! hongera mkuu kwa uzi wako kubaki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…