Nisahihishwe, lakini nimejaribu kuisoma Budget ya serikali lakini sijaona mahali ambapo mabilioni yamepitishwa kuhamisha Wamaasai toka Ngorongoro kwenda Msomero Handeni wao na mifugo yao, kujengewa nyumba, ujenzi wa shule na zahanati kijijini hapo na miundo mbinu mingine.
Wasiwasi wangu isijekuwa tunapokea pesa toka nje kwa siri kugharamia operesheni hii kwa agenda za siri.
Ni wakati sasa kufahamu yaliyo sirini kwenye hii operesheni.
Unaposikia rais wa nchi anawatangazia wananchi wake kwamba yeye ni 'Chura Kiziwi', na kwamba hataki kusikia makelele toka kwao tena usifikiri kuwa mambo yamesimama, hayafanyiki..
Sasa yanafanyika gizani, na wananchi hawatakiwi kujuwa chochote!
Wale wahindi wa Adani walipo pewa bandari, kuungana na DP World uliwahi kusikia popote habari za mchakato wa kuwaweka hapo?
Mama 'Chura Kiziwi' hataki tena kelele.
Sijui sasa ni mambo mangapi yaliyo fanyika huko gizani. Hata hao wabunge wa bandia na wao ni giza tupu, hakuna wanalo lijua.
Hii ni nchi ya watu walio huru kuamua mambo yao, au ni zizi la mtu analo wafugia watu hawa?
Hilo Baraza la Mawaziri lenyewe limekuwa lkama wacheza mpira wa kukodiwa. Kila anapojisikia kubadili wachezaji anabadili. Wote hawana la kusema. Huko kwenye vikao vya baraza hilo sasa si kujadili tena, ni kuambiwa tu na kupitisha. Akina Kabuti na mwenzie Lukubi waliwekwa benchi kuwatia adabu. Sasa wamenyooka kama rula. Huo ni mtindo anao utumia Bi 'Chura Kiziwi' kuwaweka watu wake kwenye mstari.
Kama waTanzania hawayaoni haya na kuwa na hofu kubwa na huyu mwanamke na kumruhusu aendelee kwenye nafasi hiyo kwa miaka mitano; tena ya kisingizio kapewa kura yeye mwenyewe, hata kama ni kura za kuiba, naamini hatufiki huko kwa miaka mitano salama, na kama kimuujiza tukifika nchi itakuwa imeharibiwa vibaya sana hii. Waarabu watakuwa wanawatia vidole watu mahala pasipofaa. Hizi pesa walizo nazo zitanunua utu wa kila mmoja wetu; hasa hao walioko huko CCM.