Lukonge
JF-Expert Member
- Jul 31, 2015
- 1,469
- 2,086
Na wagonjwa siku hizi tuna-google, ukinitibu hivyo nakuona hufai kwenye taaluma yako na wewe ni kajanja! Nikija kwenye kituo chako na dawa fulani nikakosa najua kituo ni cha wababaishaji, sitajua kuwa haiwezekani kituo kikawa na dawa zote zinazohitajika kwa matibabu. Nikikukuta zahanati au kituo cha afya ukashindwa kunipa pantoprazole nitakushangaa (kumbe inatakiwa kutolewa na MD na wewe ni CO), ukiniambia basi kanunue au lipia unisaidie napiga simu NHIF nawaambia kituo kinanitoza pesa ili kiniibie! Nikija na kidonda Polyclinic na ukakataa kunifanyia dressing napiga simu NHIF kuwaambia mmekataa kunipa huduma mnataka pesa yangu (kumbe dressing haipo kwenye kitita kwa polyclinic).
Mtandao wa NHIF ukisumbua mkaniambia hebu subiri utengamae ili unipe huduma nasonya na kuwaambia nyie ni wababaishaji! halafu napiga simu NHIF kulalamika, NHIF wanakuwa wakali na kutaka mimi na wenzangu tupewe huduma ila tuache kadi. Lahaula tukiondoka na mtandao ukarudi unakuta mimi au mwenzangu kadi zetu zimekuwa rejected na tumeshatibiwa, kama umepata hasara shauri yako NHIF hawatakulipa.
Halafu kuna madaraja ya wagonjwa hatujui, nikija kutibiwa na akaja mwanachama wa fast track kama BOT, NMB au TRA anapitiliza moja kwa moja kwa daktari maalum huku nikiwa nimepanga foleni na wenzangu (naanza kulaumu jinsi watoa huduma walivyo na upendeleo na kujali rushwa) hee, kumbe mwongozo wa NHIF fasttrack anatakiwa apewe upendeleo maalum kwa sababu alilipa NHIF mpunga mrefu! Ghafla naona analazwa chumba cha peke yake na mimi nipo wodi ya jumuiya, nalalamika kwa daktari kwa nini aniweke wodi ya jumuiya wakati mteja mwingine wa NHIF kawekwa private ward. Hatari!!
😂😂😂Wewe utakuwa si mgonjwa umeamua kwenda kununua ugomvi tu kituo cha afya.
1: Ingawa suala la Polyclinic kunyimwa dressing!!?? Sijawahi elewa.
2: Pantoprazole, hiyo utaambiwa kwani hakuna Omeprezole (mgonjwa usichague dawa bali daktari ndiye hukuandikia).