Serikali: Miji ya Arusha, Dar, Zanzibar na Dodoma kuipaisha Tanzania kuwa Kitovu Cha Utalii wa Mikutano Duniani.Ukumbi wa 2 kwa Ukubwa Afrika kujengwa

Achana na majiji ya kenya nenda miji ya kawaida tu kama eldoret na kisii alafu uje ulinganishe na majiji yetu.
Hapo umenena mkuu πŸ˜€πŸ˜€ mi nlipita ka mji kanaitwa kericho kana flyover na bypass kabisa dah sisi huku maneno ndio mengi kama hiyo barabara ya kutoka mjini hadi usagara wako kwenye mpango wa kuitanua tangu 2004πŸ˜€πŸ˜€ sisi maneno ndio tunajua na kutiana moyo tu
 
Hiyo barabara ndio lango kuu la kuingilia Mwanza lakini ipo kama ulimi wa mbwa, ni makorongo, lami aieleweki kama ngozi ya mbwa koko, gari mbili haziwezi kupishana

Kwa Tanzania ukitaka kuona flyover nenda Dar peke yake huku kwingine acha tumalizane na kujenga zahanati na madarasa

Leo hii wadanganyika wanataka kulinganisha Tanzania na Kenya huwa naona kama vichekesho.
 
CHATO ndio kwaheri?

Salaam toka Kizimkazi.
 
Ila Watu wa Serikali mkome kudanganya ,hizi sio zama za Nyerere.

Ukumbi huo Mpya wa Arusha wenye capacity ya watu 3,500 unaweza usiwepo hata top ten achilia mbali uongo wa kusema utakuwa wa pili Afrika.

Bukifaso wanajenga Ukumbi mkubwa wenye uwezo wa kuchukua watu 5,000 Kwa pamoja Mjini Ougadougou.
 
Tanzania tuna Viongozi wapuuzi sana,sijui Kwa nini Huwa hawataki ku design vitu standards na classic.

Imagine wanajenga 4 lanes highway Mbeya ila Cha ajabu kwenye main intersection zote kama Uyole,Mafiati,Meta au hata CBD Mpya ya Mwanjelwa hakuna hata interchange au Flyover Moja badala yake ni ma keep left ya kisengerema Kila siku.

Hawa watu wanajua Miji inakuwa lakini pia wanajua kwamba miundombinu haijengwi tuu Kwa Ajili ya kuwezesha usafirishaji bali ni pamoja na kutoa taswira Mpya ya Jiji Kwa kuipendezesha but yanaishia kujenga local roads ,yanakera sana.

Kuna interchange au Flyover simple kabisa lakini holaaa.Kiukweli Tanzania inakera sana kana kwamba Majitu Huwa hayasafiri.Angalia Entebe,Kampala,Jinja na Sasa Mji Mpya wa mafuta kule Uganda Kuna miundombinu mikali achilia mbali Kenya.
 
Acha fix Mzee 😁😁😁😁😁
 
Serikali ya hovyo haifikirii kufufua kiwanda cha Tanganyika Packers, kingeleta ajira za kudumu, kiwanda cha nguo Urafiki, Kilimanjaro, Sungura, Mutex, Morotex, Mutex na vinginevyo ambavyo vingeleta ajira za kudumu badala ya umachinga, tutaendelea kuvaa mitumba mpaka lini?
 
Arusha hii hii ambayo haina stendi watu wa mwanza mnatucheka kila siku kwamba nyie mmependelewa mnazo mbili leo mnasema tena arusha inapendelewa ama kweli kuimba kupokezanaπŸ˜‚πŸ˜‚
Arusha inaenda kuanza Ujenzi wa Stand sio mda ,acha janja janja.
 
Toa ujinga wako,kiwanda hakifufuliwi na Serikali au na mtu yeyote Bali uwekezaji unaanza Upya.

Viwanda vya teknolojia ya Mwalimu inavifufuaje? Una spea? Kila kitu Kiko outdated unaleta ujinga wa kufufua?
 
Kwa Mbeya barabara za juu zinahitaji kuchimba mlima tu na unakuwa umepunguza gharama.
 
hilo jambo la msingi sana, Rwanda inapambana sana kupora taji la Arusha kwenye tasnia hiyo, na kama ilishaanza kufanikiwa. tukijenga ukumbi mzuri namna hiyo na wakajua kuna na package ya utalii palepale na kuuona mlima kilimanjaro, tutaipiku Rwanda vizuri sana na Arusha itabaki kuwa international town/city. Mungu imbariki Tanzania.
 
Kwa Mbeya barabara za juu zinahitaji kuchimba mlima tu na unakuwa umepunguza gharama.
Hapo umeongea upuuzi gani? Umesoma nilichoandika? Hiyo section inayojengwa inapita kwenye mlima upi wa kuchimbwa?

Mifano niliyotoa umeelewa? Umewahi Safiri Nje ya Tanzania wewe au unapayuka tuu.

Mijitu kama nyie ndio mnaharibu Miji yetu na hamna hata akili ya kujiongeza.
 
Rwanda Wanajenga Ukumbi wa watu 5,000 vs ukiambi wa watu 3,000 ,still Bado Rwanda atakuwa Juu.
 
Arusha itakuwa na package nzuri kuliko Rwanda, utalii, Mlima KIlimanjaro, karibu na Nairobi n.k.
Wapi hakuna Utalii? Hadi Sasa Rwanda Iko Juu ya Tanzania ,kuwa karibu na Nairobi kumekusaidia?
 
Toa ujinga wako,kiwanda hakifufuliwi na Serikali au na mtu yeyote Bali uwekezaji unaanza Upya.

Viwanda vya teknolojia ya Mwalimu inavifufuaje? Una spea? Kila kitu Kiko outdated unaleta ujinga wa kufufua?
Kwani umewahi kwenda maeneo hayo ukavikuta hivyo viwanda? Kumkashifu mtu usiyemjua ni udhaifu, JF ni kwa ajili ya hoja si matusi msenge wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…