saidoo25
JF-Expert Member
- Jul 4, 2022
- 624
- 1,456
Mwezi Septemba 2022 Bunge lilipitisha Sheria ya kuwasamehe kodi wawekezaji wakubwa na wabunge walishangilia sana Sheria hiyo kupita.
Leo TRA inashindwa kukusanya kodi kwa wawekezaji wakubwa kwa sababu tayari Mwigulu Nchemba ameshapitisha sheria yake bungeni ya kuwasamehe kodi sasa wanahangaika kuwakamata masikini.
LAPITISHA MUSWADA WA MAREKEBISHO YA SHERIA MBALIMBALI ZA FEDHA WA MWAKA 2022
23 Sep, 2022
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali za Fedha wa mwaka 2022 (The Written Laws (Financial Provisions) Amendment Act, 2022), ambao unalenga kufanya marekebisho ya Sheria 6 za kodi, mirahaba na uwekezaji.
Akiwasilisha Muswaha huo bungeni jijini Dodoma, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba alisema Lengo la Muswada huu ni kufanya marekebisho kwenye Sheria zinazosimamia kodi na mrabaha kwa kubadili viwango vya kodi na mrabaha.
Aliongeza kuwa Muswada huo unalenga kuweka taratibu za utoaji vivutio kwa wawekezaji ili kuhamasisha uzalishaji kwa viwanda vya ndani ya nchi vinavyozalisha mbolea na maguni ya mkonge, pamoja na kuondoa changamoto zilizopo katika utekelezaji wa Sheria ya uwekezaji Tanzania, Sura 38.
Mhe. Nchemba alizitaja Sheria zinazopendekezwa kufanyiwa marekebisho kupitia Muswada huo kuwa ni Sheria ya Ushuru wa Bidhaa Sura 147, Sheria ya Kodi ya Mapato Sura 332, Sheria ya Madini Sura 123, Sheria ya Ushuru wa Barabara na Mafuta Sura 220 na Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani Sura 148.
“Sehemu ya Pili ya Muswada yenye ibara za 3 hadi 5 inapendekeza kurekebisha Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, Sura ya 147, ambapo kifungu cha 128 kinapendekezwa kurekebishwa ili kumpa mamlaka Waziri mwenye dhamana na masuala ya fedha, baada ya kupata idhini ya Baraza la Mawaziri kusamehe ushuru kwenye bidhaa zitakazotumika katika utekelezaji wa miradi ya uwekezaji mahiri na mahiri maalumu itakayoidhinishwa na Kamati ya Taifa ya Uwekezaji (NISC)”, alifafanua Dkt. Nchemba.