Serikali mulikeni haya matumizi ya energy drink!

Sasa hao wanaopayuka hapo juu sijui tuwaelewaje bora umetoa somo mkuu
 
Alafu hiyo mo energy si peke yako..Kuna mtu aliwahi patwa na hali Kama yako alivyokunywa..nikajua labda atakuwa na matatizo yake binafsi..


Ni watu wengi wanaopatwa na shida baada ya kutumia hicho kinywaji sijui kwanini Serikali (TBS na TFDA) wapo kimya, ---- sitaki kuamini kama kuna rushwa imepita.
 
Wanaomiliki hivyo viwanda ni Waswahili?

Kinywaji gani kinakuwa na masharti asinywe mama mjamzito? hata pombe haina hayo masharti, wewe Kaput nini?
Mo Dewj
Bakhressa ni Raia wa wapi? Hiv kwa nini hampend Elimu?mnapenda ujinga na majungu? Akili mpaka zinaota kutu na fungus😂🐵👆
 
Hiyo kitu ikiwa baradi afu ukaichanganya na k.vant ni nomaa!!!
 
Waafrika wamepewa silaha, wanauana badala ya kulindana.

Wamepewa pesa badala ya kufanyia maendeleo wanaziiba.

Wamepata magari, Cha ajabu wanayatumia vibaya kwenda nayo kila kona na kusahau kufanya mazoezi hata kukimbia hatimaye wanapata maradhi yasiyoambukiza.

Wameletewa vyakula vya kiwandani wanafanya ndiyo diet wanakula hadi kusahau vyakula vyenye vitamins.

Sasa wakapata energy drinks, wanavinywa ili kushiba na kuhatarisha maisha yao.
 
Kazi ya Serikali ni kulinda watu mkuu...wewe kitu kina madhara ...Serikali kimyaaaa inakusanya Kodi!?
Serikali ipi inalinda hao ?.

Mwisho wa siku vijana wengi hamna stamina kisa energy drink
 
Kaza mwendo....umeoa!?😃😃😃
 
Effects zipi ndugu tueleze. Kwanza kampuni zote hizo mlizozitaja kuwa zinatengeneza mbona za Kiislam??? Nembo ya "Hallal" imetumika vibaya hapo. Poleni mnao falakatia kila kiwekwacho mbele yenu.
Uisilam unaingiaje hapo...Kuna sehemu kwenye Dini inazungumzuzia Energy drink
 
KVant au bapa na energy drinks vinaenda kweli....! Tunamix tu sasa wakipiga marufuku tutamix na nini wakulungwa
 
Nilishaapa sitakuja kunywa huo upuuzi maana ni addiction mbaya sana na vina madhara hasa kwa central nerve system
 
Hujaeleza matatizo yake ni nini
 
Tangu 2005 nimekuwa muhanga wa Pepsi, nimefanikiwa kuachana nazo
nilikuwa nakunywa hadi kumi kwa siku
Hivyo vi energy sijawahi vigusa, at least najua madhara ya caffein kwa mbaali
Caffein ndio inasisimua mwili ukitumia vinywaji ambavyo imechanganywa, vikiwemo hivyo vi energy
 
Vijana ni jalala la kila kitu.

Energy drinks, pombe, al-kasusu, Mundende, Kasongo power, Mwafya, Pweza etc
Yaani na wengi wamepata addiction ya hizi energy drink.. Ni kunywa tu kila wakati.. So sad
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…