Namna pekee ya kuunusuru huu mfuko usife, nikuongeza wanachama wapya ambao hawaumwi. Mfuko upambane kusajili watoto karibu wote kwenye shule za msingi na sekondari wawe na NHIF, vyuo vikuu vyote na vyuo vya Kati NHIF iwe lazima. Lakini pia mfuko uongeze siku za kuwa mwanachama Kwa watu wazima kutoka siku 30 hadi 120 (Wekeza,Najali, na Timiza Afya) hii itasaidia kuwepo Kwa uelewa wa pamoja kujiunga na NHIF bila kusubiri uumwe.
Pamoja na mambo yote niliyoshauri hapo juu, mfuko usiruhusu usajili mpya kwenye polyclinic zilizo karibu karibu Kwa sababu unachochea fraud kutokana na kwamba, wagonjwa wanakuwa wachache kwenye vituo vyao na kuwalazimu kupika madai ili waweze kumuda kuendesha. Lakini vituo vikiwa mbalimbali, Dr akawa anapata wagonjwa Kwa wastani wa 20 Kwa wakatimoja anakuwa busy na kupunguza ujanjaujanja wa + or - ambazo pengine wanafanya Kwa lengo la adjustment ili makato yakifanyika wasiweze kuingia hasara kubwa Kwa sababu NHIF na wenyewe wanawakata Sana na wakati mwingine sababu za msingi wanakuwa hawana. Naomba niishie hapo Kwa sasa niweze kuendelea na majukumu mengine asante.
Suala la usajili wa polyclinic siyo issue, tumeona matumizi ya live registration unatumika. Hizi hizi za live registration/electronic bado wagonjwa ni walewale wengi. Ingawa NHIF pia walikuwa na wasiwasi, ukipeleka wanakwambia " mbona folio nyingi, wagonjwa mnatoa wapi??". Polyclinic moja inaona watu 80-100 kwa siku, huku imezungukwa na vituo vya serikali. Kuna vitu ambavyo vinafanya watu wageukie polyclinic:
1: Huduma zisizotoshereza kwenye baadhi ya vituo vya afya, ikiwemo vya serikali. Ukimuuliza mgonjwa ka nini haujaenda pale, wakati ni karibu ukamleta mgonjwa kama huyu huku mbali? anakwambia mimi pale sipaelewielewi.
Mfano: mtoto ana homa kali au amebanwa kifua, unamweleza mgonjwa ni vizuri kwanza angepatahuduma pale karibu na anapoishi.
2: Wagonjwa wa NHIF kuwa halfly treated kwa watu kuogopa makato.
Mgonjwa ana kikohozi na mafua. Anapewa dawa ya kikohozi na mafua unanikata mojawapo. Kesho akija atapewa mojawapo, mfano: atapewa ya mafua au kikohozi tu. Ili kukwepa makato.
Akiona mambo yanaendelea, anaenda kufanya consultation kwaajili ya dawa ya mafua yaliyoachwa bila kutibiwa. Na hasa haya ya sasa ni kisilani kweli.
Ingawa kuna self limiting flue and cough, lakini kama mtaalamu kafikia kumpa then wewe ukiwa ofisini unakata tu.
Ukiulizwa kwa nini mmekata: Unajibu, nadhani mlikuwa na dawa zinakaribia ku-expire mkaamua kuzitoa au mnatoa sana dawa za mafua(mtu hajui haya magonjwa ni seasonal).
Unashauriwa: tafuta cough mixture yenye multipurpose, of which ziko more expensive.
3: Tunang'ang'ana na STG kama msahafu wakati hutufanyi resistance patterns ya dawa kwenye jamii yetu ili kuwa objective and scientific. Unapataje STG kwa kukusanya tu matabibu bila data zozote kutengeneza muongozo? Hivyo, watu tunanaogelea humo blindly. At least tungefanya zonal wise ili tuwe na ushauri unaoendana na hali halisi. Ukifanya wewe C/S, mnafanya vipimo sana?? Kumbe wewe umetibia na mtu amerufi bila better response.
4: Wagonjwa kutokufanyiwa vipimo wakati mwingine hata kama wanastahili kwa kuogopa makato. Mgonjwa anaelekezwa kituo Y kufanya vipimo kwa sababu kituo B wanaogopa wakifanya vipimo wataishia kukatwa.
5: Wagonjwa kuambiwa hapa hutapata huduma kwa sababu jana mtoto/mgojwa huyu alitibiwa hapa jana.
6: Unapata mgonjwa ana fangusi na muwasho, unampatia combined(antifungal na antipruritus), mtu anakata.
Maana ya:
1: Huyu mtu umpe antifungal peke yake? Kesho ataenda kutafuta dawa ya muwasho??
2: Umwandikie separate tubes antifungal na antipruritus of which is very expensive.
7: Hili litaenda kuumiza tena kwenye form 2C kwa wazee ambao ni DM na HTN au long term/life long illnesses. Kwani wakikosa dawa hizo obviously watakuwa wanafanya multiple shopping ili mpaka watimize idadi ya dawa zao. Hii itakuwa shida sana kwa wagonjwa wenye magonjwa ya kudumu mgano yule ambaye ni DM and HTN aje ku-refill, mpaka abahatike kupata sehemu moja yenye dawa zote. Ni ngumu kuamini kuna hospitali itakuwa na dawa zote za Bp, Dm, Osteoporosis, Pumu, Kifafa nk. Labda kama kila mara utazibadili, kitu ambacho si practice.
Mgonjwa atakuja ana hitaji la dawa ya level S kwenye Polyclinic au Zahanati, kosa la nani hapo? Wakati huo, CO, AMO na MO hawaruhusiwi ku-refill.
Na wao hawajui levels za dawa.
NB: Wagonjwa wengi wataendelea kuzurula mahospitalini kwa expense za hela iliyoko kwenye mfuko. Multiple consultation ili apate dawa zake zote. 🤔🤔🤔
Kuna mambo NHIF inafanya, ni kama kukata mti uliokalia.