Serikali ruhusuni vifaranga toka Kenya

kluger

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2016
Posts
2,093
Reaction score
1,899
Salaamu,

Toka awamu hii iingie madarakani wamezuia Vifaranga/ LAYERS toka Kenya.

Sababu kubwa wakisema kuzuia magonjwa ya Ndege, lakini ukweli ni kwamba huko Kenya [emoji1139] hakuna sehemu imeripotiwa na mashirika ya kimataifa kuhusu mlipuko wowote wa magonjwa ya Ndege.

Hivi sasa wafugaji tunapata taabu sana kupata Vifaranga/LAYERS hasa wa Kuku wa mayai.
Kampuni zilizopo nchini za uzalishaji wa Vifaranga/LAYERS hawa hawana uwezo wa kulisha soko. Hivi sasa ukiweka order ya Vifaranga/LAYERS kwa kampuni za ndani inachukua hadi miezi miwili kupata Vifaranga/LAYERS.

Hali hiyo imesababisha kero nyingi, ikiwa ni ulanguzi wa Bei, rushwa, uzalishaji mdogo wa mayai, kudumaa kwa Biashara hii na mateso kwa wajasiriamali wadogo hasa wakina mama wa nyumbani ambao wengi wamejiajiri katika eneo hili.

Sasa tunajiuliza hivi hiyo serikali ya wanyonge ni ipi? Watu tunataabika na mambo madogo kama haya, viongozi wapo hawana kauli wala jinsi ya kutatua matatizo ya wananchi.

Mnataka viwanda, mazingira ya kuanzisha viwanda kama hivi si rafiki, kodi kubwa, urasimu mwingi. Lakini pia ili usitese wananchi wako, kwa nini usianzishe kwanza viwanda ndiyo uje utoe matamko yako ya kuzuia vya nje???

Mwaka jana Bei za vyakula vya mifugo vilikuwa juu kiasi kwamba wafugaji wengi walijitoa katika eneo hili kisa ni kodi kubwa za malighafi. Sasa nyinyi viongozi wa nchi hii mlisoma wapi?? Mbona hatupigi hatua?? Yaani likiisha hili mnakuja na lingine. Kwa nini mna wasumbua walipa kodi hawa wadogo??

Tanzania ni nchi ya ajabu Sana.

Sijui hili nalo mpka mheshimiwa Rais atolee tamko??

Inasikitisha Sana!!!

NB: NAZUNGUMZIA VIFARANGA VYA LAYERS/KUKU WA MAYAI YA KIZUNGU/KISASA
 
Hii ni mada ya ajabu kuwahi kutokea tangu dunia imeundwa. Tanzania hakuna vyuo vya kilimo? hakuna wataalamu wa kilimo kuweza kutengeneza breed za kuku mpaka muagize Kenya? kwani wao wanapatia wapi? Huo ndio mwisho wenu wa kufikiri? Badala ya kusema tuboreshe taasisi zetu za tafiti na uzalishaji wa mifugo na kilimo unataka short cut ya kuagiza kutoka hapo KENYA ambao ni wakulima kama wewe wanazalisha na kusambaza???
 

Eti tangu Dunia imeundwa!, unawasemea hadi Babu zako as if uliishi toka enzi, kuwa na akiba zuzu wewe.
Kama wapo miaka yote hujiulizi nini kimeshindikana? Fikiria nje ya boksi, huoni kwamba nchi imeshindwa ingali wataalamu wapo. Pili wewe si mfugaji huna unalolijua kuhusu hili jambo, ungepita tu
 
acha bangi dogo!!!!
 
Mkuu upo mkoa gani?
Naweza kukuulizia sehemu huenda ukapata vifaranga bila shida.

Saa nyingine ni mawasiliano mabovu lakini sio kwamba Tanzania nzima kuna upungufu wa vifaranga.
 
====Ungesoma vizuri post ya mtoa mada usingekurupuka kiasi hiki,amesema haya mambo yangekuja kwa hatua na sio tulivyoanza,tatizo lako hufugi unashadadia ya wafugaji......
 
====Ungesoma vizuri post ya mtoa mada usingekurupuka kiasi hiki,amesema haya mambo yangekuja kwa hatua na sio tulivyoanza,tatizo lako hufugi unashadadia ya wafugaji......
Sasa ninyi ni wafugaji gani hata vifafaranga mnashindwa kuzalisha mnategemea akili za wakikuyu na waluo? hiyo aibu wala msingeiweka hapa
 
Mkuu unauza vifaranga?
 
Kuna ndugu yangu kanipigia simu juzi kuwa kutokana na uhaba wa vifaranga alinunua hawa wa hovyo! Kati ya vifaranga 700, mia tano wamefariki, mtaji umekata. Kweli nilisikitika.
 
KENYA WAJE KUFUNGUA KIWANDA TZ WALIPE KODI,ILA KUNA MAKAMPUNI KM INTERCHICK WANATOA VIFARANGA KWA BEI YA KIWANDANI
BEI INATEGEMEA NA UPATIKANAJI WA MAHINDI NA MALIGHAFI NYINGINE
 
Sisitizeni serikali iwekeze research za uzalishaji kuku, kusema serikali iruhusu kuku kutoka kenya ni kutukosea adabu watanzania.
Wakati Trump anaingia Ikulu Marekani Ford walikua na mpango kukuza kiwanda chao cha Magari Mexico kwasababu kuna unafuu wa kodi, gharama za uzalishaji ni ndogo na ukaribu wa Mexico na Marekani hivyo bidhaa zitaingia Marekani kwa uraisi. Trump akasema wakijenga kiwanda kikubwa Mexico manake ajira nyingi zitaenda huko na Marekani itakua mlaji tu. Akasema Ford itapigwa kodi nyingi sana kama itataka kukuza kutoka Mexico. Ford wakabadili msimamo na wameanza kufikiria kujenga Marekani.
Ishaurini serikali iwekeze kwenye uzalishaji wa kuku na pia muwaambie wanaowauzia kutoka kenya waje kuwekeza Tanzania.
 
wewe ndio umeongea point. Wakati chuo kikuu SUA kinatoa wahitimu wa kozi mbalimbali kila mwaka, tunapiga hesabu na kupiga kelele hapa kwamba tuagize kenya? wao kenya wanaagiza kutoka wapi? nani ametuloga watanzania?
 
wewe ndio umeongea point. Wakati chuo kikuu SUA kinatoa wahitimu wa kozi mbalimbali kila mwaka, tunapiga hesabu na kupiga kelele hapa kwamba tuagize kenya? wao kenya wanaagiza kutoka wapi? nani ametuloga watanzania?
Mambo mengi sana tunafeli Tanzania, sisi hata bati za kiwango cha juu kabisa tunaweza kuzalisha kwasababu materials zipo na watu wa mechanical na industrial engineering wana graduate kila mwaka. Lakini kuna nyuzi za ujenzi humu watu wanakuambia bila msauzi hujapaua, sasa msauzi anafanya nini kwenye soko la mtz? na mtz anafanya nini na soko lake binafsi?
 
Mkuu hatupo kwenye closed economy kila kitu uzalishe wewe hutaweza maana itabidi upunguze sehemu ili ucover ulipoongeza ndiyo maana ikitokea shortage ya sukari huoni SUA wakiambiwa watengeneze breed ya miwa ili ivunwe kwa siku ila wanaruhusu importation ili kukabiliana na upungufu ambao unaweza kupelekea upandaji wa bei

SUA mpk waje wamalize utafiti huo ni leo wakati mlaji hali yake inazidi kuwa mbaya alichoshauri mleta uzi ni sawa kabisa kipindi hiki waruhusu wakati hicho ulichosema kikifanyiwa kazi
 
Ninyi endeleeni kufagilia vitu mnavyozalishiwa na wenzenu kuna siku mtaletewa G.M.O wao wanahasara gani si wanatafuta fedha na soko ni ninyi?
 

Unajua watu wengi kama wewe mnapenda kuonekana mnatetea utaifa, sijui hamtaki aibu hii, lakini mnashindwa kujua kitu kimoja. Huo mfano wako wa Ford ni tofauti kidogo. Wamarekani wanajitambua sana si kama watanzania. Kampuni ya Ford walikuwa wabinafsi wakitaka kujipatia faida lukuki ilingali mazingira ya uwekezaji marekani yalikuwa mazuri na fair.

Hivi nikuulize toka tumepata uhuru hii serikali yetu pamoja na wataalamu walionao hawajaona umuhimu wa kufanya research ya jambo hili? Hapana. Research zipo nyingi tu, maeneo ya kuwekeza yapo mengi tu.
Na hvi ni kampuni ngapi za wakenya zipo hapa nchini? Ni nyingi tu na wanajua sana kutumia fursa zetu kutokana na tabia za wabunge wetu kutunga sheria kandamizi dhidi ya mazingira ya uwekezaji wa ndani.

Sasa kwa ufupi tu tambua watu hawaji kuwekeza viwanda hivi hapa Tanzania kutokana na mazingira mabovu ya uwekezaji, gharama za uendeshaji zipo juu sana Tanzania kulinganisha na kenya hivyo viwanda hivi hapa Tanzania havilipi ndiyo Maana unaona ukuwaji wa viwanda hivi ni mdogo. Sasa jambo hili lilitaka viongozi wanaojali na kutatua matatizo ya wananchi wa hali ya chini.

Kama mazingira hayo viongozi hawataki kuyaandaa yawe ya kuvutia kama wenzetu wakenya nani atakimbilia kuja kuwekeza Tanzania? Atafungua kiwanda Kenya then Tanzania itaendelea kuwa soko.

Chakufanya:

Siyo tu kuja hapa na kutetea ooh ni aibu kutuhusu wakenya kutuuzia bidhaa. Sisi ni wateja wakubwa wabidhaa nyingi tu za Kenya hilo mlijue na sababu kubwa ni SIASA SIASA za viongozi wetu dhidi ya mazingira ya uwekezaji.

Kabla hujaja kutetea na kuleta ushabiki wa Tanzania, fikiria kuhusu userious wa nchi yako katika uwekezaji hapa nchini.
Umeme hauleweki, urasimu chungu mzima, wafanyakazi wavivu wakitaka malipo makubwa etc nani atakuja kuwekeza hapa??
Kama serikali imeshindwa kuboresha mazingira ya uwekezaji wa kuzalisha Vifaranga/LAYERS nchini wasizuie wengine kuleta nchini. Tusipo badilika watanzania tutaendelea kuwa soko la bidhaa za Kenya kila siku.
Maamuzi mengi ya viongozi ni kama hayana macho. Mfano wakulima hawasaidiwi na serikali kwa aina yoyote katika uzalishaji wao, lakini cha ajabu serikali inawakata kuuza mahindi nje ya nchi, huku wakiwaruhusu wakulima wa nje kuleta mahindi hapa nchini. Matokeo yake nchi imefurika mahindi na wakulima hawanufaiki na bidhaa za mahindi. Sasa unaweza ona aina ya viongozi ulionao.

Wewe Okaoni soma hapa uache kujipendekeza mada za watu kwa ushabiki maandazi kisa wewe unajiona mzalendo/ ushabiki wa kipuuzi
 

Lipo la kijifunza
Kwamiaka mingi hii nchi hainaga sera endelevu...naamini sera ya KILIMO kwanza ingeendelezwa ingekuwa imeshaibua hili jambo....kiukweli viwanda vya kuzalisha vifaranga vilivyopo Tanzania haviwezi kulimudu soko hata kidogo.....Serekali kwa miaka mingi haitoagi pesa kwa vyuo vya mifugo kwa ajili ya utafiti...Chuo kikuu cha Sokoine ni kama wamelala tena usingizi wa pono...wao walitakiwa waisaidie serekali kutokana na uwezo wao wa kuandika project na kupata donor funds.....badala yake walituanzishia SUA TV....na wenye akili wakaona ni sawa tu......wenzao Kenya chuo kikuu cha Egerton wameenda mbali na kuzalisha maziwa y kwa technologia rahisi ..........KARI Naivasha...... wamefanyia utafiti kuku wao wa kienyeji wakatoa kuku wanaomuita Kari Kienyeji....ambao ni mchanganyiko wa mbegu mbalimbali za kuku wa kieneyji wanaopatikana kenya...kuku wa kari wanaozwa mpaka Tanzania...sisi hatutaki kuambiwa ukweli......kila kitu siasa.....vyuo vyetu vyakilimo vingi vipo hoi...hawana pesa za kufanya utafiti......soko la kuku kila uchwao linazidi kuwa kubwa kutokana na kuongezeka kwa watu kila siku....

Serekali inatakiwa iamke sasa......iwekeze kwenye utafiti....ivisaidie hivi viwanda vya mifugo kuanzia vya nyama mashamba yanayozalisha vifaranga......viwanda vya vyakula vya mifugo nk
 
Umeandika pumba sana Mkuu, nikipata nafas ya kutype ntaandika upumbavu wako.
 

Safi sana, nimekupata vizuri sana.

Cha ajabu mkuu wa nchi kapeleka hela ili hicho chuo kijengewe majengo na kila kukicha anateua maprofesor ambao hata shamba wala kuku hana, anaishi posta mpya huku ni mtaalamu wa kilimo na mifugo.

Then anawaagiza wakurugenzi wa taasisi zisizotoa gawio wajiuzulu, huku akipeleka hela kwingine!

Naanza kuelewa kauli ya TRUMP!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…