Serikali, punguza kodi ya Sukari sio Pombe

Serikali, punguza kodi ya Sukari sio Pombe

idawa

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2012
Posts
25,284
Reaction score
38,364
Sukari ni kiungo mhimu kabisa kwenye maisha ya Mtanzania, haijalishi matajiri au maskini lazima atumie sukari.

Binadamu woote bila kujali mzima ama mgonjwa lazima atatumia sukari.

Ndio maana sukari ikiadimika nchi inatikisika.

Lakini ajabu tunapunguza kodi kwenye Pombe. Yaani Watanzania waongeze bidii ya kulewa...mnataka kujenga Taifa la aina gani.?

Malawi,Zambia,Kenya na Uganda sukari haizidi 2000 hao ndio majirani zetu..sasa magendo yataisha vipi?

Ndio maana biashara ya magendo ni ngumu kuisha sababu ya ukiritimba kama huu.

Punguza kodi ya Sukari, ongeza kodi ya Pombe.

Sababu hata walevi lazima watumie sukari kama sio wao Basi familia zao lazima zitumie.
 
Acha wapige vyombo[emoji2]
IMG_20210313_122001.jpg
 
Mwigulu na cabinet yake katika Wizara Ya Fedha walivyo wendawazimu, wamekaa vikao huko na kulipana posho kutoka kwenye kodi zetu halafu wanakuja na bajeti yao ambayo wanaacha kuongeza kodi kwenye "BIDHAA ZA STAREHE & ANASA" wanakwenda kuongeza kodi kwenye "KILIMO". Hapo wanajiona wameandaa bajet moja nzuri sana inayohitaji kusifiwa.

Hii nchi kuna mawaziri ni kichefuchefu, kuna mambo wanafanya hata kwa mtu alieishia darasa la 3 St.Kayumba anawashangaa na kuwaona majuha.

Tukiwasema hovyo humu kwenye mitandao, kuna watu wanakuja kuwatetea mpaka mishipa ya sehemu za siri inawasimama.
 
Aisee usifananishe pombe na vitu vya kijinga tafadhali sana 😃

Sukari Ina siasa yake kama madini na kuna watu wameikamata vizuri hata Magu alishindwa Ile vita akaishia kusema watu wanahodhi sukari Ila hajakamata hata mtu mmoja.

Hiyo biashara Hadi Kenya inawasumbua aisee MUMIAS wamekamata kule hapa bongo waulizwe ILLOVO ambao ndio mtibwa na kagera sugar.

Imagine mpaka Bakhresa amejiingiza kulima na ana kiwanda kinamalizika pale Bagamoyo utamu ni biashara nzuri Hadi ule utamu wetu mwingine 😃😃
 
Wanywa juisi ndio mnahitaji sukari kushinda sisi wazee wa mtori na supu na mkitaka ugomvi ongezeni Kodi kwenye chumvi na ndimu😃😃😃😃
 
Sukari haifai,

Sukari inasababisha magonjwa,Ukiugua kisukari
1. Utapoteza Nguvu za kiume
2. Utakaribisha shinikizo la damu
3. Unaweza kupofuka
4. Ukipata kidonda huponi
5. Ukimbukizwa Corona umekwisha

Hayo yote huwezi kuyapata Kwenye pombe.

TUSIPOTOSHANE, Acha wanywe bia[emoji2]
View attachment 1818870
Kwa maradhi uliyoorodhesha hapo moja kwa moja n maradhi almaarufu kwa matajiri na sio watu wa hali ya chini/kati,,,, N heri serikali iangalie uwezekano wa kupunguza kodi kwenye sukari ila sio kwenye pombe......Unless otherwise wananchi wataendeleza biashara za magendo tu
 
Wasituzoee aisee tumewavumilia sana
Yaani watuache kabisaaaaa! Mimi hapa nimeishadondosha K Vant ya 10,000/ peke yangu ndani ya lisaa limoja halafu unilinganishe na watu ishirini wanaotumia nusu kilo ya sukari ya sh. 1,200/?
 
Kwa maradhi uliyoorodhesha hapo moja kwa moja n maradhi almaarufu kwa matajiri na sio watu wa hali ya chini/kati,,,, N heri serikali iangalie uwezekano wa kupunguza kodi kwenye sukari ila sio kwenye pombe......Unless otherwise wananchi wataendeleza biashara za magendo tu
Watuache na pombe zetu, tukijilewea tunahitaji supu na mtori kiungo chumvi tu nashangaa watu wanahangaika na sukari ili iwe nini?
 
Sukari ni kiungo mhimu kabisa kwenye maisha ya Mtanzania, haijalishi matajiri au maskini lazima atumie sukari.

Binadamu woote bila kujali mzima ama mgonjwa lazima atatumia sukari...
Pombe nayo kinywaji tafadhali tafuta chanzo kingine cha mapato! Pombe achana nayo kwani mchango wake kwa uchumi wa nchi hii haina mfano!
 
Back
Top Bottom