Serikali punguzeni utitiri huu wa Taasisi ni mzigo kwa walipa kodi

Serikali punguzeni utitiri huu wa Taasisi ni mzigo kwa walipa kodi

Kwa hiyo hayo majukumu hayawezi fanywa chini ya Taasisi moja ambayo ina vitengo tofauti? Kuna ulazima gani wa kuwa na ofisi kwa kila Taasisi?

Ndio maana tunasema ni majukumu yanayofanana na yako kwenye wizara moja.
Lengo kuu ni kuleta ufanisi. Ukisema viwe ni vitengo ndani ya wizara mambo yataenda slow sana.

Muhimu ni kuzipa Uhuru wa kufanya kazi kwa kujitegemea ili ufanisi upatikane kutokana na umuhimu wa vitengo vyenyewe.

Kumbuka ishu za uwekezaji na uanzishwaji wa makampuni ni kitu muhimu kwa ukuaji wa uchumi. Hivyo longo longo hazitakiwi .
 
Hakuna sababu ya kuwa na lundo la Taasisi za upigaji ilhali zinafanya Kazi zinazofanana..
Tatizo huna ufahamu sahihi wa ufanyaji kazi wa hizo Taasisi, Lengo la kuanzishwa kwake na faida ya iwepo wake.

Usipende kukalili wingi sio hoja, iruhusu akili ifahamu taratibu za ufanyaji kazi wa hizo Taasisi na uelewe madhumuni ya kuanzishwa kwake.

Hoja kwamba imeanzishwa kwaajili ya upigaji haimake sense. Shida kubwa ya sisi wabongo hatupendi kufata taratibu tunapotaka kufanikisha vitu vyetu.
 
Weeeee hhh waguse hukohuko, huku kwetu watuache tujenge nchi.
Hizi bodi ndio zifutwe
Bodi ya maziwa
Bodi ya nyama
Bodi ya korosho
Bodi ya pamba
Bodi ya kahawa
Bodi ya filamu
Bodi ya bahati nasibu
Bodi ya misitu n.k
Ukiona zao lolote Tanzania limeundiwa bodi basi lazima hilo zao baada ya muda life au lidorore au lilete shida kwa wakulima maana Serikali inakuwa na tamaa kubwa ya kutaka kuwanyonya wakulima kupitia hiyo bodi.

Mazao yote yenye bodi ni yale Serikali inaona ni rahisi kuuzika nje na hivyo ili ijipatie hela bila jasho inayaundia bodi

Jiulize kwa nini serikali haiundi bodi ya Mahindi au bodi ya Mtama?
 
Ebu njoo na mfumo wako watu waujadili...
Ila mimi ni muumini wa ugatuzi...
Tatizo kubwa lilopo taasisi/idara nyingi za serikali zinafanya competition badala ya coorpetition.
Na sekta binafsi ndo zinaogopwa hazipewi ushirikiano kabisa!
Tuanzie hapo... Ila wingi wa taasisi/idara si hoja kubwa!
Mfano:

Kwanini Kuna TBS, OSHA, TMDA na wakati huo huo Mambo yote haya Kuna Watumishi ndani ya Halmashauri wanaofanya kazi hizo hizo ??
 
Nawasalimu kwa jina la JMT..na Kazi iendelee..

Ifike wakati serikali ichukue maamuzi magumu na yenye tija kwa Taifa kwa kupunguza utitiri wa Taasisi zake zilizo chini ya Wizara mbalimbali..

Ukiacha kwamba hazina tija kwa Nchi bali ni mzigo mkubwa sana wa walipakodi wa Tanzania kwani zinaongeza gharama za utawala zisizo na msingi na kuleta urasimu,gharama na usumbufu kwa wananchi.

Serikali chukueni hatua ya kuziunganisha na kufuta zile zisizo na tija.

Just imagine Wizara moja ya Viwanda na Uwekezaji ina Taasisi zaidi ya16 zilizo chini yake.Sasa piga hesabu kuna zaidi ya Wizara ngapi hapa Tanzania.

Hamuoni kuwa na lundo la Taasisi kunaongeza urasimu,usumbufu na gharama zisizo za msingi kwa wawekezaji na wananchi?

Kwa kuwa mh.Rais wewe ni Msikivu na Ili kuleta ufanisi ,basi shughulikia na hili maana imekuwa ni kichaka cha upigaji wakati ufanisi ni zero👇

View attachment 2230589
Wizara feki hiyo ndiyo maana viwanda haviwezi kuendelea Tanzania kwa sababu kunguni ni wengi.
 
Mfano:

Kwanini Kuna TBS, OSHA, TMDA na wakati huo huo Mambo yote haya Kuna Watumishi ndani ya Halmashauri wanaofanya kazi hizo hizo ??
Hizo taasisi zina competition sana utafikiri ni za serikali za nchi tofauti.
Ingefaa ukikidhi vigezo vya taasisi moja ieleweke umekidhi vigezo vya taasisi nyingine zinazoshabihiana majukumu!
Tatizo linaanzia hapo.
Alafu wao wapo kuzibana taasisi na watu binafsi. Za serikali zinazofanya biashara wala hazibanwi kiivyo!
Tulijadili kwa hivi... labda wataelewa na kuziunganisha... nasema labda!
 
Ukiona zao lolote Tanzania limeundiwa bodi basi lazima hilo zao baada ya muda life au lidorore au lilete shida kwa wakulima maana Serikali inakuwa na tamaa kubwa ya kutaka kuwanyonya wakulima kupitia hiyo bodi.

Mazao yote yenye bodi ni yale Serikali inaona ni rahisi kuuzika nje na hivyo ili ijipatie hela bila jasho inayaundia bodi

Jiulize kwa nini serikali haiundi bodi ya Mahindi au bodi ya Mtama?
Serikali ni mfumo wa kuwanyonya wananchi.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiona zao lolote Tanzania limeundiwa bodi basi lazima hilo zao baada ya muda life au lidorore au lilete shida kwa wakulima maana Serikali inakuwa na tamaa kubwa ya kutaka kuwanyonya wakulima kupitia hiyo bodi.

Mazao yote yenye bodi ni yale Serikali inaona ni rahisi kuuzika nje na hivyo ili ijipatie hela bila jasho inayaundia bodi

Jiulize kwa nini serikali haiundi bodi ya Mahindi au bodi ya Mtama?
Na bodi ya ngisi na pweza mbona haipo?
 
Unaijua National Land Use Planning Commission(NLUPC)??

Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi
Umewahi kuiona ikipanga miji au matumizi Bora ya Ardhi popote?

Kwa nini kuna migogoro ya mipaka na mizozo ya wakulima na wafugaji?

Kwa nini miji yetu imejaa uswazi kiasi kwba hadi zoezi la anuani za makazi linakuwa kama kichekesho?
 
Na bodi ya ngisi na pweza mbona haipo?
Serikali haijaona upenyo wa tozo. Ikiona tu upenyo itaweka bodi au itaanzisha kitu wanaita stakabadhi ghalani. Hauwezi uza mazao yako bila kibali cha hao jamaa wa mamlaka ya maghala na stakabadhi ghalani Shida tupu
 
Back
Top Bottom