Technically umekubaliana na mimi kwamba, ili kupunguza madhara ya inflation kwenye purchasing power lazima mshahara upande..
Sijui kwanini umempinga mwenzako?
Tatizo haukunielewa, Mimi nimekwambia kuwa umeangalia swala la mfumuko wa bei kwa context moja, Nakuelewesha tena sasa. Mfumuko wa bei unaweza kutazamwa kwa sababu au matokeo
Mfumuko wa bei kwa mtazamo wa sababu huwa kama ifuatavyo;
Mfumuko wa bei huelezeka kama kupanda kwa jumla kwa kiwango cha bei. Kwa maneno mengine, bei za bidhaa na huduma nyingine kama vile nyumba, mavazi, chakula, usafirishaji, na mafuta lazima ziwe zinaongezeka ili mfumuko wa bei utokee katika uchumi. Ikiwa bei za aina chache za bidhaa au huduma zinaongezeka, hatuwezi kusema ni mfumuko wa bei.
Zipi ni sababu kuu zinazopelekea kutokea mfumuko wa bei kwenye context hii? Wataalamu wa uchumi wanatoa sababu mbili ambazo hutofautisha kati ya aina mbili za mfumko wa bei:
Demand-Pull na
Cost-Push. Aina zote mbili za mfumuko wa bei husababisha kuongezeka kwa kiwango cha jumla cha bei ndani ya uchumi.
- Kwa upande wa Demand-Pull, Mfumuko wa Demand-Pull hutokea wakati mahitaji ya jumla ya bidhaa na huduma katika uchumi yanaongezeka haraka zaidi kuliko uwezo wa uzalishaji wa uchumi. Sababu moja inayoweza pelekea mfumuko huu ni benki kuu inapoamua kuongeza kwa haraka pesa kwenye mzunguko na kusababisha pesa kuwa nyingi kuliko bidhaa za kununua hivyo kusababisha viwango vya zamani vya mishahara visiweze kukimu bei mpya hivyo mishahara kupanda pia kunaweza kuwa ni njia kupunguza makali ya mfumuko wa Demand-Pull. Kwa namna moja au nyingine kuongezeka kwa mishahara pia kunaweza pia kuleta mfumuko wa bei ikiwa kutakuwa hakuna ongezeko la uzarishaji wa bidhaa, hii hutokea kwa kuwa watu huwa na kibuli cha manunuzi yani “Purchasing power” wakati hakuna bidhaa nyingi za kununua hivyo itabidi market forces ziingie kwenye Darwnism, yani survival the fittest ama mwenye pesa nyingi ndio atakae nunua bidhaa na mwishowe hutokea bei mpya iliyo sukumwa na kibuli cha manunuzi.
- Mfumuko wa Cost-Push, hutokea wakati bei za malighafi zinazo tumika kwenye mchakato wa uzalishaji zinaongezeka hivyo kufasababisha bei za bidhaa kupanda. Bidhaa zinapo kuwa na bei mpya maana yake mishahara ya dhamani haiwezi kumudu mahitaji mapya ya kimanunuzi sokoni. Kuongezeka kwa mishahara ya wafanyakazi waliopo kwenye mnyororo wa uzalishaji au kuongezeka kwa bei za malighafi na usafirishaji zinaweza kuwa ni sababu za aina hii ya mfumuko wa bei. Kupanda kwa bei ya bidhaa zinazotoka nje husababisha pia aina hii ya mfumuko wa bei.
Haijarishi mfumuko umeletwa na nini ila madhara yake yanatakiwa kupungzwa kwa serikali kusimamia na kuweka viwango vya mishahara kwa wafanyakazi na bei elekezi kwenye bidhaa muhimu.
Au benki kuu kutumia
contractionary monetary policy ili kupambana na mfumko wa bei kwa kupunguza usambazaji wa pesa ndani ya uchumi na kupunguza bei za dhamana na hati fungani au kuongeza viwango vya riba.
Kwa mtazamo wa mtoa mada hapo juu inaweza pia akawa hana maana hizi za mfumuko unaotokana na sababu ama anahisi kuwa madhara ya mfumuko iliopo tunaweza kuyakabili kwa kuongeza mishahara, na hapa ndipo ambapo tunapokuja na Mfumuko wa bei kwa mtazamo wa Matokeo yake.
Mfuko wa bei kwa
mtazamo wa matokeo, hapa mfumuko wa bei huelezeka kama kupungua kwa nguvu ya manunuzi ya sarafu fulani kulingana na muda. Makadirio ya kiwango ambacho nguvu ya manunuzi kwa sarafu hupungua kunaweza kuonyeshwa katika kuongezeka kwa wastani wa bei za bidhaa na huduma fulani zilizochaguliwa katika uchumi kwa kipindi fulani cha muda. Aina hii ya mfumuko inaenda sawa kabisa na price index kwa Walaji, wauzaji wa jumla na wazarishaji ambapo kutokana na sababu nyingi tofauti zikiwemo market forces, Price index huwa inapanda na marachache sana hupunguaga. Mfumuko tunapouangalia kwa mtazamo huu unakuwa na madhara ambayo tunaweza kuyapunguza kwa muda mfupi au kwa muda mrefu.
- Kwa muda mfupi tunaweza kupunguza madhara kwa kuongeza viwango vya mishahara ya wafanyakazi kwenye sekta zote, ambapo huwa kuna madhara yake pia ikiwemo kudorola kwa uchumi na kukosekana kwa ajira.
- Kwa muda mrefu serikali kupitia benki kuu inaweza kutumia contactionary monetary policy ili kupunguza uwepo wa sarafu za nchi kwenye uchumi na soko la kimataifa. Hapa huwa kuna madhara ya muda mfupi ambapo watu watashindwa kumudu bei za vitu lakini baada ya muda bei zitashuka ili ziweze kuwafuata watumiaji, ama wazarishaji wanaweza kuboresha ufanisi kwenye mnyorolo wa uzalishaji ili waweze kuendana na hali za kifedha za watumiaji
- Pia ili kucounter check market forces za demand na supply, Serikali inapaswa kuchukuwa hatua za ziada zitakazo endana na Contactionary monetary policy ya benki kwa kuweka bei elekezi, . Njia hii ni sahihi kwa kuwa mfumuko wa bei maranyingi hutokana na Uranguzi wa wafanyabiashara kwa kupandisha bei ya vitu iwapo hakuna gharama za uzalishaji zilizo ongezeka. kwenye masoko ya nchi za kibeberu mtu anaweza kupandisha bei ya bidhaa kwakuwa tu kuna watumiaji wengi wanaihitaji kuliko uwezo wake wa kuzalisha. Serikali ikiweka sheria kali na adhabu kuwataka wafanya biashara wafuate bei elekezi itawafanya hawa wafanyabiasha wenye vitendo vya kiovu vya kiranguzi kuwekeza kwenye kutanua Scale za plant zao iliwaweze kukimu mahitaji ya soko. Ambapao faida yake huwa ni ongezeko la ajira mpya wakati wafanyabiashara wanatanua scale za uzalishaji
Sina nia ya kumuunga mkono mtoa mada wala kukuunga mkono wewe ila najaribu kuonesha kuwa nyie wote wawili mnautazama mfumuko wa bie kwa upande mmoja. Hakuna nchi isiyokuwa na Tatizo la mfumuko wa bei ila huwa tunaamua kuliongeza kwa kufuata njia za muda mfupi ilikupunduza makari yake na matokeo yake ni mfumuko unaokuwa kila siku.
My take ni kuwa tusidharau kupandisha mishahara ya watumishi ila pia tupandishe kwa kuangalia inaweza kuwa na madhara gani kwenye uchumi, pia serikali itumie vizuri nafasi yake kudhibiti uranguzi, hii nchi ni ya kijamaa hivyo mfanyabiashara hawezi kujipangia bei ili ajipatia fedha nyingi kwa kuwarangua wanyonge. Kupanda kwa bei kunapaswa kuwa kuwe cost-driven na sio demand-driven.
Hata hivyo serikali pia inapaswa kuangalia sera zake za kodi, maana hizi kodi ndio sababu za kupanda kwa bei, Ukimzidishia kodi mfanya biashara na hujampa bei elekezi ujue umemzidishia bei mwananchi kwa kuwa mfanyabiashara nayeye atapandisha bei.