Augustine Moshi
JF-Expert Member
- Apr 22, 2006
- 2,556
- 1,385
Sio Lazima Kuisubiri Serikali Kwa Kila Kitu.
Masikini Watanzania wengi bado wanadhani serikali ni baba mama au mjomba. Ukifuatilia taarifa za habari zilizoko redioni, magazetini na kwenye runinga utashangaa jinsi watu wanavyoisubiri serikali iwafanyie vitu ambavyo wao wenyewe wangepashwa kuvifanya.
Nimeona wazazi wakizungumza kuhusu shule ya kijiji chao kukosa matundu ya kutosha ya vyoo. Wakatoa kilio serikali iwachimbie mashimo zaidi. Vijana na wababa wenye nguvu za kutosha wanaacha watoto wao na waalimu wao watumie matundu mawili tu ya vyoo kwa miaka wakisubiri serikali ije iwaongezee mengine!
Jana nimeona kwenye runinga wakulima waliobarikiwa kuvuna mihogo mingi kipindi hiki wanaitaka serikali iwatafutie mnunuzi! Jukumu la serikali ni kuweka mazingira mazuri ya mwenye cha kuuza apate mnunuzi na sio kwamba serikali yenyewe ndiyo itatafuta kila mnunuzi wa parachichi, mihogo, ndizi na machungwa. Serikali inatakiwa kuacha kukuzuia kuuza machungwa unapopata soko na siyo kukuletea nyumbani mnunuzi wa machungwa yako.
Vijana waliosoma wana uwezo wa kutumia mitandao (hasa Google) kutafuta soko kwa karibu kila kitu. Kinachopashwa kufanywa na serikali ni kuacha kabisa tabia ya urasimu mrefu unaozuia mchakarikaji kusafirisha mazao nje kwa muda mfupi. Serikali iweke mazingira rafiki ya kuwezesha international transactions at the person to person or person to company or company to company level. Ni pamoja na kutoa mafunzo kwa vijana kuhusu namna ya kufanya haya mambo.
Kwa mfano, wakulima wa vitunguu wakivuna kuwe na vijana wenye mikopo tayari wanaoweza kununua kutoka kwa wakulima na kuuza Comoro, India na masoko ya nchi zingine za jirani na hata za mbali.
Kifupi ni kwamba tuache huu ugonjwa wa kuililia serikali itufanyie vitu ambavyo sisi tunaviweza. Serikali ijikite kwenye kujenga miundombinu, elimu, afya na kuweka mazingira rahisishi ya biashara za ndani na nje. Yaliyobaki ni juu yetu. Tutambue serikali siyo baba mama au mjomba.
You and not the government, are responsible for the wellbeing of your family. Ukisubiri serikali utasubiri sana.