Naunga mkono hoja yako mkuu ya kuwa na unique namba kama za NIDA na mgonjwa akitibiwa sehemu inabidi visit yake ionekane National wise na pawepo na udhibiti endapo atataka kwenda kituo kingine bila sababu ya msingi yenye kuonesha ulazima wa kwenda huko.
Pia nilikuwa nawaza, hivi hamna namna pawepo na fingerprint ambazo zitalimit utoaji wa fomu za bima ili mgonjwa ahudumiwe, yaani ili mgonjwa ahudumiwe inatakiwa atumie finger print yake ili kuwezesha fomu yake kutolewa electronically ndipo iweze kujazwa na kusainiwa na pande zote mbili(Daktari na Mgonjwa). Hii itadhibiti mtindo wa fomu kusainiwa pasipo na huduma yeyote kama yanyofanyika kwenye Polyclinic ambapo Specialist anaenda kusaini tu fomu halafu hamna huduma yeyote ile.