kluger
JF-Expert Member
- Jun 16, 2016
- 2,093
- 1,899
Salaamu,
Toka awamu hii iingie madarakani wamezuia Vifaranga/ LAYERS toka Kenya.
Sababu kubwa wakisema kuzuia magonjwa ya Ndege, lakini ukweli ni kwamba huko Kenya [emoji1139] hakuna sehemu imeripotiwa na mashirika ya kimataifa kuhusu mlipuko wowote wa magonjwa ya Ndege.
Hivi sasa wafugaji tunapata taabu sana kupata Vifaranga/LAYERS hasa wa Kuku wa mayai.
Kampuni zilizopo nchini za uzalishaji wa Vifaranga/LAYERS hawa hawana uwezo wa kulisha soko. Hivi sasa ukiweka order ya Vifaranga/LAYERS kwa kampuni za ndani inachukua hadi miezi miwili kupata Vifaranga/LAYERS.
Hali hiyo imesababisha kero nyingi, ikiwa ni ulanguzi wa Bei, rushwa, uzalishaji mdogo wa mayai, kudumaa kwa Biashara hii na mateso kwa wajasiriamali wadogo hasa wakina mama wa nyumbani ambao wengi wamejiajiri katika eneo hili.
Sasa tunajiuliza hivi hiyo serikali ya wanyonge ni ipi? Watu tunataabika na mambo madogo kama haya, viongozi wapo hawana kauli wala jinsi ya kutatua matatizo ya wananchi.
Mnataka viwanda, mazingira ya kuanzisha viwanda kama hivi si rafiki, kodi kubwa, urasimu mwingi. Lakini pia ili usitese wananchi wako, kwa nini usianzishe kwanza viwanda ndiyo uje utoe matamko yako ya kuzuia vya nje???
Mwaka jana Bei za vyakula vya mifugo vilikuwa juu kiasi kwamba wafugaji wengi walijitoa katika eneo hili kisa ni kodi kubwa za malighafi. Sasa nyinyi viongozi wa nchi hii mlisoma wapi?? Mbona hatupigi hatua?? Yaani likiisha hili mnakuja na lingine. Kwa nini mna wasumbua walipa kodi hawa wadogo??
Tanzania ni nchi ya ajabu Sana.
Sijui hili nalo mpka mheshimiwa Rais atolee tamko??
Inasikitisha Sana!!!
NB: NAZUNGUMZIA VIFARANGA VYA LAYERS/KUKU WA MAYAI YA KIZUNGU/KISASA