Serikali punguzeni utitiri huu wa Taasisi ni mzigo kwa walipa kodi

Mm naomba waanzishe bodi hiz maana usumbufu tunaopata mtaan n shida

Bodi ya paka

Bodi ya kunguru

Bodi ya mbwa

Bodi ya panyaroad

Nimeandika haya sababu kila kilichotajwa hapo juu kinausumbufu wake

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
NDC inafaida Gani?
 
Umewahi kuiona ikipanga miji au matumizi Bora ya Ardhi popote?

Kwa nini kuna migogoro ya mipaka na mizozo ya wakulima na wafugaji?

Kwa nini miji yetu imejaa uswazi kiasi kwba hadi zoezi la anuani za makazi linakuwa kama kichekesho?
1.Ndio

2&3.Mizozo na uswazi ngoja waje wataalamu/wahusika
 
The National Development Corporation ilianzishwa na serikali kwa ajili ya kuchochea,kuendeleza na kukuza maendeleo ya kiuchumi ya Taifa kwa sectors zote.
Je huwa unaliona likichochea? Kuna baadhi ya taasisi ni mzigo Kwa serikali
 
Ugatuzi ni serikali za majimbo au wananchi wawachague viongozi wao wengi.
Karibu wakuu wa hayo mashirika yote na hizo bodi wanateuliwa na mtu mmoja amabaye ndiye anateua pia msururu wa viongozi watakaozisimamia.
 
TAN TRADE inatakiwa ivunjwe, ku promote biashara wanaweza kufanya wizara wizara au wakatoa tenda itakapohitajika kufanya hivyo. Maonyesho ya biashara ya 77 ni kituko kikubwa, watu wanauza viberiti, vitana, cover za simu, sufuria, bidhaa za mchina za kila aina. Maonyesho ya biashara yanatakiwa yawe kwa ajili bidhaa mpya hasa za za teknolojia zinazoingia sokoni na zinazozalishwa na kampuni za ndani ya nchi.

Hata BRELA nayo inatakiwa ivunjwe, biashara zisajiliwe Halmashauri, serikali kuu ikachukue taarifa huko na TRA kama inazitaka.
 
Mfumo wa Ujamaa unaongeza sana urasimu. Ndiyo maana unaona utitiri wa taasisi. Watumishi wa serikali wanazidi kuongezeka wakati nafasi za kazi kwenye sekta binafsi zinazidi kuadimika. Ndiyo maana mfumo wa Ujamaa unaharibu uchumi.
 
Katika Africa mashariki Tanzania ni mojawapo ya nchi ambazo kufungua biashara inachukua muda mrefu zaidi ukilinganisha majirani zake.
 
Naomba kujua kazi za NDC
 
Mimi nataka kujua Je, kazi zinazofanywa na TBS, TMDA, OSHA haziwezi kufanywa na Halmashauri?
 
Waanze kuunganisha TIC na NEEC. Pia kuna kitu kinaitwa TNBC sijui kiko chini ya Wizara ipi. Yaani utendaji ni ovlvetrlaps tu
 
Mimi nataka kujua Je, kazi zinazofanywa na TBS, TMDA, OSHA haziwezi kufanywa na Halmashauri?
TBS na TMDA hizo ni prime huwezi kuunganisha au kufuta. Ni international requirement and standards. Hizo nyingine ni Ulaji ti. Kama SIDO hivi inafanya nini? Ifutwe kabisa maana lengo la kuanzisha kwake halikutlfikiwa toka 1973. Yaani miaka 49 ya😰SIDO imeishia kuwa taasisi ya mafunzo ya ujasiriamali na mikopo. Zile karakana zilizojengwa kanda mbalimbali ni nyumba za panya na wamekodisha. Ukienda Ile ya Lindi utaumia Sana.
 
Wizara inaundwa na kupitia hizi Taasisi.

UTI wa mgongo wa wizara ni hizi Taasisi, zisipokuwepo hakuna wizara.

Kazi kubwa ya wizara ni kuzisimamia hizi Taasisi.
Tatizo kuna overlaps za majukumu mpaka wanavimbiana au kununiana. Hivyo zinazoingiliana ziunganishwe kama TIC na NEEC na TNBC then unakuwa na Moja inayobeba idara key. Hapo pia uta serve mambo mengi mno. Ningepewa hiyo miundo Yao ningeifumua Sana.
 
Hoja ya
Ke
Sumatra,latra!Tanapa,ngorongoro cons,
Bodi za mazao,benki za kilimo(Kuna moja ilikaa mwaka mzima bila kutoa mkopo,lskini watu wanavuta salary).
TBS,WMA(wanahakiki ujazo wa matenk).
Inabidi kuwe na taasisi kama TRA hii Haina mbadala,lakini mengine ni kutengeneza duplicity tu,hakuna tija,
Wizara ya kazi ajira,wizara ya Sanaa,wizara ya maji,wizara ya kilimo mifugo.
Kuna Sido na tildo.kwa ufupi taasisi nyingi zipo kisiasa tu,hazina tija.mambo mengine ingebidi yawe idara tu,
Kulikuwa hakuna haja ya kumega Tanlosds kujenga tarura,
 
Bora hata hizi maana Wizara husika imeshindwa hata kuthibiti kunguru sasa panyaroad watawezekanika? Maajabu ya Karne.
 
Bodi ya Mazao mchanganyiko na upuuzi mwingine kama huo.
... halafu nchi inaagiza ngano, sukari, na mafuta ya kula billions of money! Kuna bodi ya sukari by the way. Kazi yao kutoa vibali vya kuagiza sukari.

Wizara za Kilimo na Afya nadhani ndio zinaongoza kwa kuwa na taasisi nyingi zisizo na tija.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…