Serikali tafuteni namna ya kutoa semina kwa wananchi juu ya kutambua wajibu wao.

Serikali tafuteni namna ya kutoa semina kwa wananchi juu ya kutambua wajibu wao.

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2014
Posts
3,340
Reaction score
4,659
Nimeshaona kipindi cha upigaji kura kuna matangazo mengi kwenye vyombo vya kupashana habari,mitandao ya kijamii na kupitia mikutano ya kijiji inatoa semina kwa wananchi katika umuhimu wa upigaji kura,nimeona kelele za wanasiasa wakiwaambia wahitimu kuwa wajiajiri,nimeona makongamano mengi ya kisera,chama katika kuwapasha wananchi mambo ya kisiasai.

ila sijaona serikali ikitoa elimu ya uraia

haki
wajibu
michakato

mpaka sasa sijaona mwananchi anahimizwa juu ya uwajibikaji wake katika kuipa serikali mapato ila nimeona wengi tunalaumu serikali haijengi miundombinu na kutoa huduma za jamii kwa wakati.

sijaona namna bora ya kuwaambia wananchi wanawezaje kulipa kodi zaidi ya kutoa matangazo ya dai risiti,na hakuna elimu juu ya namna gani mwananchi anaweza kuriact ikiwa hajatendewa au kutoridhishwa na huduma za serikali.

mambo mengi ni wachache tu,wenye kuyajua.
 
Hii serikali ni wahunii angalia hili kwenye bajeti iliyosomwa sijaona zile fedha za magoli ya simba au yanga
 
Back
Top Bottom