Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu salam,
Tumeshuhudia na bado tunaendelea kuona matukio mbalimbali ambayo yanahusisha watu kutekwa huku wahanga wakubwa wakiwa ni wale ambao wanakosoa au kupinga mambo fulani kwenye mamlaka mbalimbali za serikali, wachache wanapatikana na wengine bado inaendelea kuwa kitendawili. Mbaya zaidi ni kuwa wananchi wakikimbilia polisi na kuiangukia serikali ili ndugu na jamaa zao wapatikane hapati msaada husika.
Kadri tunavyozidi kwenda wakosoaji wanaendelea kupata shuruba na matukio yakiongezeka bila kuona hatua yoyote ikichukuliwa. Mbali na hili kuna viongozi mbalimbali kutoka CCM wamekuwa wakitoa matamko mbalimbali yakiashiria kuhusika kwao kwenye matukio haya dhalimu lakini nao pia wanaishia kuondolewa tu kwenye nafasi zao au kupewa maonyo laini laini bila hatua stahiki kuchukuliwa kwao na kuisadia polisi kutokana na matamshi yao. Hii haileti picha nzuri na inazidi kuichafua serikali pamoja na mamlaka za usalama.
Hii si tu kwa kwamba inaumiza kihisia lakini pia inavunja moyo na imani kwa serikali na hata vyombo vya ulinzi kuwa wameshindwa kuwajibika kwenye nafasi zao na kuhakikisha kila mtu yupo salama na kujisi salama pia. Hili ni bomu linatengenezwa.
Kila unakopita ambako matukio haya yanatokea maoni ya watu wengi ni kuuliza kwanini mnawaangalia hawa na mnawajua (inapotokea waliotenda unyama huo wanajulikana), mmeshindwa kuwapiga kiberiti? Mmeshindwa kuwaitia wezi, huku wengine wakihamasishana kutembea na salaha.
Mnataka tufikie hatua ambayo kuuana iwe jambo la kawaida? Mnajisikia amani kutengeza chuki kubwa namna hii baina ya wananchi? Mauaji ya alaiki huanza hivi hivi, mtakuja kushtuka kuna vita kubwa kati ya wananchi wa kawaida na viongozi pamoja na familia zao.
Rais Samia amka, simama kidete, tunaelekea kubaya, act sasa kabla hatujafika huko, Bunge na Mahakama nanyi msituangushe. Sasa mnaona yanatokea kwa wananchi, pakiendelea kufukuta huku moto utawafikia tu ninyi.