DELETED ACCOUNT
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 9,805
- 15,476
Baada ya shughuli za kupongezana na kunyoosheana vidole kuisha, nadhani kuna namna inabidi Simba SC ikae chini na Serikali pamoja na TFF waangalie namna ya kuifidia Simba kutokana na upotevu wa mapato yaliyotokana na kushindwa kuutumia uwanja wa Benjamin Mkapa katika hatua hizi za mwisho za mashindano ya CAF hususani kwa ajili ya mechi ya fainali dhidi ya Berkane.
Fidia hii inaweza kuwa kwa njia ya cash moja kwa moja au kama hilo ni gumu basi kwa njia ya kupunguza au kuondoa makato yanayotakiwa kwenda kwa taasisi hizi katika mechi za nyumbani za Simba hadi pale kiasi fulani watakachokubaliana kitakapofika.
Katika fainali hii, Simba imepoteza mapato yanayokadiriwa kufikia shilingi milioni 800.
Tukumbuke pia katika mechi ya nusu fainali dhidi ya Stellenbosch iliyochezewa pia New Amaan Stadium Zanzibar, Simba pia ilipoteza mapato mengi kwa mechi kutochezewa kwa Mkapa, upotevu unaoweza kufikia shilingi milioni 500.
Hizi mechi zote mbili ni wazi zingekuwa full house pale Lupaso.