Serikali punguzeni utitiri huu wa Taasisi ni mzigo kwa walipa kodi

The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2021
Posts
19,582
Reaction score
14,167
Nawasalimu kwa jina la JMT..na Kazi iendelee.

Ifike wakati serikali ichukue maamuzi magumu na yenye tija kwa Taifa kwa kupunguza utitiri wa Taasisi zake zilizo chini ya Wizara mbalimbali.

Ukiacha kwamba hazina tija kwa Nchi bali ni mzigo mkubwa sana wa walipakodi wa Tanzania kwani zinaongeza gharama za utawala zisizo na msingi na kuleta urasimu,gharama na usumbufu kwa wananchi.

Serikali chukueni hatua ya kuziunganisha na kufuta zile zisizo na tija.

Just imagine Wizara moja ya Viwanda na Uwekezaji ina Taasisi zaidi ya16 zilizo chini yake.Sasa piga hesabu kuna zaidi ya Wizara ngapi hapa Tanzania.

Hamuoni kuwa na lundo la Taasisi kunaongeza urasimu,usumbufu na gharama zisizo za msingi kwa wawekezaji na wananchi?

Kwa kuwa mh.Rais wewe ni Msikivu na Ili kuleta ufanisi ,basi shughulikia na hili maana imekuwa ni kichaka cha upigaji wakati ufanisi ni zero👇

Screenshot_20220519-150425.png
 
Mkuu, hizo Taasisi karibia zote ulizozitaja zina umuhimu wake kwa Taifa.

EPZA, TEMDO ,CAMARTEC, TANTRADE, TIC, BRELA ,NDC, FCC, TBS, WMA na FCT .

Binafsi kila Taasisi nilizozitaja Hapo juu naelewa dhumuni la kuanzishwa kwake,kazi zake na manufaa yake kwa ujumla.

Kama ulipitia chuoni na ukasoma kozi za biashara Huwezi kumalizia degree bila kuzichambua baadhi ya hizo Taasisi.

Taasisi ndani ya wizara ni viungo muhimu mno, ambavyo hukamilisha wizara husika. Lengo la kuwa na Taasisi ni mgawanyo wa majukumu ili kupunguza wigo mkubwa wa kimamlaka.
 
Mkuu, hizo Taasisi karibia zote ulizozitaja zina umuhimu wake kwa Taifa.

EPZA, TEMDO ,CAMARTEC, TANTRADE, TIC, BRELA ,NDC, FCC, TBS, WMA na FCT .

Binafsi kila Taasisi nilizozitaja Hapo juu naelewa dhumuni la kuanzishwa kwake,kazi zake na manufaa yake kwa ujumla.

Kama ulipitia chuoni na ukasoma kozi za biashara Huwezi kumalizia degree bila kuzichambua baadhi ya hizwao Taasisi.

Taasisi ndani ya wizara ni viungo muhimu mno, ambavyo hukamilisha wizara husika. Lengo la kuwa na Taasisi ni mgawanyo wa majukumu ili kupunguza wigo mkubwa wa kimamlaka.
Pamoja na huo umuhimu,hakuna sababu ya kuwa na utitiri wa Taasisi zinazofanya Kazi zinazofanana..mf.(TIC,TanTrade,BRELA),FCC na FCT,WMA na TBS,(TEMDO, CARTEC,SIDO,TIRDO)

Hatuwezi kwenda kwa staili hii.
 
Ebu njoo na mfumo wako watu waujadili...
Ila mimi ni muumini wa ugatuzi...
Tatizo kubwa lilopo taasisi/idara nyingi za serikali zinafanya competition badala ya coorpetition.
Na sekta binafsi ndo zinaogopwa hazipewi ushirikiano kabisa!
Tuanzie hapo... Ila wingi wa taasisi/idara si hoja kubwa!
 
Nawasalimu kwa jina la JMT..na Kazi iendelee..

Ifike wakati serikali ichukue maamuzi magumu na yenye tija kwa Taifa kwa kupunguza utitiri wa Taasisi zake zilizo chini ya Wizara mbalimbali..

Ukiacha kwamba hazina tija kwa Nchi bali ni mzigo mkubwa sana wa walipakodi wa Tanzania kwani zinaongeza gharama za utawala zisizo na msingi na kuleta urasimu,gharama na usumbufu kwa wananchi.

Serikali chukueni hatua ya kuziunganisha na kufuta zile zisizo na tija.

Just imagine Wizara moja ya Viwanda na Uwekezaji ina Taasisi zipatazo 16 zilizo chini yake.Sasa piga hesabu kuna zaidi ya Wizara ngapi hapa Tanzania.

Hamuoni kuwa na lundo la Taasisi kunaongeza urasimu,usumbufu na gharama zisizo za msingi kwa wawekezaji na wananchi?

Kwa kuwa mh.Rais wewe ni Msikivu na Ili kuleta ufanisi ,basi shughulikia na hili maana imekuwa ni kichaka cha upigaji wakati ufanisi ni zero👇

View attachment 2230589

Hayo mataasisi ndio watu wamekwekwa humo na wapwa zao wale mema ya nchi. Ukija kwenye makodi tunayolipa ya mafuta vocha, hayo matasisi yote yana mgao... ni mbinu tu za kutunyonya. Inakera sana. wizi wizi tu.
 
Pamoja na huo umuhimu,hakuna sababu ya kuwa na utitiri wa Taasisi zinazofanya Kazi zinazofanana..mf.(TIC,TanTrade,BRELA),FCC na FCT,WMA na TBS,(TEMDO, CARTEC,SIDO,TIRDO)

Hatuwezi kwenda kwa staili hii.
TAN TRADE hupromote biashara za ndani na huandaa maonesho ya kibiashara reference ni maonesho ya sabasaba ni Kati ya kazi chache inazofanya.

BRELA ni Business Registration And Licensing Agency..Ni msajili wa makampuni na mtoaji wa leseni.

TIC Hii ni Investment Centre Mkuu, hawa hudeal na shughuli zote za uwekezaji ndani ya Tanzania.

How comes useme wanafanya kazi zinazofanana?
 
Kwa hiyo hayo majukumu hayawezi fanywa chini ya Taasisi moja ambayo ina vitengo tofauti? Kuna ulazima gani wa kuwa na ofisi kwa kila Taasisi?

Ndio maana tunasema ni majukumu yanayofanana na yako kwenye wizara moja.
 
Hayo mataasisi ndio watu wamekwekwa humo na wapwa zao wale mema ya nchi. Ukija kwenye makodi tunayolipa ya mafuta vocha, hayo matasisi yote yana mgao... ni mbinu tu za kutunyonya. Inakera sana. wizi wizi tu.
Serikali zote duniani ni mifumo ya wizi.
Na wananchi wakisinzia ndo wizi unaongezeka mara dufu.
 
Unakuta taasisi iko chini ya wizara ya biashara au viwanda na uwekezaji. Sasa wizara kama wizara ilitaka ifanye majukumu gani
Wizara inaundwa na kupitia hizi Taasisi.

UTI wa mgongo wa wizara ni hizi Taasisi, zisipokuwepo hakuna wizara.

Kazi kubwa ya wizara ni kuzisimamia hizi Taasisi.
 
Back
Top Bottom