Serikali tafakarini kuongeza mishahara ya Watumishi wa Umma, ukali wa maisha ni bomu linaloua taratibu!

Serikali tafakarini kuongeza mishahara ya Watumishi wa Umma, ukali wa maisha ni bomu linaloua taratibu!

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2015
Posts
6,236
Reaction score
15,677
Kwenye uchumi ambao bei za bidhaa zinapanda kila uchwao, ili mtu uendelee ku survive na maisha, ni budi kipato kipande ili kupunguza ukali wa maisha. Hii kwa wachumi tunaiita 'Cost of living adjustment - COLA'.

Ndo maana utaona salary review zinapaswa kufanyika kila mwaka, na endapo kama haitafanyika lazima kutolewe sababu ni kwanini mwaka husika hakuna salary review na increment. Kipindi cha nyuma salary review ilikuwa inafanyika kote kote Sekta Binafsi na Sekta ya Umma na wafanyakazi kote kote, waliweza kufidiwa na ukali wa maisha kwa kuongezewa mishahara. Ilikuwa ni jambo zuri mno kwa mfanyakazi, maana nao ni binadamu ambao wana mahitaji pia yanayokuwa mwaka hadi mwaka.

Lakini kuanzia mwaka 2015, kumekuwa na kilio kikubwa kwa wafanyakazi wa umma kulikotokana na kutoongezewa mishahara mfululizo kwa miaka 5.

Nimefanya utafiti wangu wa haraka haraka, kwa kuangalia movement ya kupanda kwa bei za bidhaa kwenye matumizi makuu ya mfanyakazi tangu mwaka 2015 mpaka october 2020, na nimegundua kwamba kipato cha mfanyakazi kimenyongwa karibu kwa asilimia 19%. Ikiwa na maana ili mfanyakazi wa sasa as of October 2020, aishi maisha aliyokuwa anaishi mwaka 2015, ilipaswa kipato chake kiwe kimeshaongezeka kwa asilimia 19% au zaidi.


Lakini kwa sababu serikali haijaongeza mshahara kwa kipindi chote hicho, ni sahihi kusema huyu mfanyakazi kipato chake kimenyongwa kwa asilimia 19% ya kipato chake cha 2015, au pato lake limeshuka in real terms kwa asilimia 19% !!!!!!!!!

Huu hapa chini ni mfano wa mtu aliyekuwa analipwa mshahara wa sh 700,000


% Change in general prices (December 2015 to October 2020)Wheights in %
Food and Non Alcoholic Beverages
23.37%
38
Clothing and Footwear
14.63%
8
Housing, Water, Electricity, Gas and Other Fuel
50.65%
12
Transport
7.41%
13
Others (Average % change)
8.18%
29
100
Allocaion of income of Tzs 700,000 per month in 2015 as per wheightsNeeds allocation in 2015Amount required for a person to sustain same basket they consumed in 2015
Food and Non Alcoholic Beverages266,000.00328,164.20
Clothing and Footwear56,000.0064,192.80
Housing, Water, Electricity, Gas and Other Fuel84,000.00126,546.00
Transport91,000.0097,743.10
Other consumption needs203,000.00219,605.40
Total income700,000.00836,251.50
Income increase that was required for person to live as they use to be in 2015136,251.50
Depreciation of income (2015 to 2020)
19.46%

Ombi langu kwa serikali, kwa haraka na kwa hali ya dharura waangalie namna ya kuokoa jahazi la ubora wa maisha ya mfanyakazi wa umma, hili no bomu na linawaua taratibu.

Wengi sana wame stretch maisha yao na hii imeathiri pakubwa sana quality of life ya hawa ndugu zetu... Humu JF kuna mifano mingi sana wengi wanaleta nyuzi za majuto kila uchwao..

Hali inatisha sana, halafu mbaya zaidi sijahesabia impact ya deni la HESLB kwenye mahesabu yangu, ambayo ndo inafanya hali ya huyu mfanyakazi kuwa worse kuliko hata nilivoandika hapo.

Serikali mtafakari hili, hili bomu likilipuka, msitegemee productivity yoyote kwa hawa wafanyakazi, ni kama wapo wapo tu bora liende, na hii sio nzuri kwenye uchumi.. Ni janga!!!!

Na . N.Mushi
Mtetezi wa wanyonge
 
Hii awamu ni historia! Watumishi wataikumbuka kwa mateso na adha waliopata.

Hakuna cha flai ova wala treni umeme zitakazo kumbukwa,zaidi ya umaskini wa kupindukia,kuporomoka kwa uwekezaji na mitaji.
 
Hii awamu ni historia!
Watumishi wataikumbuka kwa mateso na adha waliopata.
Hakuna cha flai ova wala treni umeme zitakazo kumbukwa,zaidi ya umaskini wa kupindukia,kuporomoka kwa uwekezaji na mitaji.
Inauma sana aisee.. japo mimi sio muhusika
 
Ngojeni kwanza tuongeze barabara na madaraja, utumishi wa umma ni kazi za kujitolea. Lazima muwe wazalendo, hakuna mtu anayeridhika na mshahara.

Nasema uongo ndugu zangu?

Akimaliza hii mitano lazima tumlazimishe aongeze hata 10
 
Ina maana watumishi wa umma wao ndo wanashida au wanauhitaji mkubwa zaidi ya watu wengine wote?

Miradi inahitaji pesa ikamilike, vijana wanahitaji ajira, watumishi tiyari wanaajira na mishahara, ila bado wanataka waongezewe dau/mshahara.

Je, ni lipi jema la kuanza nalo? na nilipi ni tamaa na kutoridhika? Ni haki na halali kabisa Mh Magu aanze kuwashughulikia watumishi wote wasio tosheka na kuridhika na wakipatacho, maana hao ndo wezi na mafisadi watarajiwa kwa tamaa za mshahara mkubwa.

Watumishi jiongezeni pesa mnazolipwa ni nyingi mno, wacheni kunywa pombe, sim za laki saba, kusugua kucha, kula chips kuku, kuvaa nguo za bei mbaya, kupaka ina na kuweka rasta tumieni pesa vzr mnajiachia mno angali mnajua mnamajukumu.
 
Bomu haliwezi kulipuka kwasbb kuna jeshi. Mfanyakazi ambaye hata-produce sawa sawa serikali hii inayotumia nguvu ya jeshi itamtumbua na kumshughulikia.
Jeshi litaweza kupambana vita isiyoonekana?
 
Back
Top Bottom