... ni watoto wetu; ni taifa la kesho; bila wao kesho hakuna kizazi. Serikali ifanye jitihada za maksudi kuwanusuru hawa mabinti. Hatua mojawapo ni kupiga marufuku kabisa hizo P2 maana zinawatia wazimu; wanaogopa mimba kuliko ukimwi; wanajiona wako salama dhidi ya mimba wakati wanapukutishwa kwa HIV.
Pili, binadamu tuna tabia ya kujisahau sana. Awareness campaigns dhidi ya ukimwi zihimizwe kwenye ngazi zote hadi ngazi za mitaa na vijiji. Bodaboda, bajaji, mabar, kumbi za starehe, n.k. vimeongeza sana risk ya maambukizi so ni muhimu Serikali ije na mbinu mpya pia. Tunaposema "Not to be sold to under 18" hivi kuna mtu anajisumbua kuhakikisha inazingatiwa?